KWELI Ndege ya Rais yaonekana Dubai, leo Julai 28, 2023

KWELI Ndege ya Rais yaonekana Dubai, leo Julai 28, 2023

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia!

Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.
Screenshot_2023-07-28-22-21-52-77_8a6ce7ef6b1c5341b022b20d7fbb4b6e.jpg
Screenshot_2023-07-28-22-23-14-93_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


1690605168257.png


1690605913889.png
 
Tunachokijua
Ndege ya Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE inaelezwa kuwa ni ndege inayotumiwa na Rais wa Tanzania. Ndege hii ilinununuliwa Mwaka 2004 Wakati Rais wa Tanzania Akiwa Mhe Benjamin Mkapa na Waziri wa Fedha akiwa Mzee Mramba na Waziri wa Uchukuzi akiwa ni Professor Mark Mwandosya.

Ndege hii imesajiliwa kwa usajili wa namba 5H-ONE, Ina uwezo wa kutembea angani kwa masaa 13, Ina Tembea umbali wa kilomita 12,501 kutokua eneo moja mpaka jingine. Ina Speed ya Kilometer 941 kwa saa, ina Urefu wa mita 15.4. Ndani yake huduma zote za kiofisi na starehe zote, Ina Uwezo wa kubeba abiria 18.

Mnamo Julai 28, 2023 uliibuka uvumi katika mitandao ya kijamii ukiohoji ndege hiyo ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa kutoka kurasa za Ikulu ya Tanzania.

Mathalani, Julai 28, 2023 Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Mpinzire aliweka andiko lake akihoji suala la ndege hiyo kwenda Dubai pasina idara ya habari Ikulu utoa taarifa. Mpinzire aliandika:
Ndege ya Rais wa Tanzania yenye usajili wa 5H-ONE imeonekana kutua Dubai na kuanza safari kuelekea Saudi Arabia! Bado idara ya habari ya Ikulu haijatoa taarifa yoyote kama Rais Samia yuko ziarani katika nchi hizo mbili za UAE na SAUD ARABIA.

Pia katika ukurasa wa Twitter wa @comanchechiefIV nao ulihoji suala la ndege ya Rais wa Tanzania kuonekana Dubai pasina kuwapo kwa taarifa hizo katika ukurasa wa habari wa ikulu ya Tanzania. @comanchechiefIV katika andiko hilo alisema:

Sijasikia @ikulumawasliano ikitangaza safari ya rais Dubai au Saudi Arabia. Lakini flight tracking data zinaonyesha ndege ya rais iliondoka jana ikitumia call sign TANZ01 ambayo ni rais on board. Ndege ilitoka Dubai leo na iko Saudi Arabia.
Baada ya kuwapo kwa fununu hizo JamiiForums imefatilia vyanzo mbalimbali vinavyofuatilia mienendo na safari ya ndege mbalimbali na kubaini mambo yafuatayo:

Katika Ukurasa wa FlightAware ambayo ni Kampuni ya Kidijitali inayofatilia mienendo mbalimbali ya safari za ndege duniani inaonesha mnamo Julai 28, 2023 ndege ya 5H-ONE ilikuwa nchini Dubai muda wa saa 2:35 Asubuhi.

Aidha inaonesha kuwa ndege hiyo pia iliruka muda wa 02:35 nchini Dubai na kuelekea Saudia ambako ilitua saa 03:03 Asubuhi hiyo. Tazama taarifa hiyo kwenye picha hapa chini sehemu yenye kivuli cha rangi ya njano.

