Ndoa katika umri mdogo/utotoni

Ndoa katika umri mdogo/utotoni

JB blue

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Makala haya mafupi yanaletwa kwenu na mwaandishi wenu Orkipirie lenaiterru kopp.

Ndoa za utotoni au katika umri mdogo ni pale ambapo msichana au mvulana wanapoingia katika ndoa wakiwa katika umri mdogo sana chini ya miaka 18.kwani umri mdogo huanzia 0-17miaka watoto ambao wapo katika umri huo basi huwa tunawahesabu kama watoto.Hali hiyo inavyo jitokeza ya msichana au mvulana kuolewa /kuoa mtu aliye mzidi umri .

Jamii nyingi hasa za wafugaji zimekuwa zikijihusisha sana na dhana hii ya kuwaozesha watoto wakike wakiwa katika umri mdogo sana. Bila kujali kwamba mtoto wao ana haki za msingi ambazo anahitaji kuzipata kabla ya kujihusisha katika mambo ya kutunza familia. Haki zenyewe ni Elimu,malenzi bora kutoka pande zote mbili yaani wazazi wote wawili,malazi,chakula bora,sehemu nzuri pa kulala.

Kuna mambo kadha wa kadha yanayopelekea familia nyingi kuwaozesha watoto wao katika umri mdogo .Mambo yenyewe ni kama yafuatayo.

1. Mimba
Wasichana wanapo pata mimba familia nyingi zimekuwa zikiwaozesha wasichana wao au watoto wao wakike kwanza wakiwa na lengo la kuwakomesha au kuwapa adhabu kwamba kwanini kapata mimba au ujauzito,familia zingine ili kuepukana na aibu ya watoto wao kupata mimba wakiwa nyumbani wamejikuta wakiwaozesha ili kuepuka aibu

2. Umasikini
hii pia imechochea kama sio kupelekea wasichana wengi kuolewa kwani familia nyingi hujikuta wakiwawozesha watoto wao kwa lengo la kujipatia mali,hivyo basi mtoto wa kike anajikuta ni kama kitega uchumi katika familia.

3. Mila na desturi
hii pia imepelekea wasichana wengi wa kike kuolewa katika umri ulio mdogo kwani jamii nyingi za kiufugaji wasichana wengi wa kike wameolewa na wazee wa makamo,jamii nyingi Bado wanaendelea kuzifuata mila na desturi za mababu zao na wanaendelea kuona kwamba ni jambo la kawaida sana kwa msichana mdogo kuozeshwa au kuolewa katika umri mdogo.

Zifuatazo ni athari za ndoa za utotoni/umri mdogo;

1. Kutengwa

wasichana wengi wamejikuta wakitengwa na familia zao na kwenda kuanza maisha mapya katika familia zao ambazo sasa wenyewe ndio wanaenda kubeba majukumu mengine kama kulea familia,kufanya kazi za nyumbani .wengi wao pia wamejikuta wakitengwa kutoka kwa marafiki zao kwani muda ambao walitakiwa wawe shuleni na marafiki zao wao wapo majumbani wanalea familia,hivyo basi wamejikuta wakitengana na marafiki zao.

2. Virusi Vya Ukimwi (VVU)
wasichana wengi kwa kuwa sasa huolewa wakati wakiwa bado hawaja pata elimu bora au kidogo tu kuhusu virusi vinavyo sababisha UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa ,wasichana wengi wamejikuta wakiwa waathirika wakubwa wa ugonjwa huu hatari.

3. Ukatili
katika jamii nyingi wasichana wengi wanapo olewa wengi hupitia changamoto kadha wa kadha,kutokana na maumbile ya miili yao Bado ni madogo wengi wao hufanyiwa ukatili.

4. Huathiri afya ,elimu na usalama
Ndoa za utotoni kiujumla Huathiri afya,elimu ,furaha na usalama wa motto kwani muda ambao mtoto alitakiwa apate elimu tayari ndoto zake zisha zimwa kwa kuolewa,wakati alitakiwa spate muda wa kukaa na kupumzika huku wazazi wake wampiganie kwa kumtafutia chalula bora na usalama wa kutosha yeye huo muda hato kupata tena kwani na yeye sasa ni mama wa familia nyingine Mpya.

5. Mimba
kutokana na wasichana wengi huolewa katika umri mdogo wengi wao hujikuta wanabeba mimba katika kipindi ambacho miili yao hayaja pevuka na kuwa tayari kupokea na kubeba mimba ,kwa kuwa basi bado via vyao vya uzazi havija komaa wengi huongeza hatari ya maradhi na kifo

Njia zifuatazo zikifuatwa zinaweza kuzuia au kutokomeza kabisa ndoa za utotoni

1. Kuwathamini wasichana

wasichana sasa waanze kuthaminiwa kama watu wengine pia wapewe ajiamulie maamuzi yao pia yaani wasome ,kiufupi wapewe elimu ya kutosha ,kwenye masuala ya kuoa basi amchague yule yeye amtakae na sio kulazimishwa kuolewa asiko taka yeye.

2. Kupasa sauti
sisi kama jamii au taasisi ambazo zinajishighulisha na masuala ya kijamii hazina budi kupasa sauti na kukemea haya mambo katika jamii zinazo tuzunguka na kuwapatia elimu za kutosha na wakati mwingine sheria kali zitungwe kama makosa ya jinai kama mtu atamuozesha msichana katika umri mdogo.

3. Elimu/kuelimisha jamii
Jamii pamoja na serikali kwa ujumla sote tuna wajibu wa kuwatetea wasichana pamoja na wavulana wote wanao ingizwa katika ndoa za utotoni katika umri mdogo ambao wao walistahili wapate elimu,malezi mazuri kutoka katika familia zao ,asasi za kiraia na zisizo za kiaraia nazo waungane kwa pamoja kutoa elimu kwa jamii ili kuwakoa hawa vijana tena taifa la leo na sio la kesho kwani humo tuna marais,mawaziri,waandishi ,watangazaji na wengine kibao tu.

4.Kutoa taarifa
kwa walimu,wazazi,walezi,na viongozi katika jamii,endapo kutaonekana kuna msichana analazishwa kuolewa.

5.Kuwakumbusha
watu wanaolazimisha wasichana kuolewa, kuwa wanavunja sheria na sheria itachukua mkondo wake dhidi yao. Taasisi, asasi, watu wazima ambao wanataka kutokomeza ndoa za utotoni, washirikiane na vijana kuhakikisha kuwa sauti za wasichana na wavulana zinasikika pale maamuzi muhimu yanapofanyika kama vile kubadili sheria na Sera mbalimbali katika masuala ya kuwatetea wao.
 
Back
Top Bottom