Hiyo ndoa haivunjwi kwa sababu haijawahi kuwepo kwa sababu wakati wanafunga ndoa hiyo mwanaume alikuwa na kizuizi cha ndoa: kizuizi cha kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa (impotency). Kwa kuwa huyo bwana alikuwa hivo, "ndoa"hiyo haikuwa valid, japo madhehebu (rites) ya kufunga ndoa yalifanyika.Makubaliano yao maharusi hayakuzaa ndoa kwa sababu ya hicho kizuizi, hivyo ndoa hiyo ni null and void.
Na kwa kuwa ni null and void ndoa hiyo haivunjwi kwa sababu haijawahi kuwepo.Kumbe inatangazwa rasmi na Kanisa kuwa ilikuwa batili baada ya kuthibitisha kwa mahojiano na wanandoa, na wale waliokuwa wanawajua wanandoa na hasa bwana harusi ambaye ndiyo mwenye tatizo. Na katika hatua hii ya kutafuta ushahidi wa kuwepo kizuizi hiki cha impotency lazima madakatari wamchunguze jamaa na kutoa ripoti kwa maandishi kwa mahakama ya kanisa. Mahakama ya kanisa ikiridhishwa na ushahidi usio na shaka basi itatangaza rasmi (declare) kwamba ndoa hiyo ilikuwa null and void; na hivo kumpa ruhusa bibi harusi kufunga ndoa na mwanaume mwingine.
Kwa sasa si lazima bibi harusi aendelee kukaa na bwana harusi. Aweza kwenda kwao, yaani wakatengana mpaka kesi itakapokuwa imehukumiwa. Na kwa kawaida kes ihizo huchukua muda mrefu ndo hukumu itolewe. Kumbe hawezi muathirika kukaa tu na mwenzake wakati hakuna kinachofanyika. Lakini yafaa pia aombe ushauri wamchungaji wake.