Ndege zetu ziko wapi, Kwenye kusafirisha mazao kwenda Ulaya?

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,313
Reaction score
6,895
Hivi majuzi Kenya walionekana wakisafirisha mbogamboga na matunda kuelekea kwenye masoko ya Ulaya kwa kubadili matumizi ya ndege za aboria kuweza kubeba mizigo kufuatia upungufu wa abiria.

Hatua ya kupata masoko hayo imekuja baada ya mataifa mengi kusimamisha shughuli kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona COVID-19.

Hapa nyumbani napo hatukubaki nyuma baada ya Naibu waziri Hussein Bashe kupost picha ya Waziri Wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa kwenye ndege akipakia mizigo. Na tani 37 za mazao zikisafirishwa kwenga Ubeligiji.

Jana shirika la ndege la Ethiopia limeweka taarifa ya kupata tenda ya kusafirisha mazao kutoka Tanzania kuelekea nchi za Ulaya.

Swali la msingi ni je ndege zetu tulizogharamikia mabillioni ya shilingi ziko wapi?
Ni mbovu? Hazina vibali? Au ni kukosa maarifa kwa viongozi?

Je, huu sio wakati muafaka wa ndege zetu kufanya kazi ya kuitambulisha nchi katika safari za anga?

Waliokuwa wanapinga mradi wa ndege je serikali inachochote cha kujitetea baada ya aibu hii?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwnye twitter Ethiopia Airlines wamesema kuwa wameidhinishwa kupeleka matunda na mboga mboga huko ulaya kutokea tanzania
 
Biashara ya mbogamboga ni mikataba nafikiri
Kenya ni lazima walete Ulaya kwa sababu ni biashara ya muda mrefu na inahitajika
Hatuwezi kujua wanalipanaje kwa sasa kama ni kati ya serikali ya [emoji636] na wafanyabiashara hatujui ila ni lazima tupate nyanya jamani
Tukipakia holela yataishia kwenye skip

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ikiwezekana zimsafirishe hata aliyezinunua

Seek respect, not attention. It lasts longer
 
Mengine sio muhimu kwa sasa tupambane na corona kwanza
Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…