Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Najua jamaa alikuita kwenye ile kamati yake enzi za utukufu wake, lakini asamehewe tu kama alivyoomba. Amekosa jamani, amekosa sana, wazanzibari ..... I mean watanzania tumsamehe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee ! Ya kuambiwa alama ya kuuliza haikuonekana? Ha ha haaa! Muacheni ndugu yetu Pascal.Analipiza kisasi
KaribuTikaribishane humo kambini basiii.[emoji125]
.
Je, Wajua Kuna Msamaha wa Kweli, Msamaha Batili na Msamaha Batilifu?
Sasa kama ilivyo kwenye ndoa, si wengi wanaojua kuwa kwenye msamaha, pia kuna msamaha wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu.
Hata msamaha huu ni msamaha batili!, kwasababu kilichosemwa ni kitu cha ukweli kabisa, kimesemwa kwa kudhamiriwa, kitendo cha kusema it was a joke, ni uongo just to pay lip servicesWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba radhi wananchi na wapenda demokrasia nchini kutokana na kauli aliyoitoa kuwa si lazima CCM ishinde kura kwenye boksi, bali kuna njia nyingine zikiwemo alizosema za haramu.
Akizungumza kupitia video aliyorekodi, leo Jumatano Julai 17, 2024 Nape ameomba radhi wote walikerwa na kauli yake.
“Nimeuona mjadala kwenye mitandao, lakini kama nilivyosema kauli ile ilikuwa utani lakini naona umekuwa mjadala mrefu wakati huu kwa sababu tunaelekea katikia uchaguzi. Nawapa pole ambao wamesumbuliwa na kuteseka na huu mjadala, nawapa pole na naomba radhi, nasisitiza haikuwa serious,”amesema Nape.
Nape aliyewahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, alitoa kauli hiyo iliyoibua mjadala juzi Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi.
Muktadha wa kauli hiyo ilikuwa ni kuwahakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025, Nape ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema:
“Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi tu mkishamaliza, unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea,” alisema.
Kauli hiyo ya Nape, ilipingwa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ambaye alisema kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.
“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” alisema Makalla.
Hii si mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli tata zenye kuzua mjadala katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, hata Juni 2015, akiwa ziarani Sengerema alisema “CCM ingeshinda uchaguzi mwaka huo hata kwa bao la mkono.”
Pia soma
Pole wahanga wote wa kauli hizi na jua hata aliyekuwa mbunge tarajiwa wa kawe alikuwa mhanga pengine wa bao la mkono ama kunyolewa kichwa na waishimiwa wajumbe.Hata msamaha huu ni msamaha batili!, kwasababu kilichosemwa ni kitu cha ukweli kabisa, kimesemwa kwa kudhamiriwa, kitendo cha kusema it was a joke, ni uongo just to pay lip services
P
Kwenye kura za maoni za CCM, kule hakuna bao la mkono, kule ni kila mbuzi kula urefu wa kamba yake kuwafikia wajumbe. Mimi ni Nyerere type, siku reach out kwa mjumbe hata mmoja kwa kumshika mkono!, matokeo yake, niliambulia kura moja, ya mtu aliyeshikwa mkono na wengine!.Pole wahanga wote wa kauli hizi na jua hata aliyekuwa mbunge tarajiwa wa kawe alikuwa mhanga pengine wa bao la mkono ama kunyolewa kichwa na waishimiwa wajumbe.