Ndege ya Tanzania yakamatwa nje, Taifa ladaiwa bilioni 380 kwa kuvunja mkataba bila utaratibu

Enzi za Magufuli wakina Lissu walikuwa wanafurahia hizi news, sahivi wako kimya
Wewe furahia na familia yako mnatosha. Unampangia mwenzio wakati wa kufurahi unamlisha wewe?
 
Anakula Kodi na tozo zetu wanyonge na haya matoto ya viongozi wa Leo yatajuta sana Kwa ujinga wa wazi wao
Wew mbona unakulwa watoto wa watu kisa masikini acha ufala
 
Kuna vitu mtu unatakiwa kufikilia wengi hapa mnafanya kazi mfano leo amefukuzwa boss wako kesho ww umeteuliwa ukaimu pale je vitu vyote utakavyo vikuta vitakuwa sawa kuna mikataba ya hiyo ndege alisain mwenda zake now inakuja kuonyesha effect kwa DR samia then msiosoma shule mnakuja kumps lawama mama yaani sioendi kuona mtu ana msema vibaya mama yangu huyu
 
Ule mradi wa shamba la sukari Bagamoyo ACTION AID wanahusika sana kushawishi wananchi waugomee, sijui ilikuww kwa maslahi gani?
 
Hizi kesi mara nyingi zina mengi yumkini hata hujuma! Yericko ndio anabeba mapoint hapa na kitabu chake cha ujasusi wa kiuchumi.
 
Ndege imekamatwa wapi? Mbona habari yako iko kiumbea umbea?
Unajifanya chawa kumbe Mambo ya muhimu huambiwi?

NDEGE YA TANZANIA YASHIKILIWA UHOLANZI KWA DENI LA MWEKEZAJI TSH 380B.

Muwekezaji wa Kiswidi aliyeshinda tuzo ya Dola za kimarekani milioni 165 ameishawishi Mahakama ya Uholanzi kuishikilia ndege ndege ya Tanzania wakati pingamizi zikiendelea.

Mgogoro huo umetokana na kufutwa mpango wa kuendeleza mashamba ya sukari wilayani Bagamoyo umbao ulikuwa na malengo ya kuzalisha sukari kwaajili ya kuuza nje ya nchi na ethanol ili kuzalishia umeme.

Mradi huo ulipata pingamizi kutoka kwa wanaharakati wa ndani wakiwawakilisha wakulima 1300 ambao bado walikuwa wakitumia ardhi hiyo. Pia muwekezaji huyo aliilaumu Serikali ya Tanzania kushindwa kutengeneza kanuni za sekta ya sukari na kufanya ardhi hiyo kuwa na vikwazo.

Serikali mwaka 2016 ilifuta hati hiyo. Aprili, 2022 Mahakama iliipa ushindi wa tuzo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 165 Kampuni ya EcoDevelopment. June 16, ikiwa ni siku moja baada ya ICSID kupokea maombi ya Tanzania kubatilisha hukumu hiyo, Ecodevelopment ilipata ruhusa (leave) kutoka kwenye mahakama ya wilaya ya The Hague kutimiza na maamuzi ya upande mmoja kutoka kwa jaji wa Limburg yaliyotoa kibali cha kuishikilia ndege.

Ndege ya Airbus A220 ilikuwa tayari imenyimwa ruhusa ya kupaa tangu Januari kwenye kiwanja cha ndege cha Maastricht Aachen taarifa ikisema ni kutokana na matatizo kwenye injini.
 
Ndugu, nafikiri hapa wewe ndio umetafsiri vibaya. Hizo issue za GDP ni pale utapoweza ku transform rasilimali zako kuongeza tija kwenye uchumi wako lakini vita na mabeberu ni juu ya rasilimali zilizopo! GDP ni end product ambayo kwanza inabidi ushinde vita ya uchumi ili ufaidi hizo rasilimali.

Vita huko Kongo ni vita ya uchumi kaka ingawa GDP yao ni ndogo tu! Huku hatujafikia kwenye war lakini vita ya uchumi ukishindwa kuhandle carefully ndio hupelekea vita!

Ukoloni umebadilika kutoka kwenye utawala wa moja kwa moja na kugeukia utawala wa kiuchumi kwa principle ya wewe kubakia tegemezi! Ukoloni huu wa sasa ni hatari zaidi maana badala ya wazungu kutuzuia kufanya siasa na kutawala kimabavu sasa wanatumia global standards walizoweka wao kutudhibiti.

Baada ya kizazi cha akina Nyerere tumeacha kujihusisha na siasa za dunia na kuishia kupangiwa kila kitu na ukibisha unapigwa kwa standards ulizosaini mwenyewe!

Kwenye haya mambo hatupaswi kujadili na akili za Chadema wala CCM bali kupitia mwanga kidogo wa elimu tuliyonayo ili tuwe tofauti na akina Chief Mangungo.
 
Mwendazake kila alichogusa alileta hasara kwenye Nchi Kama hivi Sasa
 
Hata Mimi nimefurahi kwa sababu hii mindege inatuletea hasara na umasikini bure!
 
Hii kesi nikipewa mimi asubuhi na mapema tu nashinda na narudisha dege langu
 
Mwendeleo wa maamuzi ya kukurupuka ya Mwendazake hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…