Ndoa humpa hadhi na heshima mwanadamu

Ndoa humpa hadhi na heshima mwanadamu

Leo dereva wetu ameniambia weekend hii anaachana rasmi na mkewe, jamaa anasema kapambana sana kuiokoa ndoa yake lkn imeshindikana.

Wamekubaliana mke ataondoka na mtoto pamoja na vitu vyote vya ndani, hivyo jamaa ataanza upya kama mfungwa aliyetoka jela

Ushauri pekee niliompa..KIJANA KATAA NDOA
Ni Kama kufa na kuzaliwa tu. hatuwezi kuto owa sababu changamoto alizopata nguru mbili, mbona hujandika zuri wanayofanyiana wana ndoa.
 
Sidhani kama hii mijadala ina umuhimu sana, ila acha niseme chochote. Wanaokataa ndoa, wana sababu zao so waendelee kukataa, tunaokubali tuna Imani zetu hivyo tuendelee kuoa ama kuolewa. Kila mmoja achague fungu lake.

Kama ndoa ni nzuri basi tuache zijitetee zenyewe, kama ubachela ni mzuri tuache ujitetee wenyewe. Kizuri kijiuze kibaya kijitembeze. Kama ndoa ni nzuri tutaona results kupitia maisha yetu na kama ubachela mzuri tutaona evidence kupitia maisha ya team kataa ndoa. Kila mtu abaki kwenye lane yake.

Kwanini kupiga kelele za kukubali ama kukataa for what? Muda wetu hapa duniani ni mchache sana kubishana kwenye mambo yasiyo na faida. Kila mtu aonavyo vyema na afanye, what I know nataka kuliishi kusudi ambalo Mungu ameniumbia nilifanye for his Glory. Sitakaa nimpersuade mtu mzima mwenye uwezo wa kuchagua aoe ama kuolewa. Hakuna asiyejua ndoa ni nini.

Katika Imani yangu, nimeambiwa nitubu na kuiamini Injili na pia nizae matunda yapasanayo na toba. Hii mijadala sioni kama ina tija sana maana imekua kelele zisizo na faida. Asietaka ndoa, aendelee kuruka majoka. Anaetaka ndoa aende akaoe ama kuolewa. Imeisha iyo..we mooove!!
Kataa ndoa mkuu kenya wambadili sheria za ndoa kwa kelele kma hiz
 
Ma shaa allah, hakika nami naona wenye kukataa ndoa hawana hofu na mola wao (allah awaongoze wao na sisi pia)
Hii kampeni yao ingeendana na kusema hata hao wanawake wasiwale🤣🤣🤣 ingekua bora lkn wao wanakataa ndoa na wanawakr wanawataka, hapa ndipo swala la msingi linakuja kua haja zao zinahitaji kukidhiwa,
Je kwa mwenye kumhofu Mungu ajiulizi vipi atakidhi haja zake matamanio? Hakika upo sahihi kumfananisha mtu huyu na mnyama kwani amepewe utashi na bado ameshindwa kuutumia
Ndoa ni baraka, ndoa ni sababu ya kuzidishiea rizki, ndoa ni ibada, ndoa ni utulivu, allah ajalir wote wenye kutaka ndoa wapate wenza wema watakao kua vitulizo vya nafso zao na waliopo kwenye ndoa awazidishie upendo ana amani ktk ndoa zao
Note, changamoto zipo kwenye ndoa lkn twapaswa kujua nan twatakiwa kumtaka msaada ktk changamoto hizi
Subra ni nguzo pia ktk ndoa, unyenyekevu huleta maelewano pia
 
Ma shaa allah, hakika nami naona wenye kukataa ndoa hawana hofu na mola wao (allah awaongoze wao na sisi pia)
Hii kampeni yao ingeendana na kusema hata hao wanawake wasiwale🤣🤣🤣 ingekua bora lkn wao wanakataa ndoa na wanawakr wanawataka, hapa ndipo swala la msingi linakuja kua haja zao zinahitaji kukidhiwa,
Je kwa mwenye kumhofu Mungu ajiulizi vipi atakidhi haja zake matamanio? Hakika upo sahihi kumfananisha mtu huyu na mnyama kwani amepewe utashi na bado ameshindwa kuutumia
Ndoa ni baraka, ndoa ni sababu ya kuzidishiea rizki, ndoa ni ibada, ndoa ni utulivu, allah ajalir wote wenye kutaka ndoa wapate wenza wema watakao kua vitulizo vya nafso zao na waliopo kwenye ndoa awazidishie upendo ana amani ktk ndoa zao
Note, changamoto zipo kwenye ndoa lkn twapaswa kujua nan twatakiwa kumtaka msaada ktk changamoto hizi
Subra ni nguzo pia ktk ndoa, unyenyekevu huleta maelewano pia
Mashallah baby zu hakika umenena vyema sana,

