Ndege ya Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini

Ndege ya Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Tuliwaita mabeberu na majina ya kuwabeza lkn wao bado wanatujali.

Hatimaye dege letu lililokuwa limepigwa pin huko kwa mabeberu hatimaye limefunguliwa.

Asante sana wazungu kwa uwajibikaji.

Kuhusu ndege kukamatwa soma
===


Serikali imesema ndege aina ya Airbus A220 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini jana.

“Leo niko hapa kuwapa habari njema, siku chache zilizopita niliwajulisha kuna ndege yetu tulikuwa na kesi nchini Uholanzi ikakamatwa, ilikuwa chini ya mikono ya sheria. Bahati nzuri tumefanya mazungumzo na jambo limekwenda vizuri ndege yetu imerudi jana jioni iko Tanzania,” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipozungumza na waandishi wa habari leo Julai 8, 2023 mjini Arusha.

Amesema ndege hiyo inaendelea kuandaliwa ili ianze shughuli zake.

“Chuma kimerejea kiko Tanzania, tunaendelea kuimarisha shirika letu, mambo yetu yatakuwa yaanaendelea kuwa mazuri,” amesema Msigwa aliyezungumzia masuala mbalimbali, ikiwamo miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti nchini.

Mwananchi
 
Hakuna vya bure labda hewa tu

Tuseme wamemalizana kwa kulipa $165m
Screenshot_20230708_193803_Chrome~2.jpg
 
Tuliwaita mabeberu na majina ya kuwabeza lkn wao bado wanatujali.

Hatimaye dege letu lililokuwa limepigwa pin huko kwa mabeberu hatimaye limefunguliwa.

Asante sana wazungu kwa uwajibikaji.View attachment 2682344
Ahsante mama Samia kufanya vitendo bila jazba na kuirudisha ndege.

Waliokuwa hawaelewi sasa waelezwe kilichokuwepo na kilichafanyika mpaka ndege kurudi.

Mficha maradhi kifo humuumbua.

Kabudi tueleze.
Matindi tueleze.
Nape Nnauye tueleze

Au tufiche kombe mwanaharamu apite?
 
Back
Top Bottom