Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Midege mingine mitano ya nini?
👇
--
Serikali inakusudia kununua ndege mpya tano katika mwaka wa fedha 2022/23 ikiwemo ndege moja ya mizigo, idadi ambayo itaifanya serikali kuwa na jumla ya ndege 16.
Tayari serikali imetenga Sh353 bilioni katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kugharamia masuala mbalimbali katika sekta ya usafiri wa anga ikiwemo ununuzi wa ndege hizo.
Akizungumzia utekelezaji wa bajeti katika wizara yake mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema hadi kufikia Mei 2022, Serikali ilikamilisha ununuzi wa ndege tatu mpya na kuzikabidhi kwa Shirika la Ndege nchini (ATCL) na kuendelea kutumika.
Alizitaja ndege hizo kuwa ni Dash 8 Q400 moja yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na ndege mbili aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.
Profesa Mbarawa alisema kuongezeka kwa ndege hizo kumeifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege mpya 11 ikilinganishwa na ndege nane zilizokuwepo mwaka 2020/2021.
Waziri huyo alisema malengo ya mwaka wa fedha 2022/23 ni malipo ya ununuzi wa ndege tano mpya ambapo ndege moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F na ndege moja aina ya Dash 8 Q400.
“Tumepanga kugharamia mahitaji ya awali ya uendeshaji wa ndege tano ambazo ni Boeing 787 – 8, Boeing 737- 9 mbili (2), Boeing 767 - 300F na Dash 8 Q400 (1). Pia, kununua vifaa vya kuhudumia ndege na abiria viwanjani,” alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kwamba wamepanga kuendelea na ukarabati na ununuzi wa vifaa vya karakana za matengenezo ya ndege (Hangar) za Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Profesa Mbarawa alibainisha Mipango mingine ya wizara yake mwaka huu kuwa ni ukarabati wa jengo la ofisi za makao makuu ya ATCL lililopo kiwanja cha ndege cha JNIA Terminal I.
Alisema serikali itaendelea na ukarabati wa nyumba 38 zilizopo KIA, kujenga eneo la mafunzo ya awali kwa wana anga, kuendelea kulipa madeni ya Shirika na kukarabati na kujenga majengo ya kuhifadhia mizigo katika viwanja vya ndege vya JNIA, KIA na Songwe.
Kuhusu treni ya kisasa, Profesa Mbarawa alisema Septemba mwaka huu itafanyiwa majaribio na baada ya hapo watatoa taarifa rasmi baadaye kuhusu kuanza kutumika kwa usafiri huo katika kipande cha Dar es Salaam - Morogoro.
Chanzo: Mwananchi