Kama ulivyosema kama kweli hawataki ndoa basi wakatae kuwala pia hapo ndio tutajua kweli kampeni Yao INA mashiko vinginevyo ni matapeli kama matapeli wengine tu
 
Ndoa ni kwa ajili ya masikini na mbumbumbu pekee ili wakikutana waungeunge mwana maisha yaende.

Sisi matajiri wacha tuendelee kusasambua mbususu za kila mwanamke tumtakae maana pesa ipo!!!

Yaani na pesa zangu hizi atokee mpuuzi mmoja anipangie muda wa kurudi nyumbani?

Yaani na pesa zangu hizi utokee ukoo mmoja wa kipumbavu unipangie mahari na jinsi ya kumtunza binti yao?

Yaani na pesa zangu hizi atokee mpuuzi mmoja anipande kichwani halafu nimchekeechekee tu kwa kisingizio cha she's my wife?


Yaani na pesa zangu hizi atokee mpuuzi mmoja atake kulifaidi jasho langu kizembe kwa kugawana mali zangu pasu kwa pasu kisa tumeachana??

The word "Marriage" is nowhere to be found in my dictionary.

Chief

Sasa wewe tajir gani ambaye mahari inakuwa tatizo kwako?

Na pili Kwa uzoefu wangu WA kusoma na kuona ndoa za wenye hela mara nyingi huwa hazina changamoto kama ndoa za maskini

Sasa vigezo vya kuwa na ndoa yenye furaha na Amani unavyo kwakuwa Una hela mingi

Je unakwama wapi chief?
 
Kumekuwa na Maandiko kadhaa na mijadala kadhaaa kuhusiana na umuhimu wa ndoa na wengine wakisimamia katika kampeni Yao ya Kataa ndoa,ndoa ni utapeli na kadhalika.

ETUGRUL BEY nae ameona achangie kidogo katika Jambo hili, nianze Kwa kusema Kwanza wale ambao wanakataa ndoa hawakatai Bila sababu,Ila kuna mambo ambayo wanayaona hayako Sawa katika ndoa ndio mpaka yanawapelekea kuamini kuwa ndoa ni gareza,maumivu,mateso,usaliti na ndio chanzo cha mabalaa mbali mbali ikiwemo kutoana Uhai.

Lakini kila Jambo lina changamoto zake hapa duniani,na wakati mwingine changamoto hizo ndio sehemu ya kutufanya kukua na kukomaa zaidi.

Ndoa ndiyo ambayo inampa mwanadamu hadhi na heshima hapa duniani tofauti na viumbe wengine,viumbe wote wanasex au wanaingiliana, lakini Mwenyezi Mungu amemtofautisha mwanadamu na viumbe wengine Kwa kujaaliwa kuwepo Kwa ndoa. Kwani ndoa ndio takaso Bora na linafanya kitendo kile cha kuingiliana kiwe tofauti na viumbe wengine.

Kama hatufungamani na ndoa na kuendelea kuingiliana nje ya mpango wa Mungu basi hakika hatuna tofauti yoyote na wanyama,ingawa kimwonekano sio kama wanyama Ila kitabia ni kama wanyama.

Pamoja na changamoto mbali mbali ambazo zipo katika ndoa,lakini bado ndoa itabakia kuwa taasisi imara ya kuendeleza kizazi cha mwanadamu katika njia halali kabisa ambayo inampendeza Mungu,kwahiyo vyovyote itakavyokuwa bado ndoa ina umuhimu mkubwa Sana.

Wakataa ndoa Kwa mtazamo wangu ni watu ambao hawana Imani na Mungu kabisa,kwasababu kama ndoa ndio mpango ambao amewatayarishia wanadamu waufuate na njia salama Kwa Maisha Yao hapa duniani na kesho siku ya hesabu je wewe ni nani usie na hofu ya Mungu wako mpaka ukatae kuwepo Kwa ndoa?