1690605168257-png.2701846

Taarifa za FlightAware kuhusu ndege 5H-ONE
Nao, Flightrader24 waliojikita kuonesha mienendo ya safari mbalimbali za ndege ulimwenguni hawatofautiani na FlightAware kwani nao wanaonesha kuwa mnamo Julai 28, 2023 ndege hiyo ya Tanzania ilipaa ikitokea Dubai lakini wao hawajaonesha ilipoelekea. Tazama kielelezo hapa chini:

1690605913889-png.2701849

Taarifa za Flightrader24 kuhusu ndege 5H-ONE

Aidha, JamiiForums pia imepitia katika ukurasa wa Twitter wa @Ikulumawasiliano na ukurasa wa Instagram wa @ikulu_mawasiliano ambako wanaweka taarifa mbalimbali za safari za viongozi wa kitaifa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku hiyo ya Julai 28, 2023. JamiiForums pia imepitia kurasa Twitter na Instagram za Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu safari ya ndege hiyo siku ya Julai 28, 2023.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiForums, hoja inayoeleza kuwa ndege ya 5H-ONE ilionekana Dubai mnamo Julai 28, 2023 na ikaelekea Saudia na taarifa hizo hazikuwekwa katika vyanzo rasmi vya ikulu ni ya ukweli.
Bata batani la jimbo la ash-Sharqīyah
The Kingdom of Saudi Arabia

Damman, ni mji mkuu wa Jimbo la Mashariki Saudi Arabia. ash-Sharqīyah province (Arabic: المنطقة الشرقية.



Wenyeji jimbo hilo linakwenda wakiliita Al-Mintaqah ilipoenekana 5H-ONE ndege ya kiserikali ya Tanzania kwa mujibu wa tovuti za plane spotter maarufu wa kuaminika duniani na kutupiwa JamiiForums habari zake.

Miji-pacha iliyoungana kieneo Damman na Khobar ni eneo la kusifika kwa mapumziko na utalii. Jimbo lina idadi ya watu wakaazi 4 millioni. Huku wenyeji raia wa Saudia ni 3 million na wageni wakaazi 1 million wa kimataifa toka nje waishio jimboni humo .

Hivyo kwa kila watu 4 kuna wastani wa watu 3 ni wenyeji kwa mtu mmoja (1 )ni mgeni kutoka nchi za nje hivyo ni maeneo murua kabisa kubarizi kufanya utalii na matembezi ya holiday.

Damman ndipo kisima cha kwanza cha mafuta kilichimbwa nchini Saudia na kuanzia hapo utajiri wa mafuta ukaanza kuineemesha nchi hii mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani kupitia kampuni ya Aramco ambayo imewekeza vilivyo si tu katika sekta ya mafuta bali hata masuala ya kijamii kama bata la kitalii tajwa.

Tanzania inaweza kujifunza kuhusu matumizi mazuri ya maliasili za nchi kama mafuta, gesi, pwani, fukwe na utalii kutoka yanayoonekana katika jimbo hili la mashariki kabisa la Saudi Arabia.

Inside King Fahd International Airport A Saudi Aramco aircraft at Shaybah Airport in Shaybah
Dammam's King Fahd International Airport, operating since October 1999

Kutoka mji wa Damman Saudi Arabia ni kilometa chache yaani 20 unavuka bahari kupitia daraja refu kabisa unaingia Bahrain nchi nyingine tajiri kuendelea na utalii na mapumziko
1690641427480.png

The Kingdom of Bahrain
 
Kwa kawaida huwa tunamwona raisi akitumia ndege za ATCL ambazo ni brandy new, hatumiagi hilo dege la enzi za Mramba.
Flight history ya 5H ONE haionyeshi ndege hiyo, kutua kwenye viwanja Vya Karibu na St. Petersburg huko Russia mahali alipokwenda Waziri Mkuu. Labda kama hiyo CD ya flight radar ime"staki"!

 
Kuna taarifa kuwa mara nyingi weekend anakua huko
Si na sisi tujenge tuwe kama Dubai ?!.

1. Tanganyika ilipata uhuru 1961.
2. UAE (dubai) ilipata uhuru 1971.

WamewezaJe huku sisi tunashindwa ?!. Hali ya hewa yetu nzuri kuliko wao. Tunazo rasilimali nyingi kuliko wao. Tatizo letu akili na kukosa uzalendo.
 
Back
Top Bottom