KWELI Ndege ya Rais yaonekana Dubai, leo Julai 28, 2023

KWELI Ndege ya Rais yaonekana Dubai, leo Julai 28, 2023

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia!

Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.
Screenshot_2023-07-28-22-21-52-77_8a6ce7ef6b1c5341b022b20d7fbb4b6e.jpg
Screenshot_2023-07-28-22-23-14-93_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


1690605168257.png


1690605913889.png
 
Tunachokijua
Ndege ya Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE inaelezwa kuwa ni ndege inayotumiwa na Rais wa Tanzania. Ndege hii ilinununuliwa Mwaka 2004 Wakati Rais wa Tanzania Akiwa Mhe Benjamin Mkapa na Waziri wa Fedha akiwa Mzee Mramba na Waziri wa Uchukuzi akiwa ni Professor Mark Mwandosya.

Ndege hii imesajiliwa kwa usajili wa namba 5H-ONE, Ina uwezo wa kutembea angani kwa masaa 13, Ina Tembea umbali wa kilomita 12,501 kutokua eneo moja mpaka jingine. Ina Speed ya Kilometer 941 kwa saa, ina Urefu wa mita 15.4. Ndani yake huduma zote za kiofisi na starehe zote, Ina Uwezo wa kubeba abiria 18.

Mnamo Julai 28, 2023 uliibuka uvumi katika mitandao ya kijamii ukiohoji ndege hiyo ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa kutoka kurasa za Ikulu ya Tanzania.

Mathalani, Julai 28, 2023 Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Mpinzire aliweka andiko lake akihoji suala la ndege hiyo kwenda Dubai pasina idara ya habari Ikulu utoa taarifa. Mpinzire aliandika:
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia! Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.

Pia katika ukurasa wa Twitter wa @comanchechiefIV nao ulihoji suala la ndege ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa hizo katika ukurasa wa habari wa ikulu ya Tanzania. @comanchechiefIV katika andiko hilo alisema:

Sijasikia @ikulumawasliano ikitangaza safari ya rais Dubai au Saudi Arabia. Lakini flight tracking data zinaonyesha ndege ya rais iliondoka jana ikitumia call sign TANZ01 ambayo ni rais on board. Ndege ilitoka Dubai leo na iko Saudi Arabia.
Baada ya kuwapo kwa fununu hizo JamiiForums imefatilia vyanzo mbalimbali vinavyofuatilia mienendo na safari ya ndege mbalimbali na kubaini mambo yafuatayo:

Katika Ukurasa wa FlightAware ambayo ni Kampuni ya Kidijitali inayofatilia mienendo mbalimbali ya safari za ndege duniani inaonesha mnamo Julai 28, 2023 ndege ya 5H-ONE ilikuwa nchini Dubai muda wa saa 2:35 Asubuhi.

Aidha inaonesha kuwa ndege hiyo pia iliruka muda wa 02:35 nchini Dubai na kuelekea Saudia ambako ilitua saa 03:03 Asubuhi hiyo. Tazama taarifa hiyo kwenye picha hapa chini sehemu yenye kivuli cha rangi ya njano.

1690605168257-png.2701846

Taarifa za FlightAware kuhusu ndege 5H-ONE
Nao, Flightrader24 waliojikita kuonesha mienendo ya safari mbalimbali za ndege ulimwenguni hawatofautiani na FlightAware kwani nao wanaonesha kuwa mnamo Julai 28, 2023 ndege hiyo ya Tanzania ilipaa ikitokea Dubai lakini wao hawajaonesha ilipoelekea. Tazama kielelezo hapa chini:

1690605913889-png.2701849

Taarifa za Flightrader24 kuhusu ndege 5H-ONE

Aidha, JamiiForums pia imepitia katika ukurasa wa Twitter wa @Ikulumawasiliano na ukurasa wa Instagram wa @ikulu_mawasiliano ambako wanaweka taarifa mbalimbali za safari za viongozi wa kitaifa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku hiyo ya Julai 28, 2023. JamiiForums pia imepitia kurasa Twitter na Instagram za Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku ya Julai 28, 2023.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiForums, hoja inayoeleza kuwa ndege ya 5H-ONE ilionekana Dubai mnamo Julai 28, 2023 na ikaelekea Saudia na taarifa hizo hazikuwekwa katika vyanzo rasmi vya ikulu ni ya ukweli.
Hizo tarehe mbona rais alikuwa hapa hapa nchini.

Aliyesafiri ni Waziri Mkuu hadi kwa Putin, inawezekana alienda na ndege hiyo hadi Urusi na safari hiyo iligharimiwa na Russia.

Kwa kawaida huwa tunamwona raisi akitumia ndege za ATCL ambazo ni brandy new, hatumiagi hilo dege la enzi za Mramba.
 
Kwa hiyo yale madai ya mdau wa JF ni kweli? Kuwa kaitwa na DPW kuhusu mambo yanayoendelea nchini kupinga mkataba huo?
 
Mwacheni mama aende kupumzika dubai na saudi Arabi mnampa stress za kuuza bandari munamfanya asiwe na raha Mama Rais wetu mwacheni akapumzike kidogo .
 
[emoji19]

1. Aliyekaa ni Mke wa Mwl. Nyerere. Mama Maria Nyerere.

2. Aliyemlalia kiupendo ni Mke wa Samora Machel na Nelson Mandela, anaitwa Graca Machel.

3. Mwanamke aliyevunja rekodi kuolewa na Marais wawili wa nchi mbili tofauti Afrika.

4. Alifika juzi Msasani Dar es Salaam kumpa hi shost yake Mama Maria Nyerere.

5. Nyerere ameishakufa, mke wake yupo; Samora na Mandela wameishakufa mke wao yupo.

6. Sijui wanaume wenzangu mnanielewa? Ngoja niendelee. Mkapa ameishakufa mke wake yupo. Kenyatta aliishakufa mke wake yupo.

7. Naendelea; Karume ameishakufa, mke wake yupo; Magufuli ameishakufa mke wake yupo; Sokoine aliishakufa mke wake yupo.

8. Kama bado uko hai mwanaume mwenzangu refusha maisha yako kwa kukumbuka kuishi.

9. Hii habari ya kuishi kwa mashaka ukiwaza ati siku ukifa familia yako itabaki wapi hebu achana nayo uchelewe kufa. Anza kuishi. Kula vinono.

10. Lakini pia hii tabia ya kuwalazimisha watu mkale hela zako, inakuwahisha kufa. Achana nayo. Kula kwanza ushibe.

FB_IMG_1690635816588.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom