Black Rose
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 243
- 171
- Thread starter
-
- #41
Haya wewe tuoneshe hii mahakama isiyo ya kadhi imeleta maendeleo yepi? labda ya rushwa iliyokithiri mahakamani.
Kwanza, Mtazamo wako kuwa kuna jamii ya wanaume waislamu hawawatendee haki wanawake wao ni sahihi kabisa, lakini napenda nikufahamishe kuwa hayo ni makosa yao wanaume wa kiislam na si makosa ya uislamu na mahakama ya kadhi haiwezi kunyimwa kwasababu kuna wanaume wa kiislamu wanawatesa wanawake kinyume cha mafundisho ya dini.
Pili nafikiri mahakama ya kadhi iliyo na waadilifu itasaidia kutoa hukumu kama hizo ulizosema, sidhani kama ni sawa kidini kwa mwanaume asiye na uwezo kuoa wake zaidi ya moja mfano kuwalaza wake zake kwenye chumba kimoja kama ulivyosema. sharia inaufafanuzi wa kutosha kuhusu nani anaruhusiwa kuoa, sababu za kuoa nk. imetoa mfano mzuri ni kwanini mtume alioa hizo sababu za mwanamume muislamu kuoa na si vinginevyo..
Tatu, sisi tunaotaka mahakama ya kadhi si kwa ajili ya kunyanyasa wanawake bali kwa ajili ya kufanya ibada zetu, kuona kuwa mali zetu na maisha yetu yanakuwa katika hukumu ya Allah, mahakama itasaidia kutoa ufumbuzi wa mirathi za mali zetu ..above all ni choice kwako kama unaona bado uzito kufuata hukumu hiyo unaweza kutumia sheria za nchi..
Nafikiri swala hili ni la imani hakuna kulazimishana katika imani
SUALA LA RUSHWA TANZANIA NI KAMA CANCER ILIYOENEA KILA PAHALA.
MI SIDHANI KAMA RUSHWA NI SUALA LA DINI FULANI BALI NI LA WATU FULANI.
SASA HIVI JAJI MKUU WA Tanzania ni Mwislam, je imabadili mwelekeo wa rushwa?
Tusijitukanishe wenyewe kwa kupambanisha tabia na dini zetu. Tujenge hoja mahususi katika kudai haki zetu.
Jaji Muislaam anahukumu kwa Sharia au kwa hukumu zisizo za dini? Uozo aliokuta hapo unafikiri bila kuwa na sharia ataumaliza kwa mwaka wake mmoja au miwili aliokuwepo? maawe!
Kwani kabla ya Jaji Chande ( JM) unataka kusema hawakuwepo Majaji waislam? Je huko ZNZ ( kwenye Kadhi courts) unataka kusema mambo ni shwari hakuna rushwa wala uozo?
Unajua Faiza, nchi yote ina uozo wa namna moja ama nyingine.
Sharia itawezaje kumaliza matatizo? Nchi yenyewe ina imani za kila aina.Huwezi hata kuthubutu kuwazia kutumia Sharia hapa. Wananchi wenyewe wenye imani zao, hata hawazitii ndio itakuwa kutumia Sharia?Assuming kuwa Tanzania inatumia Sharia, nani atapona?Its such a mixed up society!
Hivi ikiwa unashindwa kujiondoa wewe mwenyewe kwenye umaskini unategemea nani akuondoe? Kanisa limeshakutoa kwenye umaskini?
Umaskini hauko kwenye mali au kipato chako umaskini upo ndani ya damu yako. Hata uletewe Papa hatokuondolea umaskini uliokuwa nao.
Uwepo wa kadhi ni kuhakikisha kuwa Muislaam ana haki kama yule asie na dini. Au mwenye haki nchi hii ni yule ambae hana dini?
Kodi za Waislaam na wasio Waislaam zinalipia Mahakama za wasio na dini. Jee hiyo ni haki? Ambae ana dini yake hana haki? Mnanshangaza.
Usichanganye Muislaam na Uislaam,
Jaji hata akiwepo Muislaam kwani anahukumu kwa sharia? Ya Kenya siyajuwi kwa hiyo sina uwezo wa kuyaongelea. Mahakama zetu zinanuka uozo wa rushwa, na hiyo haihusiani na uwepo wa majaji wa Kiislaam.
Mimi hii kitu ya watoto nje ya ndoa kutotambulika kwenye mirathi inanitia huzuni maana ndiyo inasababisha sana uduni wa maisha ya watu wengi. Lakini mwisho wa siku utasikia ni 'mfumo kristo' ndiyo unaleta ufukara ...kumbe ukweli ni kuwa ufukara unasababishwa na viidume vingi vilivyokosa maadili na kujaa zinaa.
Topical and Co wapo likizo ya Xmas nini?
Black Rose nimekupenda. Umeongea point ingawa wameshindwa kukujibu kwa point husika. Tunahitaji kama wewe muwe wengi kusaidia upotoshaji humu.
Twende point by point
A) Kuchanganya MUISLAM na UISLAM - Muislam ni yule anayamini uislam iwe kamili au nusunusu.Unafikiri hao majaji utakaowapata ambao ni waislam kwa standard zako watatoka wapi kwa nchi kama Tanzania?Na kama unataka Uislam tu bila waislam, basi Tanzania mbona siyo pahala pake!
