na do u expect kua hzo ndege zitaenda sehemu moja kila siku???nimekwambia utalii ni moja ya sababu ziko sababu nyingi lakin nimekutolea moja tu
so unamaumivu makali sana kwasababu tz imenunua ndege brand new cash deal 7 kwa pamoja?
Sina maumivu bali sifurahii kodi yangu kutumika bila mpangilio unaoeleweka!!! Inaelekea hujui biashara na ndege, unafikiri ni sawa na biashara ya bajaj unakwenda kokote unakotaka wewe wakati wowote!!! Safari za ndege zina utaratibu wake ambao lazima ufuatwe ; huwezi kukurupuka tu leo unasema unakwenda America ukirudi unasema unakwenda China, haiko hivyo!!! Njia za angani ni lazima uwe na kibali.
Kununua ndege saba kwa kulipa cash sio sifa bali ni kutokujua mbinu za biashara; kwani hizo hizo ndege zingeweza kupatikana kwa masharti ambayo nchi ingebakiwa na fedha nyingi tu za kuwahudumia wananchi wanaoteseka na mafuriko kila mvua zinaponyesha!!
Haya ni mapungufu yanayozikumba nchi zinazoendeshwa kwa utawala wa kutokufuata sheria na katiba za nchi zao.