Ndege yapaa na kuacha chini matairi

Ndege yapaa na kuacha chini matairi

Agosti 9, 2024, Ndege aina ya
DHC-8-300 yenye usajili 5Y-SMI (Kenya) inayoendeshwa na Renegade Air kupitia WFP UNHAS, ilitengana na tairi zake kuu wakati wa kupaa kutoka Buny Airstrip huko Jonglei.

Licha ya hitilafu hiyo, ndege hiyo ilifanikiwa kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Malakal.

Abiria wote 35 na wafanyakazi walitoka salama, na hakuna ripoti ya majeruhi.
Uchunguzi bado unaendelea juu ya tukio hilo.
Kenya kwa hujuma hawajanbo, inakuwaje seti zote mbili mbele na nyuma zinyofoke kwa mpigo? Nani maarufu alikuwemo humo
 
Alafu wanasema usafiri wa anga ndio salama kushinda zote
Nandio ukweli usafiri wa anga ndio usafiri salama kuliko zote
Ndege hua hazianguki mara kwa mara ila siku ikianguka ujue kupona hata mtu shughuli
Sidhanii kama duniani inapita siku tusishuhudie ajali kadha wa kadha ila za ama ya ndege hua zakutafuta tafuta sanaa
Kama kusingekua na mabara kama afrika na asia yenye usafiri mbovu wa baharini (majini)
Nadhani usafiri wa majini ndio ungekua salama kuliko
 
Hakuna Maintenance ya kutosha kwasababu hizi Ndege za WFP na UNHCR huwa ziko Bize sana huko South Sudan.
Labda sema kingine lakini siyo kwamba hazina maintenance, SOP za UN kwenye maswala ya security ni za hali ya juu kuzidi hata za serikali! Kwa hilo serikali wakasome!
 
Labda sema kingine lakini siyo kwamba hazina maintenance, SOP za UN kwenye maswala ya security ni za hali ya juu kuzidi hata za serikali! Kwa hilo serikali wakasome!
Ninalwambia hivyo kwasababu hata mimi nisipobadilisha Wheel bearings au nidipozipa Lubrication huwa zinafeli nimefanya kazi na WFP sana ni Watu wa kawaida sana sembuse huko Jonglei South Sudan.
 
Back
Top Bottom