B) Umezungumzia kutumia SHARIA -Unauliza kama Jaji muislam anahukumu kwa Sharia. Kwani tatizo wewe unadhani ni nini? kwa Tanzania bara, unafikiri hili linawezekana? Tanzania bahati mbaya ni nchi "isiyo na dini" ila watu wake wana dini zao ikiwepo Uislam.Taratibu zinazofuatwa ni za nchi na siyo za wenye dini zao.Sharia zetu ni zetu siyo za Watanzania wote.Kwa msingi huu, ni muflisi kulilia kwanini Sharia haitumiki, au kutarajia Sharia itumike.
C) Mambo ya Kenya - Nimetoa mfano wa Kenya kwa sababu:
1. Kenya na Tanzania zinachangia mengi - historia, kwa maana zote ni nchi za kiafrika, zilizoingiliwa na wageni ( wazungu na waarabu) walioleta hizi dini zinazotuchanganya na kutugonganisha vichwa hadi tunajadili haya tunayoyajadili.
2. Nchi hizi mbili zina sheria zinazofanana ( common law, religious ( Islamic and other)laws and customary laws
3. Wananchi wake hawajajiondosha kwenye mila na desturi zao kiasi ambacho hili linaleta conflict of laws. Mtu ni Muislam lakini utashangaa hajaacha mambo ya mila zake za kimakua, kinyamwezi, kingoni etc. Kama akitaka kufunga ndoa anachanganya mila na dini, maisha yake anaishi kwa mtindo unaomtambulisha zaidi na mila badala ya dini utasema huyu ni mdini au mkabila? Kumbuka mtu anaweza badili dini lakini hawezi kamwe kubadili kabila hata angetamani vipi.Kadhalika, huwezi kubadili race.Hizi ni facts.Kwa msingi huu utaona tatizo liko wapi kwenye ishu tunayojadili.
4. Waislam wa Tanzania wanapenda kurejea kinachofanyika Kenya hasa kwenye kuanzisha Kadhi courts
Yaani unaweza kuamini nusunusu bado ukawa muislam labda hii dini ya babu yako!
Usikurupuke wewe!
Umekurupushwa na mafuriko au ??
Umefuatilia mada au unakuja na "ignorance"?
Umesoma FF kasema nini kuhusu UISLAM NA MWISLAM? NA JINSI JAJI MWISLAM ASIVYOWEZA KUSIKILIZA KESI AKATOA HAKI KUFUATA NA MATARAJIO ya SHARIA?
Tena wewe unaweza ukawa mmoja wa hao wasikuwa na "aa" wala "bee" kuhusu nini maana ya kuwa Muislam!
Ndugu yangu, hii mada siyo yale malumbano ya kidini. Hapa ni facts na points na siyo hekaya.Huna point za nguvu kaa pembani uwaache wanaojua nini kinaendelea.
Kwanza, Mtazamo wako kuwa kuna jamii ya wanaume waislamu hawawatendee haki wanawake wao ni sahihi kabisa, lakini napenda nikufahamishe kuwa hayo ni makosa yao wanaume wa kiislam na si makosa ya uislamu na mahakama ya kadhi haiwezi kunyimwa kwasababu kuna wanaume wa kiislamu wanawatesa wanawake kinyume cha mafundisho ya dini.
Pili nafikiri mahakama ya kadhi iliyo na waadilifu itasaidia kutoa hukumu kama hizo ulizosema, sidhani kama ni sawa kidini kwa mwanaume asiye na uwezo kuoa wake zaidi ya moja mfano kuwalaza wake zake kwenye chumba kimoja kama ulivyosema. sharia inaufafanuzi wa kutosha kuhusu nani anaruhusiwa kuoa, sababu za kuoa nk. imetoa mfano mzuri ni kwanini mtume alioa hizo sababu za mwanamume muislamu kuoa na si vinginevyo..
Tatu, sisi tunaotaka mahakama ya kadhi si kwa ajili ya kunyanyasa wanawake bali kwa ajili ya kufanya ibada zetu, kuona kuwa mali zetu na maisha yetu yanakuwa katika hukumu ya Allah, mahakama itasaidia kutoa ufumbuzi wa mirathi za mali zetu ..above all ni choice kwako kama unaona bado uzito kufuata hukumu hiyo unaweza kutumia sheria za nchi..
Nafikiri swala hili ni la imani hakuna kulazimishana katika imani
Umeishaona muislam anasifiwa na wasio waislam? Ahahahaha! Endelea na porojo zako za Kipepe!
Faiza Foxy said:Watoto nje ya ndoa wakiwemo kwenye mirathi wataleta matatizo zaidi. Kumbuka Uislaam unasisitiza ndoa na hausisitizi zinaa na kama mtu aliteleza na kuzaa nje ya ndoa basi ampe mali (kama anayo) huyo mtoto nje ya ndoa na kabla hajafa na si kuleta rabsha baada ya kufa.
Umeishaona muislam anasifiwa na wasio waislam? Ahahahaha! Endelea na porojo zako za Kipepe!