Ndege ya saba boeing 787 dreamliner

Ndege ya saba boeing 787 dreamliner

kuna thread hapa mkitania waKenya kwa kiswahili kibovu, hivi Denge ni nini?? Annael njoo ujibu.
 
Inasikitisha sana kuona wengine wakiiombea NCHI YETU mabaya KILA kukicha.
Sijajua wana MAANA GANI. KAMA unakumbuka ndege ilivyokamatwa Canada ilikuwa FURAHA kwao.
Yaani wanatamani nchi ibaki kuwa duni ili wapate makosa ya kujinadi majukwaani,

Rwanda iliponunua ndege mpya za kisasa walianza kuponda serikali yetu kuwa haina maana tunazidiwa mpaka na Rwanda? Leo hii wameshageuka tena ndege hazina faida yoyote Kwao.
 
Sijajua wana MAANA GANI. Kama unakumbuka awamu iliyopita walikuwa wakimtukana jk matusi ya kila aina eti serikali legelege. SASA amekuja jembe bado kulalamika hakuishi.
 
images

Dude lingine hilo
 
Sijajua wana MAANA GANI. Kama unakumbuka awamu iliyopita walikuwa wakimtukana jk matusi ya kila aina eti serikali legelege. SASA amekuja jembe bado kulalamika hakuishi.
Kiufupi hatuna wapinzani tuna waharibifu wa taifa letu, cha kushukuru ni kuwa rais anawajua vizuri ndo maana hataki kuwachekea hawa koko!!
 
Safi sana JPM wakati dude moja linaruka kuelekea uarabuni na China lingine linaruka Europe na Australia

zile nyingine mbili zinaruka South Africa na Uganda nyingine west Africa

Hizi ndogo ndio wakina Fast jet wajiandae kufunga virago sababu moto lazima uwake
 
Biashara ya ndege ni kama biashara nyingine, ni ngumu.
Kutarajia faida ndani ya miaka miwili au hata mi5 ni kutojua biashara inavyoenda.

Biashara hii inahitaji long term planning, tunaingia kwenye biashara hii tukiwa tumezungukwa na washindani, hatawezi kupata faidi siku za karibuni. Ila kwa mipango na uendeshaji mzuri tutavuka.

Wengi hatujui faida ya ndege. Kwa ufupi kabisa, faida moja wapo ya ndege ni utalii na uwekezaji.
Ukipanda Kenya Airways, lazima itue Kenya, ukipanda Ethiopian Air lazima itue Ethiopia, sasa unatarajia vipi mtalii atue Kenya then apande nyingine kuja Tanzania kutalii? Kwa nini aangaike na asibaki kutalii Kenya?
Ndege zetu zitaleta watalii moja moja. Inaweza isiwe mwaka huu ila tutafika.
Uwanja wa ndege wa Nyerere umetanuliwa sana, je tunataka ujae na ndege za Kenya, Ethiopia, Rwanda na South Africa bila kuwa na Air Tanzania?

Yaani ni sawa kuwa nyumbani kwako kuna parking kubwa nzuri ila yana paki magari ya majirani tu.
 
Back
Top Bottom