Ndoa hapana! Sitaki

Ndoa hapana! Sitaki

Ipo philosophy moja kuna rafiki yangu humu jf aliwahi kuniambia kwamba ukienda kutoa posa halafu utajiwe kutoa mahari kubwa hiyo huwa ni mbinu ya kukufukuza kama endapo familia haijakupenda

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilikwenda kuchumbia mahali fulani...majibu yakatoka nikaambiwa nipeleke milioni mbili..,nimejitafakari aisee ni hapana sijajua wazazi wa Binti watanifikiria vipi ...ila watanisamehe tu.

Kwanza naenda kumnunua mtu...pesa inatoka hapo,pili natakiwa niwe namhudumia kwa kila kitu nikiwa naye nayo ni pesa hio,tatu Mwanamke atakuja kunibana aisee nishazoea kulala pekeangu,nne nahofia tukiachana nitapoteza hata hivi vichache nilivonavyo...mwisho kabisa Mwanamke nimemuona mtu wa lawamalawama sana...kwanza ni ngenye ndio zilisababisha harakaharaka nichumbie

Binafsi nikifikisha miaka 40 labda ndio nifikirie kuoa kwa saivi najitafuta kwanza nahitaji niimarike kiuchumi

Mikakati ninayokuja nayo

1.naacha pombe,sigara
2.nakuwa mtu wa ibada na kusoma vitabu.
3.nakuwa mchumi na mbahili lakini nataka nifanye kazi kwa bidii sana
4.naweka akiba
5.nakuwa mtu wa kujipenda na kupendeza kuvaa vizuri
6.mbinafsi.

Note:ndoa ni muhimu lakini sio lazima
Kuna tapeli mmoja aliimba HATAKI NDOA ANATAKA MIGUU YA KUKU NA SODA.
 
Ipo philosophy moja kuna rafiki yangu humu jf aliwahi kuniambia kwamba ukienda kutoa posa halafu utajiwe kutoa mahari kubwa hiyo huwa ni mbinu ya kukufukuza kama endapo familia haijakupenda
Wasukuma huwa wanatumia mbinu hiyo. Kama hawakutaki unaweza kuambiwa utoe hata ng'ombe 70. Wakipunguza sana 65. Hapo washenga ulowatuma watajua kuwa hapa hatutakiwi. Halafu wakati huo huo chakula ni dagaa tu na ugali.

Dalili ya kwanza kwamba mmekubaliwa mtakuta mbuzi au kondoo keshala kisu tayari...na pombe ziko stendibai. Na negotiations hazitakuwa ngumu sana. Hapo mnajua hapa tumepokelewa vyema!
 
Back
Top Bottom