salim710
New Member
- Sep 12, 2021
- 1
- 5
NDOA NI CHANZO CHA UMASKINI AFRICA
Wa hali gani wapenzi wasomaji wa jukwaa hili la Hadithi za mabadiliko. Bila shaka ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya. Karibuni katika makala hii ambayo inaangazia ni kwa kiasi gani ndoa huchangia umaskini Afrika. Najua wengi mmeshaangaa lakini baada ya kumaliza kusoma kila mmoja atapata picha halisi.
NDOA NI NINI; Kwa mujibu wa sheria ya ndoa tafsiri ya ndoa namba 5 ya mwaka 1971 ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke,unaokusudia kudumu kwa muda wote wa maisha. Ndugu zangu ni wazi ya kwamba kila mtu anatakiwa kuwa mwenza ili aweze kujitosheleza kijinsia hasa kujiepusha na zinaa, kuendeleza kizazi kwa wanadamu, kutengeneza mapenzi,huruma na ushirikiano,kujijenga katika uchumi na mwisho kukuza mahusiano na undugu katika jamii.
Ingawa kuwepo kwa malengo mazuri katika ndoa sio wanandoa wote hutimiza ndoto hizo katika nchi za Afrika. Utafiti wa kufuatilia kaya Tanzania (National Panel Survey) wa mwaka 2014/2015 uliofanywa na ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) unaonyesha kiwango cha talaka kimeongezeka kutoka kutoka asilimia 1.1 mwaka 2008/2009 hadi asilimia 2.1 mwaka 2014/2015. Kwa mwaka 2012 watu 715,447 walikuwa wametalakiwa sawa na asilimia 2.9 ya umri wa kuoa na kuolewa.
Lakini wataalamu wa masuala ya ndoa wanasema idadi ya ndoa zilizovunjika ni kubwa kuliko takwimu zilizopo. Mshauri wa masuala ya ndoa nchini Tanzania, Chriss Mauki alisema akihojiwa na BBC takwimu ambazo zinapatikana za talaka kwa Tanzania huenda si sahihi kwani watu wengi wametalikiwa bila hata kupewa hati za ndoa na hali hiyoni sawa na mataifa mengine ya duniani. Amesema katika nchi za afrika mashariki idadi ya ndoa zilizovunjika ni kubwa kuliko zinavyoorodheshwa katika takwimu za nchi kwani watu wengi hutalikiana bila kupeana makaratasi, na hivyo kutosajiliwa rasmi kwenye takwimu rasmi.
Nafikiri ndugu zangu tunaona ni kwa jinsi gani mdudu talaka huathiri ndoa zetu. Na napenda tufahamu ya kwamba nchi yeyote huanza kujengwa katika familia,tunapoharibu familia tunatengeneza jamii isiyo sahihi katika nchi yetu. Lakini Je, jamii na serikali kwa ujumla linatazama hili tatizo kwa jicho la tatu. Ngoja tuone madhara ya talaka yalivyo makubwa katika jamii yetu.
Madhara kwa watoto
Katika tafiti iliyofanyika katika chuo cha London imegundulika ya kwamba watoto ambao wazazi wao wametalikiana pindi wapo umri wa miaka 7 hadi 14 wanapendelea kupata matatizo ya kitabia na kimawazo. Pia husababisha kushuka kimasomo kwa watoto, kushindwa kushiriki katika shughuli za kijamii na pia watoto wengi wanaokumbwa na kitendo cha kuwa na hasira pia watoto wengi wanaonekana kuacha shule ivyo kupelekea ongezeko la watoto wa mitaani.kama watoto ndio kizazi kijacho chenye kupokea mwendelezo wa jamii kama watakosa vitu vya msingi je urithi wa jamiii etu utashikwa na nani?
