Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Status
Not open for further replies.

Ukiacha dharau na kijeli tunaweza kufanya mjadala

Lakini bado una hasira na waislamu wamekufanya nini?? au mafundisho yako ndio yamekufanya uwe na hasira hivyo

Calm down sema shida yako tujadili..hunijui sikujui, hunilishi sikulishi ok..
 


Ndugu yangu,
Naomba radhi kwa wenzangu maana inakuwa kama vile nimehodhi mjadala maana maswali yanaelekezwa kwangu nijibu kama vile mimi ni "mtaalamu" la hasha!

Naomba niseme mimi siyo mtaalamu.Wapo wenyewe wanazuoni waliobobea. Ninachofanya hapa ni kushirikishana kile ninachojua.Vile vile nitaomba wenzangu nao washiriki kikamilifu katika kutoa uelewa.
Uislamu unatoa muongozo kuhusu kuwaoa watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo hawa walipewa torat na biblia kabla waislam hawajateremshiwa Kuraan). Ruhusa hiyo imetolewa kwa sharti ambalo linahitajika lipatikane "kusihi" hiyo ndoa. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

"Na ni halali kuwaoa wanawake wema walio waumini na wema miongoni mwa wale waliopewa "Kitabu" kabla yenu nyinyi ikiwa mtawapatia ujira wao (mahari) mkafunga nao ndoa, bila kufanya uzinzi wala kuwaweka wanawake wa kinyumba" (5: 5).

Hata ikiwa mwanamke wa Kikristo ni mwema anayejitunza vizuri kimaadili na tabia yake , hua inaonekana kuwa si katika maslahi kwa Waislamu kuwaoa kwani ikiwa kila Muislamu atakimbilia Mkristo, wasichana wa Kiislam wataolewa na nani? Itabidi wasichana hawa nao wachukuliwe na Wakristo hivyo kuleta "maafa " kwa jamii ya waislam kwa maana watoto watakaozaliwa mara nyingi wataingizwa katika Dini za mama zao. Au ikiwa kunatokea ugomvi unaopelekea wanandoa hao kuachana, sheria za nchi zinampatia haki ya ulezi mama. Na ikiwa mama ni Mkristo basi inatarajiwa kuwa na mtoto naye atakuwa wa Dini hiyo. Mtoto huyu anaweza akaja kupoteza haki zake nyingine.Hivyo Waislam wanatahadharishwa juu ya suala hilo.Ikitokea mwanaume mwislam anachukua mwanamke wa Kikristoanatakiwa amfanyie Da‘wah huyo mwanamke ili apate kusilimu na kisha afundishwe Dini ili ajikite katika imani.

In short, wanatakiwa wafunge ndoa kwa njia ya Kiislamu ili haki nyingine ziweze kupatikana katika mahakama ya kadhi.Angalizo" mwanaume wa Kikrito hawezi kuoa mwanamke wa Kiislam na ndoa ikatambulika Kiislam!

Wakristo hawawezi kurithi mali ya Muislam kama Kadhi courts zitaamua.Ila masuala haya ndio tunaona yakienda mahakama za serikali.Ndiyo maana waislam kama ndugu yangu Topical wenye kutaka ibada kamili wanataka sana KADHI Courts ili kila jambo lake lifuate Sharia kwa ukamilifu.

 
wewe uko upande gani? Je ni halali au siyo halali kumuoa au kuolewa na Mkristu?

Mimi upande niliopo ni Halali kumuoa mwanamke mkiristo, lakini si halali kuolewa na mwanamke muislam na mkristo ntaeleza sababu kabla hujaja na majibu yako:

Kwanza madhumuni ya kuumbwa watu duniani ni ili kumuabudu MUngu moja TUU! (kufanya ibada on all aspects of life) hivyo marriage ni ibada; hivyo kwakuwa

a. Uislamu unaamini kwamba leader of the house (Jamii/familia) ni mwanaume leadership is not dictoatrship??? maana wengi wamebadilisha uongozi kuwa udikteta hivyo kuwaumiza dada zetu. Leader huyu ataongoza watu wake katika kumuabudu Mungu moja TUU!

b. Kwakuwa Mwanaume ni leader, hivyo nyumba hii inatagemewa kuongozwa kiislamu na watu wakaishi katika kumuabudu Mungu moja hapa duniani hivyo ni sawa mwanaume wa kiislamu kuoa mwanamke wa kikristo and not the other way round..

Huo ni msimamo wangu lakini haina maana kwamba msimamo mwingine (thoughts) ni zambi no; hiyo demokrasia halali ya dini yetu.
 
Ukiacha dharau na kijeli tunaweza kufanya mjadala

Lakini bado una hasira na waislamu wamekufanya nini?? au mafundisho yako ndio yamekufanya uwe na hasira hivyo

Calm down sema shida yako tujadili..hunijui sikujui, hunilishi sikulishi ok..

Unaweza kunionesha sentensi moja yenye dharau katika hayo niliyoandika?
 