Mtu yoyote ambaye ana Imani juu ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi anajua na kuamini kabisa njia pekee ya kukwepa dhambi ya zinaa ni kuoa au kuolewa Tu. Sasa ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kukataa ndoa ujue huyo hamjui Mungu na hajui hatima yake itakuwaje baada ya kumaliza Mda wake hapa duniani.

Hawa ni WA kuwahurumia Sana na bahati mbaya zaidi kuna watu wengine ambao nao kichwa kichwa wanaingia katika mtego huo huo ima Kwa ushabiki Tu au kwakujua au kutokujua,naomba niwazindue Kwa kuwaambia akili za kuambiwa changanya na zako,mwisho wa siku kila mtu atavuna anacho panda,hapo hakutakuwa na Sisi bali utakuwa wewe Tu na Mola wako.

Hoja inaweza kuja mbona kuna watu wameoa na bado wanazini? Hayo ni makosa mengine ambayo bado mwanadamu anaendelea kumkosea Mola wake. Tunapo kusudia kuoa INA maana sasa tunaachana na zinaa na kuwa katika ibada ya ndoa takatifu,tunakuwa katika njia ambayo inampendeza Mola wetu.

Na ndoa ni ibada, kwasababu ibada ni Matendo mazuri au maneno mazuri ambayo yanampendeza Allah, na unapata thawabu Kwa Jambo lolote la ibada. Kwa mfano unaposex na mumeo au mkeo ujue unapata thawabu,kwasababu unafanya kitendo ambacho kinampendeza Mungu,Maswahaba walipo sikia hili Kwa Mtume (s.a.w) walistaajabu Sana,wakamuuliza Nabii "yaani tunastarehe wenyewe na wake zetu na bado tunapata thawabu"?

Nabii akawajibu " vipi kama mngezini je msingeandikiwa madhambi"? Wakajibu ndio tungeandikiwa madhambi basi akawaambia na anayemwingilia mkewe WA halali basi anapata thawabu. Naam mpaka hapo naona umepata picha ni Kwa kiasi gani ndoa ni Jambo la muhimu na la kiibada.

Kwa mfano Kwa Sisi Waislamu, ndoa ni nusu ya Dini,Kwa maana ambaye ameoa basi ana asilimia 50 ya Dini na 50 iliyobaki ni kufanya ibada nyingine mbali mbali,kwasababu kwenye ndoa kunapatikana familia ambayo inatakiwa iishi katika misingi ya Dini na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu,kifupi ndoa ni taasisi ambayo ina mambo mengi ndani yake ambayo mume na mke watakuja kuulizwa je walisimamia vipi malezi ya watoto wao na mambo kadhaa WA kadhaa.

Je tufanye nini ili taasisi ya ndoa iwe imara na hatimaye ifikie malengo yake.

Kwanza nianze na vigezo vinne ambavyo ndio sababu ya kuoa au kuolewa.

1) Tunaoa kutokana na uzuri WA mhusika - uzuri unao zungumziwa hapa ni uzur ambao wewe mhusika unakupendeza Kwa mwanamke wako au mwanaume wako,kwamba Oa mwanamke ambaye hata ukimtazama basi nafsi yako inafurahi/na mwanamke vile vile.

2) Tunaoa kutokana na Nasabu/Ukoo husika - nenda kaoe kwenye nasabu au ukoo ambao unafahamika Tabia zake na mwenendo wake,kwani kuna koo nyingine ni mtihani Sana,huko maugomvi na mabalaa ni sehemu ya Maisha Yao,na Tabia huwa inafuata mkondo.

3) Tunaoa kutokana na Mali - wakati mwingine tunaenda kuoa kutokana na Mali au kuolewa kutokana na Mali za mhusika,sasa hapa ndio Pana mitihani Sana,unajua kabisa Fulani humpendi lkn unafuata Mali zake au hela zake,ndio baadae hela au Mali zikikata balaa linaanza.

4) Na mwisho Tunaoa kutokana na Dini ya mhusika - hapa ndio penye Jambo la muhimu Sana,Yani cheza kote lakini hapa usikosee, hakika mwenye hofu na Imani ya Mungu mara nyingi ni mtu Bora Sana katika kuanzisha nae Maisha ya ndoa. Kwani huyu atakulindia Mali yako,atajihifadhi na machafu Kwa maana hata zini au kuchepuka hata ukiwa mbali nae,na hata malezi ya watoto wako yatakuwa katika mikono salama kabisa.