Uchumi
Talaka inaathiri sana uchumi kutoka tovuti ya “verywell” katika tafiti iliyofanywa mwaka 2014 inasema walezi wa watoto wanaopoteza 25% hadi 50% ya kipato walichokua wanakipata kabla ya kutalakiana. Kwa nchi ya Tanzania tunaona wake na waume hueza kugawana mali walizochuma kipindi cha ndoa lakini tujue ya kwamba watu wengi hasa wake ambao hupata mali kutoka kwa wanaume zao wengi huzipoteza hizo mali na kushindwa kuziendeleza na wanaume hushuka kiuchumi.uchumi umekua tatizo mama kwa vijana na matamanio makubwa kulikabili ili tatizo.tumekua wafuasi wakubwa kuamini mbinu za kufanya kazi kwa juhudi ndio jawabu la mafanikio la hasha ndugu zangu kama atutajenga misingi imara ya familia tutakua ni watu wa hasara.
Matatizo ya kiafya
Asilimia 20% ya watu wanaotoka katika talaka hukumbwa na matatizo ya moyo, saratani na matatizo ya akili. Ivyo bhasi tutambue ya kwamba kuna baadhi ya watu upoteza maisha kwa kua na matatizo yalosababishwa na talaka ni wazi ya kwamba afya ni sehemu nyeti ya maisha ya mwanadamu kuingiliwa na talaka ni wazi inatubidi wote tujaribu pigana na ili jinamizi ambalo linaonekana kuishambulia jamii etu na wengi tukifumba macho
Jamii
Inatubidi tutambue ya kwamba jamii ya kitanzania huathirika sana na tumeona kwa ivi sasa ongezeko kubwa la watoto mitaani wakijishughulisha na shughuli zisizo rasmi ili kujikidhi maitaji asa kula ivyo bhasi ongezeko ili inakua rahisi ata awa watoto kujiusisha na shughuli kama wizi kwa watoto wasichana ongezeko la mimba za utotoni,matumizi ya madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia kama ubakaji
Uchukua miaka mitano kwa watu waloathirika na talaka kurudi katika hali yao ya kawaida kiuchumi na kisaikolojia tunagundua ya kwamba watu wengi upunguza kasi ya ujengaji wa nchi na jamii kwa muda mrefu ivyo bhasi inabidi tutambue ni kwa jinsi gani tunaeza punguza matokeo ya talaka katika ndoa zetu ili tujenge kasi ya uchumi katika jamii zetu
Wazazi
Wazazi tukumbuke ya kwamba ndoa ni kitu cha hiari kabla ya ndoa mlifanya makubaliano na kila mmoja akakubali kuishi na mwenzie .Ivyo basi kabla ya ndoa kila mmoja inabidi ajiridhishe ya kwamba mwenza wake ni sahihi kwake .Na maisha ni kitu ambacho kwa bahati mbaya sana ayana nafasi ya kufuta jambo na kuandika jingine ivyo inabidi kila mmoja atafute elimu ya kutosha kabla ya ndoa na ajiridhishe ni muda sahihi kwake ni lazima kila mmoja amchunguze mwenzie na maamuzi yatoke ndani ake bila kushawishiwa na mtu
- Serikali Inabidi tutambue ya kwamba familia ni msingi wa nchi malezi na maandalizi ya vijana kwa jamii uanza katika familia nchi kama watu watakosa malezi mazuri ni wazi tunatengeneza nchi iendayo pabaya.tafiti za ndani ziwe zenye kuangalia mazingira halisi ya nchi zetu .Pia serikali inajukumu la lazima kuelimisha jamii elimu ya ndoa na kutunga sheria ambazo zitasaidia kutovunjika hovyo kwa ndoa
- Dini Dini huhusika hasa katika ndoa viongozi wa dini watoe elimu ya kutosha kwa wanandoa kama vitabu takatifu vilivyotuonesha ni kwa jinsi gani mwenyezi mungu anafurahia jambo la ndoa na kuchukizwa na talaka ivyo kila mmoja anaeingia katika ndoa afahamu ya kwamba yampasa amshirikishe mwenyezi mungu katika kutatua changamoto na daima akitegemewa akuna linaloshindikana.
Mwisho nashukuru kwa kua pamoja katika kuisoma makala ii binafsi sina cha kuwalipa ila nawaombea kwa allah kutujaria afya njema sisi na vizazi vyetu pamoja na kutuongezea ridhiki……
Upvote
10