Ndoa na Dini

Chance ndoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
4,363
Reaction score
10,265
Habari ndugu zangu,

Nakuja kwenu nikiwa na nia ya kuomba maelekezo ya maswala ya ndoa na dini kwa upande wa ndoa ya kiislamu na ukristo.

Naomba kufahamu! Hivi mtu akioa wake wawili ndoa ya kiislamu, akabadirisha dini na kuwa mkristu (Roman catholic) baada ya muda.

Akiwa bado na wake zake, na wake wapo tayati kufata dini ya mume wao.

Je, Dini inasimamaje hapa, anabatilisha hii ndoa au?
 
Sio mbaya maana watamtenga. Hivyo ataishi kwa tabu sana. Uislam watamuona msaliti,wakristo watamuona ndumila kuwili,wapagani hawatamuelewa
Hapo abadili dini halafu alindindishie kanisa abaki na wake zake hao hao wawili
 
Wapuuzi sana wamekaa chini na kujitungia kuoa mwisho mke mmoja tu
Iwe ni men made au Gods plan huu utaratibu umesaidia wengi.

Wapo watu vipato vya kuunga unga ili wale lazima watoke lakini wanamiliki wake wanne na kila mke watoto zaidi ya watatu na currently hao wake wana ujauzito sasa jiulize wote wangeruhusiwa hivyo hii nchi ingetutosha?

Wajinga wangekuwa wengi sana.
 
Iwe ni men made au Gods plan huu utaratibu umesaidia wengi...
Huo ni mtazamo wako wako nchi isingetosha ina maana watu hawafi?Kama ni hivyo nchi za kiarabu pasingetosha.

Wazee wa zamani mke mmoja anazalishwa watoto 15 na life linasonga,kwa sasa hivi hata uwe na wake 4 hauwezi kufikisha watoto 15.
 
Kama umehamia ukristo unabaki nao kama wamehiyari kukaa na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…