Ndoa na kanisa

Ndoa na kanisa

Mageuzi92

Member
Joined
Jan 14, 2023
Posts
6
Reaction score
3
Hello,

Ningependa kujua mamlaka ya kanisa kufungisha ndoa iliyatoa wapi? Ikiwa Bible inawapa majukumu wazazi wakikubali ndoa tayari.

Kuna makanisa yalikuwa yanasitisha baadhi ya huduma Kwa wazazi ambao watoto wao hawajafunga ndoa kanisani. Je, mamlaka hii inatoka wapi? Anyway mwenye andiko lenye mashiko kuwa ndoa lazima ifungiwe kanisani alilete.
 
Hakuna mahali popote kwenye Biblia walipopewa Mamlaka. Ni utaratibu tuu wa madhehebu.

Hivyo sio dhambi kutunga ndoa kijadi, Yaani unaenda upande wa kiukeni, unatoa posa, kisha unachukua Jiko lako.

Ndoa inahusu MKE na Mume tuu, kisha kama kuna nyongeza basi ni familia za Pande mbili full stop.
Mambo ya wachungaji ni janja na mbinu ya kuhakikisha Watoto watakaozaliwa wawe Wateja/waumini wa dhehebu Hilo. Na sio vinginevyo
 
Hakuna mahali popote kwenye Biblia walipopewa Mamlaka.
Ni utaratibu tuu wa madhehebu.

Hivyo sio dhambi kutunga ndoa kijadi,
Yaani unaenda upande wa kiukeni, unatoa posa, kisha unachukua Jiko lako.

Ndoa inahusu MKE na Mume tuu, kisha kama kuna nyongeza basi ni familia za Pande mbili full stop.
Mambo ya wachungaji ni janja na mbinu ya kuhakikisha Watoto watakaozaliwa wawe Wateja/waumini wa dhehebu Hilo. Na sio vinginevyo
Nyongeza, sheria ya nchi (Tanzania) inaeleza uwepo wa ndoa kwa imani ya ukristo au uislamu; kwa hiyo uwepo wa sheria pia umelazimisha ndoa zifungwe makanisani na misikitini. Biblia haina takwa hilo la ndoa kufungwa kwenye sinagogi
 
Ni kweli Kabisa.
Ila kama ningekuwa mshauri wa Vijana ningewaambia wafunge ndoa za kijadi. Kulingana na tamaduni zao.

Ndoa za kijadi Sifa yake kuu NI ngumu kukushinda Kwa sababu imebeba mfumo na asili ya kiafrika.
Wakati ndoa za Kikristo na uislam zipo mbali na asili na mifumo ya kiafrika.
 
Sisi tuliambiwa ndoa ni sakramenti, sakramenti ilianzishwa na Yesu, ili kuleta ukamilifu wa wokovu.

Na vilevile ndoa ni mali ya kanisa, na watakao tokana na ndoa ni mali ya kanisa, yaani watoto.
 
Ni kweli Kabisa.
Ila kama ningekuwa mshauri wa Vijana ningewaambia wafunge ndoa za kijadi. Kulingana na tamaduni zao.

Ndoa za kijadi Sifa yake kuu NI ngumu kukushinda Kwa sababu imebeba mfumo na asili ya kiafrika.
Wakati ndoa za Kikristo na uislam zipo mbali na asili na mifumo ya kiafrika.
Umenena vyema sana. Aliyeleta dini za kimagharibi na mashariki ya kati mwambieni ana adhabu yake inamsubiri
 
Ndoa ni Utaratibu

Na kila jamii, jumuiya au imani ina utaratibu wake
 
Ni kweli Kabisa.
Ila kama ningekuwa mshauri wa Vijana ningewaambia wafunge ndoa za kijadi. Kulingana na tamaduni zao.

Ndoa za kijadi Sifa yake kuu NI ngumu kukushinda Kwa sababu imebeba mfumo na asili ya kiafrika.
Wakati ndoa za Kikristo na uislam zipo mbali na asili na mifumo ya kiafrika.
Ili wafunge ndoa za kijadi na ziwe na maana ni lazima waishi kijadi kabla ya kufunga ndoa. Yaani watu walioishi kisasa hawawezi kufunga ndoa ya kijadi na ikawa na maana.
 
Back
Top Bottom