Twende point by point
A) Kuchanganya MUISLAM na UISLAM - Muislam ni yule anayamini uislam iwe kamili au nusunusu.Unafikiri hao majaji utakaowapata ambao ni waislam kwa standard zako watatoka wapi kwa nchi kama Tanzania?Na kama unataka Uislam tu bila waislam, basi Tanzania mbona siyo pahala pake!
B) Umezungumzia kutumia SHARIA -Unauliza kama Jaji muislam anahukumu kwa Sharia. Kwani tatizo wewe unadhani ni nini? kwa Tanzania bara, unafikiri hili linawezekana? Tanzania bahati mbaya ni nchi "isiyo na dini" ila watu wake wana dini zao ikiwepo Uislam.Taratibu zinazofuatwa ni za nchi na siyo za wenye dini zao.Sharia zetu ni zetu siyo za Watanzania wote.Kwa msingi huu, ni muflisi kulilia kwanini Sharia haitumiki, au kutarajia Sharia itumike.
C) Mambo ya Kenya - Nimetoa mfano wa Kenya kwa sababu:
1. Kenya na Tanzania zinachangia mengi - historia, kwa maana zote ni nchi za kiafrika, zilizoingiliwa na wageni ( wazungu na waarabu) walioleta hizi dini zinazotuchanganya na kutugonganisha vichwa hadi tunajadili haya tunayoyajadili.
2. Nchi hizi mbili zina sheria zinazofanana ( common law, religious ( Islamic and other)laws and customary laws
3. Wananchi wake hawajajiondosha kwenye mila na desturi zao kiasi ambacho hili linaleta conflict of laws. Mtu ni Muislam lakini utashangaa hajaacha mambo ya mila zake za kimakua, kinyamwezi, kingoni etc. Kama akitaka kufunga ndoa anachanganya mila na dini, maisha yake anaishi kwa mtindo unaomtambulisha zaidi na mila badala ya dini utasema huyu ni mdini au mkabila? Kumbuka mtu anaweza badili dini lakini hawezi kamwe kubadili kabila hata angetamani vipi.Kadhalika, huwezi kubadili race.Hizi ni facts.Kwa msingi huu utaona tatizo liko wapi kwenye ishu tunayojadili.
4. Waislam wa Tanzania wanapenda kurejea kinachofanyika Kenya hasa kwenye kuanzisha Kadhi courts