Ndege za jeshi la Israel zafanya mashambulizi makali nchini Syria kwenye miji ya Aleppo na Idlib na kuleta madhara makubwa

Ndege za jeshi la Israel zafanya mashambulizi makali nchini Syria kwenye miji ya Aleppo na Idlib na kuleta madhara makubwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Wanajeshi kadhaa wa Syria walijeruhiwa kutokana na "shambulio" la anga la Israeli karibu na mji wa Al-Safira, nje ya Aleppo na Idlib, vyombo vya habari vya serikali viliripoti mapema Jumamosi.

Shambulio hilo lililenga maeneo kadhaa vijijini nje ya Aleppo na Idlib. Jeshi la Israeli halikutoa majibu ya haraka juu ya shambulio hilo.

Soma pia: Iran imetangaza kulipiza tena Kisasi kwa Israel baada ya shambulizi huko Syria

Israel imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria kwa miaka kadhaa sasa lakini imeongeza mashambulizi hayo tangu uvamizi wa Hamas tarehe 7 Oktoba.

Source: Reuters
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa imetolewa na Serikali ya Syria no IDF wameshambulia miji husika.

Taarifa kamili tutazidi kuwaletea

Time's of Israel
Syria says several soldiers hurt, damage caused in Israeli strike in Aleppo and Idlib area

By Emanuel Fabian Follow
Today, 1:18 am
5
Syria’s state-run SANA news agency says several soldiers were wounded and damage was caused in an Israeli airstrike a short while ago in the Aleppo and Idlib area.

There is no comment from the IDF on the strike.
Hiki kitaifa kina hangaika sana aisee....kilianza huvyo hivyo kukuru kakara kikaenda kuangasha ubalozi ..na sasa tupo hapa kwenye vurugu zao na iran hajamaliza bado anahaingaika tena
 
Israel sio wajinga au vichaa ukiona wameenda kupiga kule ujue kuna kitu huenda kulikuwa na silaha nyingi zilikuwa zmetumwa kwenda kwenye uwanja wa vita kuwashambulia kwahyo zimewahiwa kabla ya kufika
Acha wahaingaieke tu maana Damascus kwa ubalozi wa Iran ulianza hivi hivi
 
Ila huo mji wa Aleppo duh! Ni wa kuhurumia; umeteseka sana huo mji. Anyway, kwa kuwa umejitolea kuficha waovu utateketea kwa uovu wake.
Umepigwa Sana Miaka Tele
 
Ulijiuliza why pia Iran wakati Iran ipo mbali sana na Israel? Syria ni jirani yao wa karibu. IDF na Mossaid sio wehu; wanajua wanacho kifanya.
Msitafute justification kwamba unajisahaulisha Israel ilitaka kumng'oa Assad ila baada ya Urusi kutia timu wakakimbia!! Hawataki amani middle east maana wanajua siku amani ikipatikana waarabu watakaa meza moja na kupatana!!!

A peaceful middle east is a deathbed of Israel, knowingly so it has to be avoided at any cost!!
 
Amani middle east inapatikana vipi? Tangu lini mashiha na massuni wakaishi kwa amani?

Hebu fafanua hilo kwanza na usisahau kugusia pia nani atakuwa mmiliki wa mji wa macca na madina baada ya hao jamaa kuamua kuishi kwa amani
 
Ndio hivyo wanapambana na magaidi wa kiislam wanaofadhiliwa na makafiri wa Iran.
 
Makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa na Iran, yapo Syria, Iraq, Lebanon, Yemen na Gaza.

Silaha zote za kundi la kigaidi la Hezbollah, zinapitia Syria.
Gaidi kwa mtizamo wako,ila dunia inawafahamu hao kama freedom fighters.
Sasa wewe na kizazi chako kizima sidhani kama mnamfikia hata waziri wa haki za binadam wa Hispania ambaye anawatambua hao kama freedom fighters apart from that wewe ni brainwashed empty headed.
 
Hiki kitaifa kina hangaika sana aisee....kilianza huvyo hivyo kukuru kakara kikaenda kuangasha ubalozi ..na sasa tupo hapa kwenye vurugu zao na iran hajamaliza bado anahaingaika tena
Hujui kuwa Iran anataka ifuta Israel?
 
Truely definition of IDF being the best army in the world.

JWTZ safari yetu ni ndefu sana.
 
Makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa na Iran, yapo Syria, Iraq, Lebanon, Yemen na Gaza.

Silaha zote za kundi la kigaidi la Hezbollah, zinapitia Syria.
Umempa za uso.
 
Back
Top Bottom