Watu wengi hapa ndio tunafeli na ndio maana ndoa zimekuwa mitihani kila kukicha,tunakutana huko vyuoni,makazini na mabarabarani bila hata kuangalia vigezo muhimu ambavyo vingeweza kutusaidia kuwa na ndoa imara huko mbeleni.

Mifano tunayo huko zamani wazazi walikuwa Makini Sana katika kuangalia wachumba sahihi Kwa watoto wao na hata ndoa zao zilidumu Sana kwakuwa zilifuata mifumo sahihi ya kutambua mtu sahihi na kufunga ndoa sahihi.

Nashauri kabla ya kueneza kampeni yako ya Kataa ndoa,sijui ndoa ni utapeli sijui ndoa ni batili ebu tafakari hayo niliyoandika hapo na fanya tathimini na uone tatizo liko wapi.

Ni hayo Tu!

baby zu
Mademoiselle
Sharia za dini ya kiislamu zingekua zinaongoza sirikal, kidgo ungekua umeongea point , huwezi kuta wanaume wa Afghanistan [emoji1023] wanakataa ndoa ,kwa sababu ya mfumo dume , tukubali tukatae utamaduni wa kigeni umefanya ata kusiwe na umuhimu wowote kwenye ndoa
 
Sharia za dini ya kiislamu zingekua zinaongoza sirikal, kidgo ungekua umeongea point , huwezi kuta wanaume wa Afghanistan [emoji1023] wanakataa ndoa ,kwa sababu ya mfumo dume , tukubali tukatae utamaduni wa kigeni umefanya ata kusiwe na umuhimu wowote kwenye ndoa
Ni kweli utamaduni WA kigeni umesababisha au kuchangia Kwa kiasi Kikubwa kuporomoka au kuziepuka ndoa.

Je swali la msingi, kuna haja gani ya kukumbatia tamaduni ambazo zinaenda kinyume na asili ya mwanadamu?
 
Ni kweli utamaduni WA kigeni umesababisha au kuchangia Kwa kiasi Kikubwa kuporomoka au kuziepuka ndoa.

Je swali la msingi, kuna haja gani ya kukumbatia tamaduni ambazo zinaenda kinyume na asili ya mwanadamu?
Ni kukataa ndoa mkuu mpka waone kuna umuhimu wa kurudi kwenye asili.
 
Ni kukataa ndoa mkuu mpka waone kuna umuhimu wa kurudi kwenye asili.
Kwa upande mmoja upo sahihi chief

Lakini

Je tutarudi vipi katika asili ikiwa kila kukicha Sisi ndio WA Kwanza kupinga kile ambacho kitaturidisha katika asili yetu?

Kama kweli tuna Nia ya kurudi katika asili yetu basi Kwanza tungetambua changamoto ambazo zinatukabili na kisha tutafute mwarobaini WA ishu nzima.

Au waonaje chief
 
Chief siwezi kutoa hela yangu (Mahari) kununua majanga (mwanamke) ili niishi nayo ndani mwangu.... wanawake ni mashetani chief dawa yao ni kutoishi nao bali ni ku-hit and run, one night stand bablai!!!

Tajiri halisi awe mwanamke au mwanaume huwa hataki kusikia upuuzi unaoitwa ndoa maana ndoa ni kuuza utu na uhuru wako kwa mtu mwingine.

Ni tajiri gani halisi atayekubali kuutweza utu wake na kuuza uhuru wake kwa mtu mwingine?

Wanawake wengi wanafuata mali tu kwenye ndoa maana asilimia kubwa ya wanawake wanaojiweza kiuchumi hawataki habari za ndoa bali wanataka kuzalishwa tu na waachwe free kulea watoto wao, unafikiri sababu ni nini?? Hawataki kuuza utu na uhuru wao kwa mpuuzi mwingine.

Chief nimesikia maoni yako

Nami sina neno zaidi ya kusema kila Mtu ana maoni yake na mtazamo wake

Shukrani
 
Shukrani Sana mtu wangu Kwa maoni yako ambayo naweza sema yapo Kati Kwa Kati na hii ndio maana halisi ya kuwa na mitazamo tofauti.

Nimependa zaidi juu ya kauli yako kwamba,kila kitu kijitetee chenyewe.

"Imeisha iyo..we mooove!!"
Ndoa inaleta Heshima Kwa WANAWAKE TU
 
Back
Top Bottom