Ndege za ATCL na huduma ya Kahawa

Ndege za ATCL na huduma ya Kahawa

Kahawa ya kijiwe cha mchikichini inatosha. Unapanda ndege bei kubwa alafu una-mind kahawa ya shilingi 20 kikombe!
Hiyo kahawa ya kwenye kijiwe ndiyo kahawa ndugu. Sasa ya kwenye kijiwe ni proper, unapanda kwenye ndege umelipa malaki unaletewa maji ya kahawa. Huu uzembe ni mkubwa sana.
 
Kwa wasafiri wa ndege zetu za ATC, hivi mmeshawahi kuhudumiwa kinywaji cha kahawa? ni kitu cha ajabu sana kiwango cha ubora wake ni cha chini kabisa. Yaani wanahudumia chai ya kahawa au kahawa ya rangi.
Kwa kuwa Tanzania inalima na kuzalisha kahawa ya kutumia, basi shirika letu lingetumia pia kuitangaza kahawa kwa kuhudumia kahawa kwa kiwango cha kimataifa na siyo kahawa ya rangi.
Unataka quality nzuri ya kahawa au kahawa ya maziwa? Wanaoipenda kweli kahawa huinywa nyeusi bila maziwa. Na quality inatofautiana kati hii ya kwenye makopo ya kusagwa ( instant) na ile ya kusaga mwenyewe au inayobidi kutengenezwa kwa kutumia mashine maalum.

Amandla...
 
Amandla...Ninaposema kahawa ya rangi nina maana ya kahawa nyepesi. hawa ATC kahawa yao wanayohudumia haifikii kiwango cha uhudumiaji kahawa. Huwa ni kama maji yenye harufu ya kahawa. Ukisafiri waambie wakuhudumie kahawa uone.
 
Kwa wasafiri wa ndege zetu za ATC, hivi mmeshawahi kuhudumiwa kinywaji cha kahawa? ni kitu cha ajabu sana kiwango cha ubora wake ni cha chini kabisa. Yaani wanahudumia chai ya kahawa au kahawa ya rangi.
Kwa kuwa Tanzania inalima na kuzalisha kahawa ya kutumia, basi shirika letu lingetumia pia kuitangaza kahawa kwa kuhudumia kahawa kwa kiwango cha kimataifa na siyo kahawa ya rangi.
Wanachakachua hata kahawa,dah
 
swala si ku-mind. Hizi huduma kwenye ndege ni muhimu sana kwa msafiri. Mimi kwa kuwa ni mywaji mzuri wa kahawa. Ninatarajia, basi kahawa pia iandaliwe kwa ubora wake. siyo maji ya kahawa.
Punguzeni njaa jmn
Local flights nyingi 1 hr na ushee kidogo unataka ukashibie kwenye ndege
Si mle makwenu ama mgahawa wa Airport?

Binafsi huwa naishia kunywa maji ama soda tu hata korosho nakuwa sina njaa

Kula ushibe kabla ya safari afu uone kama utalaumu

Ule mlo pale ni by the way tu
 
ATC ni wajinga sana,wanatoa beer moja ukimaliza ukiuliza ya pili wanakimbia kujificha huko nyuma mimi sipandi ndege njaa.

Siku moja natoka KIA kwenda DAR na hizi pangaboi yaani masikio yanauma utafikiri umepigwa ngumi halafu sijui rubani alikuwa mwanafunzi yaani ndege ilisota wakati wa kutua abiria jasho lilitutoka.
Ha ha ha ha ha ha ha nimecheka hapo ndege kuyumba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa ndugu beer au kilevi kwenye ndege hatakiwi kupewa kuzidi kiwango cha usalama walichojiwekea maana kilevi hawawezi jua kama wewe ni heavy drinker au lightheaded.

So wanakupatia kiasi tu kama kuonja ili isije ikawa tafrani huko juu ukataka kuendesha ndege kwa nguvu.
 
Ni perception Tu...wakongwe wa kahawa ndo wanajua thamani ya kahawa ya rangi...watoto watoto na wasiojua ndo wanataka wamixiwe na hizo creamers
 
Kwa wasafiri wa ndege zetu za ATC, hivi mmeshawahi kuhudumiwa kinywaji cha kahawa? ni kitu cha ajabu sana kiwango cha ubora wake ni cha chini kabisa. Yaani wanahudumia chai ya kahawa au kahawa ya rangi.
Kwa kuwa Tanzania inalima na kuzalisha kahawa ya kutumia, basi shirika letu lingetumia pia kuitangaza kahawa kwa kuhudumia kahawa kwa kiwango cha kimataifa na siyo kahawa ya rangi.

Hii ni sawa lakini nadhani tuwashauri huku tukiwapongeza kwa jinsi wanavyo itangaza Korosho ya Tanzania. Wanakorosho nzuri sana za kiwango cha kimataifa.
 
Punguzeni njaa jmn
Local flights nyingi 1 hr na ushee kidogo unataka ukashibie kwenye ndege
Si mle makwenu ama mgahawa wa Airport?

Binafsi huwa naishia kunywa maji ama soda tu hata korosho nakuwa sina njaa

Kula ushibe kabla ya safari afu uone kama utalaumu

Ule mlo pale ni by the way tu
Hujaielewa mada. Kila kinachofanyika kwenye ndege zetu ni kujitangaza na kuitangaza nchi. ATCL haibebi wasukuma wa mwanza tu. Ni mpaka na wageni na ninaamini kwa uhudumiji huo hata international flight huduma ya kahawa ni ileile. Kwa kuwa uhudumiaji wa kahawa unautaratibu wake, ninashangaa kwa nini wenzetu wa ATCL hawauzingatii ukizingatia sisi ni walimaji na wazalishaji wakahawa?
 
swala si ku-mind. Hizi huduma kwenye ndege ni muhimu sana kwa msafiri. Mimi kwa kuwa ni mywaji mzuri wa kahawa. Ninatarajia, basi kahawa pia iandaliwe kwa ubora wake. siyo maji ya kahawa.
Kahawa bora inakuwaje mkuu
 
Kahawa bora inakuwaje mkuu
Kama si mnywaji wa kahawa huwezi kuelewa mkuu.
Nakushauri ukipata muda nenda kwenye migahawa inayouza kahawa au vile vijiwe vya kahawa utajua tofauti yake, na ni kwanini ATC na kuwa ni brand kubwa hilo hawalijai au hawalijui.
 
Zile kahawa za vijiweni zilinishinda sijui wanaweka chroloquin washenzi wale
 
Umenifurahisha sana. Hiyo ndiyo kahawa sasa. ATC siyo lazime iwe chungu sana. iwe ya kati kidogo.
Sasa yao ni maji kabisa. Ni embarrassment kwa Tanzania coffee industry.
 
Lile ni shirika la ndege jmn si kahawa

Mtu serious yeyote na kununua kahawa hatojali a one time taste in a flight
 
Kwangu si one time taste. Nina panda sana, na wakati mwingine saa 11 alfajiri. A best cup of coffee kunichangamsha ni kitu cha kwanza. Sasa unapambana na maji yaliyowekewa kahawa.
Kuhusu ATC kuwa siyo shirika la kahawa napo siyo sahihi. Ile multplier effect iko wapi? Mbona korosho yao ni top class, au hivyo vinywaji including wine ya dodoma na nzuri tu.
Kwa ufahamisho, hili ni shirika letu, na tunalishauri lijipange. Bado naamini wazalishaji wa kahawa bora wanaweza kuwasaidia ikiwa ni eneo la kutangaza na kuboresha huduma yake.
 
Back
Top Bottom