Panapoukweli uwongo hujitenga.
Ndio maana mihimili mikuu ya dora ni mitatu nayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Mihimili hii kikanuni na ukweli inapaswa kufanya kazi kwa uhuru, bila kuingiliana ila hufan ya kazi kwa kutegemeana. Kamwe mhimili mmoja usingilie mihimili mingine huo ndo ukweli.
Kuruhusu muhimili mmoja kumeza mihimili mingine mbeleni tatizo ni lazima litatokea.
Wakati wa serikali ya awamu ya tano Bunge chini ya Spika huyuhuyu liliruhusu mhimili wake umezwe na serikali.
Lilipitisha kila sheria au miswada yote iliyoletwa nna serikali kwa kelele na vifijo bila kujua madhara yake mbeleni, Bunge likawa kama dodoki kupitisha uchafu wotewote ulioletwa bungeni bila kujadili kwa marefu na mapana.
Bunge hilihili likaruhusu mazumbukuu kama Livingstone Lusinde ambaye alikuwa Mbunge wa Mtera na Joseph Kasheku(Msukuma) Mbunge wa Geita wakawa ndio wadadavuaji wa miswada na kuwapuuza kabisa wabunge wasomi kama Sosipeter Mhongo Mbunge wa Butiama.
Wakapitisha haraka sheria ya kuwawekea kinga Spika na wengine wasishitakiwe pindi wamalizapo mihula yao sijui waliona mbele kuna nini.
Leo hii Spika ndo wa kusema eti Bunge haliisimamii vizuri serikali ndiyo maana deni la taifa limepaa hadi kufikia Sh Tillion 70, kweli! Wakati wanamwajibisha CAG kinyume na taratibu hawakuyaoha haya?
Kauli hii kwa rugha rahisi ni kama mkuu wa gereza anasema hatukufunga mlango ndio maana mfungwa wa uhaini alitoroka, ni nini kitafuata si Mkuu wa gereza kuwajibika?
Sasa kwa kauli hiyo ambayo inatosha kabisa Spika kuhojiwa mbele ya Kamati haki, kinga na madaraka ya bunge? Mtampelekaje na hali mumemuwekea kinga?
Ndiyo maana walipitisha sheria ya spika kuwa kinga ya kutokushitakiwa, kumbeee!
Wamuache Rais afanye kazi zake za ki-Urais.