Unaweza kunionesha sentensi moja yenye dharau katika hayo niliyoandika?


Unaposema aliyekutuma una maisha nini?, pili unaposema uislamu unaonea wanawake kwanini uwasemee wanawake wa kiislamu hiyo ni dharau kwasababu hakuna aliyelazimishwa kuwa muislam Tanzania?? unafikiri watu wote 1.5 bilions muslims arround the world ni wajinga kufuata uislam?? think before posting things of that nature..

Back to the Topic; wewe kama mkristo unakosa nini kwa sisi waislamu kupewa mahakama ya kadhi? please usiniambie habari ya costs etc maana hiyo ya gharama linazungumzika na mifano ya MoU unatosha ..
 

Am so sorry my pathetic friend, sina maneno ya kukufurahisha zaidi ya kukwambia ukweli. Naposema umetumwa namaanisha kwa maana siamini kama unaweza kuongea mambo haya yasiyo na maslahi hata kwa jamii yako bila kulipwa.

Just think about this: unawezaje kulinganisha HOSPITALI ambayo ni huduma kwa jamii (bila kujali dini wala rangi) na Mahakama ya kuamua ndoa za dini yako?

Nini kinakufanya uamini kuwa MoU ni kwa faida ya KANISA na sio kwa faida ya JAMII? Na ukitaka kujua jinsi mlivyo wategemezi na mizigo angalia hii sentensi yako (wewe kama mkristo unakosa nini kwa sisi waislamu kupewa mahakama ya kadhi?) Unaamini sana ktk kupewa na huna hulka ya kujitengenezea. Hii ndio sababu huoni umuhimu wa MoU kwa JAMII kwani sasa umesahau kuwa TUMEJENGA HOSPITALI KWA FEDHA ZETU na SERIKALI INAGHARAMIA NA KUSIMAMIA UENDESHAJI kwa manufaa ya jamii nzima.


Anyway, acha mimi niishie hapa. But that is what I think of you. Elimu ni tatizo na si dogo ni kubwa kweli kweli. Kama mtu mzima wa umri wa kujua kuoa na kutoa talaka huwezi kutofautisha Hospitali na Mahakama, what can I do?
 

Ndio maana nikakwambia wewe huwezi kujadili hadi utoe dharau oh pathetic friend oh elimu ndogo why all these kama unajiamini umesoma wewe??

Ok, I am done with you endelea kufikiri upendavyo..kuhusu mimi, kwa ufupi wewe huwezi mjadala wala huwezi kuhalalisha uwizi wa fedha za umma in the name of church projects???..

endeleeni kuwadanganya siyo sisi ambao tumefanya kazi muheza hospitala, tunajua mna charge shilingi ngapi wananchi per head, tunajua mnapewa kiasi gani kutoka serikalini

Unajisifia uwizi, anyway kwako wewe mafanikio ni fedha hata kama ni haramu kila la heri..tuko tofauti sana kimawazo I am sorry..
 
Ndio maana nikakwambia wewe huwezi kujadili hadi utoe dharau oh pathetic friend oh elimu ndogo why all these kama unajiamini umesoma wewe??

Nadhani na wewe ujifunze kuangalia unavyojadiliana na watu si lazima uwaite majina ili kufanya hoja yako iwe na nguvu. Kujadiliana kwa heshima ndiko kunakotakiwa.
 

Hivi, ukiandika usia wako na ukagawa mali yako mapema kwa mujibu wa dini na kuhakikisha umempata executor (anaweza kuwa yeyote umtakaye) inakatazwa?
 
Nadhani na wewe ujifunze kuangalia unavyojadiliana na watu si lazima uwaite majina ili kufanya hoja yako iwe na nguvu. Kujadiliana kwa heshima ndiko kunakotakiwa.

Hakuna mahali nimuita majina ila yeye ndio anaandika kejeli na dharau kwa uislamu na hilo halitaachwa kupita hivi hivi..

Kama hupendi sheria za kiislam siyo lazima ndio maana kuna wakristo, na wasio na dini..yanini kudharau hukumu zetu na kudharau watu 1.5 bilions duniani wanaofuata uislam halafu yeye (mkristo kutoka Tanzania) awadharau wote?? does it make sense??

kwa heshima nimemwambia aache kudharau tujadiliane aseme tatizo lake ni nini?? he keep on repeating same thing..
 
Hivi, ukiandika usia wako na ukagawa mali yako mapema kwa mujibu wa dini na kuhakikisha umempata executor (anaweza kuwa yeyote umtakaye) inakatazwa?

