Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kumekuwa na Maandiko kadhaa na mijadala kadhaaa kuhusiana na umuhimu wa ndoa na wengine wakisimamia katika kampeni Yao ya Kataa ndoa,ndoa ni utapeli na kadhalika.
ETUGRUL BEY nae ameona achangie kidogo katika Jambo hili, nianze Kwa kusema Kwanza wale ambao wanakataa ndoa hawakatai Bila sababu,Ila kuna mambo ambayo wanayaona hayako Sawa katika ndoa ndio mpaka yanawapelekea kuamini kuwa ndoa ni gareza,maumivu,mateso,usaliti na ndio chanzo cha mabalaa mbali mbali ikiwemo kutoana Uhai.
Lakini kila Jambo lina changamoto zake hapa duniani,na wakati mwingine changamoto hizo ndio sehemu ya kutufanya kukua na kukomaa zaidi.
Ndoa ndiyo ambayo inampa mwanadamu hadhi na heshima hapa duniani tofauti na viumbe wengine,viumbe wote wanasex au wanaingiliana, lakini Mwenyezi Mungu amemtofautisha mwanadamu na viumbe wengine Kwa kujaaliwa kuwepo Kwa ndoa. Kwani ndoa ndio takaso Bora na linafanya kitendo kile cha kuingiliana kiwe tofauti na viumbe wengine.
Kama hatufungamani na ndoa na kuendelea kuingiliana nje ya mpango wa Mungu basi hakika hatuna tofauti yoyote na wanyama,ingawa kimwonekano sio kama wanyama Ila kitabia ni kama wanyama.
Pamoja na changamoto mbali mbali ambazo zipo katika ndoa,lakini bado ndoa itabakia kuwa taasisi imara ya kuendeleza kizazi cha mwanadamu katika njia halali kabisa ambayo inampendeza Mungu,kwahiyo vyovyote itakavyokuwa bado ndoa ina umuhimu mkubwa Sana.
Wakataa ndoa Kwa mtazamo wangu ni watu ambao hawana Imani na Mungu kabisa,kwasababu kama ndoa ndio mpango ambao amewatayarishia wanadamu waufuate na njia salama Kwa Maisha Yao hapa duniani na kesho siku ya hesabu je wewe ni nani usie na hofu ya Mungu wako mpaka ukatae kuwepo Kwa ndoa?
Mtu yoyote ambaye ana Imani juu ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi anajua na kuamini kabisa njia pekee ya kukwepa dhambi ya zinaa ni kuoa au kuolewa Tu. Sasa ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kukataa ndoa ujue huyo hamjui Mungu na hajui hatima yake itakuwaje baada ya kumaliza Mda wake hapa duniani.
Hawa ni WA kuwahurumia Sana na bahati mbaya zaidi kuna watu wengine ambao nao kichwa kichwa wanaingia katika mtego huo huo ima Kwa ushabiki Tu au kwakujua au kutokujua,naomba niwazindue Kwa kuwaambia akili za kuambiwa changanya na zako,mwisho wa siku kila mtu atavuna anacho panda,hapo hakutakuwa na Sisi bali utakuwa wewe Tu na Mola wako.
Hoja inaweza kuja mbona kuna watu wameoa na bado wanazini? Hayo ni makosa mengine ambayo bado mwanadamu anaendelea kumkosea Mola wake. Tunapo kusudia kuoa INA maana sasa tunaachana na zinaa na kuwa katika ibada ya ndoa takatifu,tunakuwa katika njia ambayo inampendeza Mola wetu.
Na ndoa ni ibada, kwasababu ibada ni Matendo mazuri au maneno mazuri ambayo yanampendeza Allah, na unapata thawabu Kwa Jambo lolote la ibada. Kwa mfano unaposex na mumeo au mkeo ujue unapata thawabu,kwasababu unafanya kitendo ambacho kinampendeza Mungu,Maswahaba walipo sikia hili Kwa Mtume (s.a.w) walistaajabu Sana,wakamuuliza Nabii "yaani tunastarehe wenyewe na wake zetu na bado tunapata thawabu"?
Nabii akawajibu " vipi kama mngezini je msingeandikiwa madhambi"? Wakajibu ndio tungeandikiwa madhambi basi akawaambia na anayemwingilia mkewe WA halali basi anapata thawabu. Naam mpaka hapo naona umepata picha ni Kwa kiasi gani ndoa ni Jambo la muhimu na la kiibada.
Kwa mfano Kwa Sisi Waislamu, ndoa ni nusu ya Dini,Kwa maana ambaye ameoa basi ana asilimia 50 ya Dini na 50 iliyobaki ni kufanya ibada nyingine mbali mbali,kwasababu kwenye ndoa kunapatikana familia ambayo inatakiwa iishi katika misingi ya Dini na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu,kifupi ndoa ni taasisi ambayo ina mambo mengi ndani yake ambayo mume na mke watakuja kuulizwa je walisimamia vipi malezi ya watoto wao na mambo kadhaa WA kadhaa.
Je tufanye nini ili taasisi ya ndoa iwe imara na hatimaye ifikie malengo yake.
Kwanza nianze na vigezo vinne ambavyo ndio sababu ya kuoa au kuolewa.
1) Tunaoa kutokana na uzuri WA mhusika - uzuri unao zungumziwa hapa ni uzur ambao wewe mhusika unakupendeza Kwa mwanamke wako au mwanaume wako,kwamba Oa mwanamke ambaye hata ukimtazama basi nafsi yako inafurahi/na mwanamke vile vile.
2) Tunaoa kutokana na Nasabu/Ukoo husika - nenda kaoe kwenye nasabu au ukoo ambao unafahamika Tabia zake na mwenendo wake,kwani kuna koo nyingine ni mtihani Sana,huko maugomvi na mabalaa ni sehemu ya Maisha Yao,na Tabia huwa inafuata mkondo.
3) Tunaoa kutokana na Mali - wakati mwingine tunaenda kuoa kutokana na Mali au kuolewa kutokana na Mali za mhusika,sasa hapa ndio Pana mitihani Sana,unajua kabisa Fulani humpendi lkn unafuata Mali zake au hela zake,ndio baadae hela au Mali zikikata balaa linaanza.
4) Na mwisho Tunaoa kutokana na Dini ya mhusika - hapa ndio penye Jambo la muhimu Sana,Yani cheza kote lakini hapa usikosee, hakika mwenye hofu na Imani ya Mungu mara nyingi ni mtu Bora Sana katika kuanzisha nae Maisha ya ndoa. Kwani huyu atakulindia Mali yako,atajihifadhi na machafu Kwa maana hata zini au kuchepuka hata ukiwa mbali nae,na hata malezi ya watoto wako yatakuwa katika mikono salama kabisa.
Watu wengi hapa ndio tunafeli na ndio maana ndoa zimekuwa mitihani kila kukicha,tunakutana huko vyuoni,makazini na mabarabarani bila hata kuangalia vigezo muhimu ambavyo vingeweza kutusaidia kuwa na ndoa imara huko mbeleni.
Mifano tunayo huko zamani wazazi walikuwa Makini Sana katika kuangalia wachumba sahihi Kwa watoto wao na hata ndoa zao zilidumu Sana kwakuwa zilifuata mifumo sahihi ya kutambua mtu sahihi na kufunga ndoa sahihi.
Nashauri kabla ya kueneza kampeni yako ya Kataa ndoa,sijui ndoa ni utapeli sijui ndoa ni batili ebu tafakari hayo niliyoandika hapo na fanya tathimini na uone tatizo liko wapi.
Ni hayo Tu!
baby zu
Mademoiselle