Hakuna anaebishia hilo na kwenye moja ya post ata ni mimi nimeelezea stabilisation clause is the norm kwenye FDI.
Sasa kwakuwa kesi imesikilizwa nje ya nchi aina maana specific contract terms both expressed and implied (including Tanzania statue laws) are ignored. Moreover breach and damages are based on investment evidence, hilo shamba lilikuwa bado pori wakati hati inafutwa sasa how they justify hiyo hasara.
Tatizo kwa uongozi wa Magufuli, nikiambiwa kwamba huo mkataba ulivunjwa bila hata kuangalia uvunjaji strategically sitashangaa. Yani kama umevunjwa kwa "amri kutoka juu" tu, sitashangaa.
Na kwa sheria zetu mambo ya ardhi, rais ndiye muhifadhi wa mwisho, kwa hiyo ana haki hiyo, kikatiba.
Lakini, kama mkataba una clause inayosema kwamba kama kuna dispute, arbitration iwe mahakama za kimataifa, na mahakama za kimataifa hazitambui habari za "amri kutoka juu" kutoka serikali ya Tanzania, hapo imekula kwetu.
Tatizo si tu mikataba inavunjwa. Kuna namna ya kuvunja mikataba na kushinda kesi ya arbitration, kwa sababu unavunja mkataba kwa kutumia clauses za mkataba.
Mimi miaka fulani mzee wangu alishiriki kuongoza kutetea kesi moja kubwa sana ya arbitration ya Tanzania London, ni kati ya kesi chache ambazo Tanzania imeshinda arbitration. Alisema hii mikataba ikifikia international arbitration, ni vigumu sana nchi kushinda, kwa wakati huo, ilikuwa kama 9 times out of 10 arbitration za London Court of International Arbitration zinaishia kwa wafanyabiashara kushinda.
Lakini, kwa uvunjaji wa Magufuli ambao sasa kamrithisha Samia habari za "mkitubana kwa sehria za nje, tutawabana kwa sheria za ndani", tunavunja mikataba kijinga.
So, tatizo si tu tunavunja mikataba. Hata tunapovunja mikataba hatuvunji strategically. Inakuwa kama rais anaamini nguvu zake za kikatiba kuwa last custodian of the land zinakubalika mpaka London!
Mimi nafikiri ni wakati sasa wananchi wa Tanzania watumie international arbitration clauses katika mikataba na serikali, kuondokana na usumbufu na uonevu wa maamuzi ya "amri kutoka juu".