Ndoa ya Bomani na ndoa ya kidini

Ndoa ya Bomani na ndoa ya kidini

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Wakuu wabobezi habari za asubuhi.

Napenda kuuliza, ikiwa nimefunga ndoa ya kiserikali na ikafikia wakati tukawa tumetengana na mwenzangu kwa maana ya kuachana japo tuna watoto, naruhusiwa kufunga ndoa ya kidini na mwanamke mwingine bila ya kutengua ndoa ya awali ya kiserikali?
 
Wakuu wabobezi habari za asubuhi. Napenda kuuliza, ikiwa nimefunga ndoa ya kiserikali na ikafikia wakati tukawa tumetengana na mwenzangu kwa maana ya kuachana japo tuna watoto, naruhusiwa kufunga ndoa ya kidini na mwanamke mwingine bila ya kutengua ndoa ya awali ya kiserikali?
Cheti cha ndoa anatoa nani? Kama ukikuwa haujui cheti cha ndoa ni kile kile,ufunge kanisani, msikitini,bomani mtoaji ni mmoja ila wahudumu tofauti.

Hapo labda ukafunge ya kimila tu ambayo haitambuliki serikalini.
 
Nawaelewa wakuu. Nimesikia asubuhi leo kwenye redio, hakimu akihojiwa na kusema kuwa aliyefunga ndoa ya serikali na mbeleni huko akaamua kufunga ya kidini na mwanamke mwingine utaratibu wa mgawanyo wa mali na matunzo utazingatiwa. Sikusikia akizungumza kuhusu kuvunja yakwanza ambayo ni ya bomani
 
Sawa zote ni za serikali Ila ndoa za kanisani hazina mkataba, serikalini ninaweza kuchagua ya mkataba. Palipoandikwa alichounganisha Mungu asitenganishe binadamu panakaririwa sana na waumini.
 
Ndoa ya pili ni batili

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ya Kimila/ Bomani ikoje? Na Ina tofauti zipi na hizi ndoa nyingine?? Naomba shule tafadhali.
 
Sawa zote ni za serikali Ila ndoa za kanisani hazina mkataba, serikalini ninaweza kuchagua ya mkataba. Palipoandikwa alichounganisha Mungu asitenganishe binadamu panakaririwa sana na waumini.
Una chet cha ndoa? Ili twende sawa
 
Wakuu wabobezi habari za asubuhi.

Napenda kuuliza, ikiwa nimefunga ndoa ya kiserikali na ikafikia wakati tukawa tumetengana na mwenzangu kwa maana ya kuachana japo tuna watoto, naruhusiwa kufunga ndoa ya kidini na mwanamke mwingine bila ya kutengua ndoa ya awali ya kiserikali?
Yote kwa yote, kufunga ndoa nyingine hakubatilishi ama kuvunja ndoa ya awali, kinachovunja ndoa ni talaka tu inayotolewa na mahakama.
 
Ndoa ya Kimila/ Bomani ikoje? Na Ina tofauti zipi na hizi ndoa nyingine?? Naomba shule tafadhali.
Ndoa ya kimila inafungwa kufuata mila na desturi husika ina hadhi kama ndoa ya kiserikali yaani ya bomani.
 
Yenyewe Haina Cheti cha Ndoa?? Niliona hapo juu Kuna mtu ali-comment hivi.
 
Back
Top Bottom