Ndio, Rais anaifungua nchi lakini wapigaji (wafanyabiashara/wanasiasa) nao wanaupiga mwingi sana

tamsana

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
3,842
Reaction score
8,266
Salam wadau.

Kwa kweli kama wanavyosema 'mama anaupiga mwingi' hatukatai tunaweza tukakubaliana na hoja zao lakini tangu mama ashike hatamu, wafanyabiashara/wanasiasa hawako nyuma, wanaupiga mwingi sana.

Mfano mdogo tu ni gharama za ujenzi jinsi zinavyopaa mathalani saruji.

Kama viwanda vya ndani vimeshishwa kukidhi mahitaji ya soko, kwanini tusiruhusu majirani walete saruji yao ili bidhaa hii muhimu kwenye ujenzi isipande sana?

Ni kweli tunaweza kusema awamu ya 4 ilikuwa na upigaji sana lakini gharama za vifaa vya ujenzi zilikuwa nafuu kwa wananchi wote.

#Kaziiendelee
 
Kundi linaloongoza kumchukia mama ni wale ambao wameridhika na umasikini hawataki kujishughulisha, kile kipindi walifurahi sana watu hawaajiriki, watu wanafunga biashara, n.k.

Kwa upepo huu ifikapo 2023 mzunguko wa pesa utakuwa mkubwa sana.

Penye pesa lazima dili ziwepo, au mmesahau ile Trilioni 1.5 ilivyoibulowa CAG akafutwa kazi ili asifichue
 
Hii ni kama awamu ya 4 tu. Ile awamu Nchi haikuwa na heshima kabisa, mataifa mengine yalitudharau sana.

Awamu ya 3 ya Hayati Ben na awamu ya 5 ya Hayati JPM zilileta heshima sana kwenye Nchi hii, hapakuwa na uswahili swahili na kufanya mambo kienyeji enyeji. Viongozi hawa walikuwa na vision na walikuwa na principles zenye faida kwa Taifa kwa vizazi vijavyo.
 
Kundi linaloongoza kumchukia mama ni wale ambao wameridhika na umasikini hawataki kujishughulisha, kile kipindi walifurahi sana watu hawaajiriki, watu wanafunga biashara, n.k.

Kwa upepo huu ifikapo 2023 mzunguko wa pesa utakuwa mkubwa sana.

Penye pesa lazima dili ziwepo, au mmesahau ile Trilioni 1.5 ilivyoibulowa CAG akafutwa kazi ili asifichue
Utoko huu, ondoa
 
Back
Top Bottom