Ndoa si msiba, kwanini ziwatese watu wengine?

Ndoa si msiba, kwanini ziwatese watu wengine?

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 34:
Tukizungumzia msiba ni tukio la ghafla - msiba hutokea ghafla. Kwa watu ambao wana maisha ya kawaida matukio ya misiba yanawakuta wafiwa kwenye hali mbaya ya kiuchumi. Hivyo ni muhimu kumchangia hela mfiwa za kumsaidia.

Kuhusu ndoa/harusi:
Siku hizi matukio ya harusi yamekuwa ni madeni kama madeni mengine yanayohitaji marejesho. Ndoa/harusi si tukio la ghafla ni tukio la kupangwa. Muowaji, muolewaji na waozeshaji ndio wanapanga hilo tukio kwa matakwa yao. Kwa mtazamo wangu ndoa/harusi ni tukio la hiari.

MASWALI MATANO:
1. Je, unapangaje tukio la hiari bila kuwa na hela?

2. Je, unapangaje tukio la hiari kwa kutegemea pesa za ndugu, jamaa, marafiki na majirani?

3. Je, ni lazima kufanya tukio la hiari ambalo litahitaji pesa nyingi kuliko uwezo wako?

4. Je, mtu ambaye anahitaji kufunga ndoa ya gharama kuliko uwezo wake, ana utofauti gani na mtu ambaye atahitaji msaada wa kuchangiwa pesa ya kwenda kutalii (kula bata) nje ya nchi?

5. Je, kanisani na msikitini hawafungishi ndoa ambayo haitokuwa na sherehe yoyote?

Kama unaamua kuoa, kuolewa au kuozesha mtoto wako kwanini usiwekeze hela zako kisha uoe/uolewe bila kuwasumbua watu wengine wakuchangie hela. Nadhani hii pia itasaidia vijana kutokuvunja ndoa zao kiholela (bila sababu za msingi) hasa wakikumbuka machungu pesa zao.

Watu wanahangaika kuchanga pesa, wengine wanakopa hela wananunua magodoro, mabeseni, vitanda, makosheni, TV, makabati na makolokocho kibao wanakwenda kuwatunza wanandoa ukumbini, baada ya miezi mitatu mbele wanaambiwa ndoa imevunjika kwasababu mke alichelewa kurudi nyumbani.

Wapo watanzania ambao kwa mwezi anaweza kuwa hata na kadi 4 za michango ya harusi na kila kadi anatakiwa kuchangia si chini ya Tsh 100,000, bado kushonesha sare. Mtu huyu ukikutana nae barabarani amevurugwa unaweza kudhani ana madeni ya benki au Vicoba.​

Right Marker
Dar es salaam.
 
Msimamo wangu ni uleule, nachangia msiba magonjwa na matatizo mengine ya kijamii tu. Harusi, kipaimara, kumunio, birthday na takataka nyingine nisione kadi ya mchango nyimbani kwangu.
 
Msimamo wangu ni uleule, nachangia msiba magonjwa na matatizo mengine ya kijamii tu. Harusi, kipaimara, kumunio, birthday na takataka nyingine nisione kadi ya mchango nyimbani kwangu.
Uhakika, raha na starehe zako na familia yako zisababishe watu wainhie gharama za kukuwezesha kwenda kula nyabe kiurahisi.
 
Japo sio lazima kutoa hata ukipewa kadi unaweza usitoe ila haka ka msemo "KUTOA NI MOYO WALA SI UTAJIRI" Kamekaa kinafiki sana.

Ukweli Kuna kadi zingine unaona kabisa usipotoa Kwa namna Moja ama nyingine utaonekana wewe ni umejitenga na wenzio.

Mfano huu mwaka kazini kwangu tumekuwa na Ndoa Saba hizi Tyr zimepita Bado 2 nazo zote zipo mwezi huu. Na anawekwa kwenye kamati basi na kianzio wale wapambe wanasema 120k daaah
 
Me sitoagi michango ya harusi kwasababu najua sitafunga harusi yaan card napokea lakini ela yangu utaisikilizia redioni
 
Back
Top Bottom