Kwanza mtu mwenyewe alipewa eneo ambalo lilikuwa ni makazi ya watu tayari hakulipa fidia sahihi; na hakuna la maana zaidi ya empty promises.
Japo kapewa hector 20,000 tena kwa lease ya miaka 99 yeye mwenyewe hakuwa na mpango wa kulima bali kukodisha maeneo hayo kwa wakulima wadogo wamlimie watu ambao anataka kuwatoa.
Baadhi ya donors waliojitokeza kufadhili hu mpango wa ku support G8 farming in Africa walishaanza kujitoa baada ya kuona utekelezaji una minajili ya land grabbing kuliko kuwasaidia wenyeji.
Huyo mzungu kapata hizo hela kupitia nchi wafadhili wa huo mradi kabla ya kujitoa, ni mambo ya wapiga deal wazungu huwa wanatafuta projects ambazo nchi zao zina policy ya kusaidia. Wakishapata hela wanakuja Africa wanajifanya wanaweka weka tu mambo kidogo (boshen) waonekane wanafanya kitu ili wapate hizo funds.
Ukienda Bagamoyo kabla ya kunyan’ganywa ukuti ata uwekezaji wenye thamani ya dollar 5 let alone $50 million anazodai, hizo ajira elfu 30,000 anazodai angetengeneza mpaka anaondolewa ata 100 si ajabu ajafikisha.
Haya ndio mambo yaliyokuwa yakifanyika enzi za J.K, ajabu kwenye kichwa chake anaamini alikuwa zinga moja la president.