Wosia unaandkiwa hivi "Naomba nikifa mgawanye mali zangu kwa mujibu wa dini ya kiislam"


Anayeweza kufanya hivyo ni kadhi aliye na mamlaka, otherwise wewe mwenyewe uwe mtaalamu kweli wa dini na sharia za mirathi ambazo watu husomea miaka mingi ( na wote sisi japo tunataka hatuna utaalum huo)

Pili kuna swala la mgongono la tafsiri katika wosia maana wosia kwa mujibu wa uislam lazima uendane na sharia; kama mtoa wosia akikosea sharia inahurusu kutoa hukumu sahihi ili asipate dhambi siku ya kiama
 

asante sana kwani umejibu kitu ambacho najaribu kuonesha umuhimu wa kufikiria Kadhi katika Tanzania atafanyaje kazi. Kwa maneno mengine, mwanamke Mkristu aliyeolewa na Muislamu (ambaye hakukubaliwa kufanyiwa da'wah na kusilimu) hana haki katika mahakama ya kadhi na watoto wake wanaweza wasiwe na haki ya kurithi (kama wamechukua dini ya mama). Na mgogoro utakuwa mkubwa zaidi kwenye familia ambazo watoto wamechangia dini (wapo walio Waislamu na wapo walio Wakristu) kwani mahakama ya kadhi inaweza kuwapendelea watoto ambao ni Waislamu dhidi ya waoto wa Kikirstu kuhusu mali za baba yao yule yule.

Nije kwenye hili jambo jingine:

Angalizo" mwanaume wa Kikrito hawezi kuoa mwanamke wa Kiislam na ndoa ikatambulika Kiislam!

Hili ni jambo muhimu sana na kama unavyosema ningependa sana kusikia maoni ya wanazuoni wetu Tanzania. Wapo (bila shaka hata wewe unaweza kuwajua baadhi) wanawake wa Kiislamu ambao wameolewa na Wakristu kwa mujibu wa sheria zetu. Je, mwanamke Muislamu akiolewa na Mkristu anapoteza Uislamu wake? Labda swali lililofichika ni kwanini Mwanamme wa Kiislamu akioa Mkristu bado anakuwa ni Mwislamu na anawajibu wa kumsaidia mke wake kuishika imani lakini Mwanamke wa Kiislamu hana hilo? Vipi kama Mkristu anataka kuwa Muislamu?
 



Kwani ni kiasi gani cha kuendesha mahakama ya Kadhi?

Mbona kanisa linachota Billioni 60 (sasa hivi yanapata Billioni 91) .

Toka 1992- 2011 ni miaka 19= 60,000,000,000 x 18 + 91,000,000,000= Trilioni 1.17 or Trilioni 1.2. Kutoka katika kodi za WATANZANIA. Ambao waislam wapo humo?


Acheni roho mbaya kila kitu chenu tu.


 
Hivi, ukiandika usia wako na ukagawa mali yako mapema kwa mujibu wa dini na kuhakikisha umempata executor (anaweza kuwa yeyote umtakaye) inakatazwa?


Mwanakijiji.

Naomba ufahamu kuwa kuna sharia ya mirathi iliyowekwa na Mola ambayo ni lazima ifuatwe. Huwezi kuwa na mirathi pasi na mtu kufariki (kwa maana nyingine ni lazima mtu afariki ndio mali yake ifanyiwe mirathi). Huwezi kugawa mirathi wakti mwenyewe ukiwa hai. Labda utoe au uandike uusia.

Lakini hata usia huo una mipaka yake kwa mujibu wa Dini yetu ya Kiislam. Huruhusiwi kutoa usia wa mali yako zaidi ya thuluthi moja. Na unaempa katika usia mali ile ni sharti asiwe miongoni mwa warithi wako. Kwani mtu anapofariki mali yote ina rudi kwa Mola na yeye ndie mwenye kutoa mwongozo wa mali ile nani amiliki na ndio akatoa sharia ya mirathi.
 

wewe si ni raia wa Oman!?
 
wewe si ni raia wa Oman!?



Ukweli unauma eeh. Hata nikiwa raia wa wapi lakin ukweli unasimama pale pale.
Mbona kanisa linachota Billioni 60 (sasa hivi yanapata Billioni 91) .

Toka 1992- 2011 ni miaka 19= 60,000,000,000 x 18 + 91,000,000,000= Trilioni 1.17 or Trilioni 1.2. Kutoka katika kodi za WATANZANIA. Ambao waislam wapo humo?


Acheni roho mbaya kila kitu chenu tu.


 

mwambieni rais Kikwete awapatie na nyie mchote sio kulalamika lamika na kutoa povu tu...
 

Hiyo ndoa haitambuliki Kiislaam na hao wanazini tu. Hakuna cha ziada.

Hilo nililokuwekea "blue" ni swali invalid, kwani hakuna ndoa hapo kuna zinaa tu, tena hilo ni kukiuka Sharia na afanyae hivyo anakuwa kaukana Uislaam. Kwa hiyo swali lako ni invalid. Hakuna Mwanamke Wakiislaam anaeolewa na Mkristo au mtu wa dini nyingine yoyote ile akabaki kuwa Muislaam, huyo ni Murtaad na ikiwa anajidai bado Muislaam wakati yuko kwenye ndoa isiyo halali Kiislaam huyo anajidanganya. Invalid Question.
 
Hii thread siyo ya ligi za kidini.
Ni kuelimishana zaidi
Ukitaka ligi rudi kule walikozoea.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…