Ndoa ya Jacqueline Wolper yavunjika

Ndoa ya Jacqueline Wolper yavunjika

Unajua wanawake kila wakati wanaamini sie ndiyo huleta magonjwa majumbani. Lakini Mungu huwa anawaumbua. Ninaye ila tunaishi kama mtu na dada yake

duh kwa hiyo unalala na dada yako? hiyo ni dhambi kubwa …
 
Mimi nilivyoona tu viatu alivyovaa bwana harusi siku ya harusi nilijua safari hii haiendi mbali atawahi kuchoka maana sio kwa viatu vile
 
View attachment 3193375Ile NDOA iliyosimamisha internet. Imevunjika rasmi.

NB: Je atarudia FANTASY ya Zamani kama Shishi?

Source: Wolper mwenyewe
BCC: kataa ndoa

View attachment 3193318
Celebrities wote wa bongo walikuja hapa duniani kwa ajili ya matumizi ya starehe tu na kupokezana, siyo wa kuweka ndani. Mwanaume yeyote anayemweka celebrity ndani ni mwehu, hana akili kabisa.
 
Mimi nilivyoona tu viatu alivyovaa bwana harusi siku ya harusi nilijua safari hii haiendi mbali atawahi kuchoka maana sio kwa viatu vile
Viatu vilikuwaje na vina uhusiano gani na ndoa kuvunjika
 
Kwa nini unapenda kuvisoma hivi vitu ndugu yangu? Huwa nikiangalia nilipotoka, kwa kweli namshukuru sana Mungu wangu kwa jinsi alivyonipigania... siku moja nilikuwa nauza maembe huke kwenye mabasi ya mkoani, siku tatu mfufulizo hayanunuliwi... nikakaa nikafikilia sana, usingizi ukakosa mida ya saa 8 usiku nawaza tu kwamba leo mtaji umedoda. Nikaamuka , nikapiga magoti na kuongea kama mlevi hivi, " hivi wewe Mungu nimekusosea nini? umenitoa kijijini kwa kalindinga la jeshi, niko hapa najipambania, lakini bado mambo hayaendi, sasa nifanyeje"... hiyo ndio ikawa sala yangu... baada ya maneno hayo, nikapitiwa na usingizi kwa lisaa limoja, nikaamuka , nikaanza tena safari ya saa tisa asubuhi kwenda kuwahi daladala za super Najmunisa huko kariakoo. Njiani toka Yombo Dovya hadi Vingunguti muda huo bado nafikiria tu hiyo kauli " Hivi wewe Mungu nimekusosea nini?, njia nzima ... hadi kufika darasani ni wazo hilo tu na ikafikia hatua ya kuanza mchakato wa kunywa dawa niondoke hapa duniani... Mchana baada saa 9 mchana (mida ya shule kuisha, sijala chochote kile) siku hiyo nikayarudia maembe yale, nikielekea pale pale stendi nikajisemea, leo hata moja lisipo nunuliwa, mimi basi tena, naondoka zangi hapa duniani...

Nikiwa njiani kuelekea kituo cha mabasi ya Mikoani, mtu mmoja akasimamisha gari lake- suzuki Vitara, muda huo hizi garo zilikuwa maalufu san kwa wakuu wa wilaya, akayanunua yote na kunipa elfu8 zaidi kwa huruma yake tu kuniona nimebeba maembe yale nikiwa nina uniform kaptula ya kaki.... nililia sana kwa kweli. Yule mtu hadi sasa bado namtafuta, kama yumo humu aje tuonane- Mungu alimtuma kuyanunua, nikapata pesa ya tuition, viatu na mahitaji yote, shule ikaendelea, nikapasua zaidi. Ni episode nyingi sana za maisha niliyopitia. Ni kama movie hivi. Anyway, niishe hapa, maana the past ni chumvi kwenye kidonda bado.
Dah!! Unetoka mbali mzee...itabidi uandike kitabu mzeee
 
Unajua wanawake kila wakati wanaamini sie ndiyo huleta magonjwa majumbani. Lakini Mungu huwa anawaumbua. Ninaye ila tunaishi kama mtu na dada yake
Dah...!! atakuwa full kukuomba msamaha na kulia
 
Ndio hivyo mkuu, hakuna kukata tamaa. Vijana wetu wa sasa wana lawama nyingi sana hasa kwa serikali na hizi kauli za hakuna kazi... Kijijini nilipotoka, ugomvi wangu na dingi tofauti na ule wa kutengana na mama yangu ulikuwa ni kwa sababu niligoma kumpa pesa ya kwenda kunywea pombe na kula mishikakin siku ya mnada. Yaani nilikuwa naficha pesa porini na siku moja mafuriko ya mvua yakazibeba zote kwenye mfuko wa nailoni... lakini sikukata tamaa.

Nilikuwa naponda kokoto za ujenzi na nalipwa hadi Tshiling elfu 1 kwa siku kwa ndoo 20 za kokoto. Mida hiyo ya miaka ya 1985 na kuendelea, elfu 1 ilikuwa pesa ndefu sana. DIngi akanitimua toka nyumbani kwake mara tu alipo achana na mama yangu na mama kurudi kwao. Nilikuwa mtoto wa mitaani, na ilibidi niende site kuponda kokoto za mawe ili nipate pesa ya shule- primary school, wakati huo ilikuwa chini ya shiking elfu 5 ila baadae ilufutwa ( Serikali ya Nyerere). Nikaenda Dar, nikauza maji ya mikokoteni, pipi, kalanga na vifuko vya maji vya azam wakati huo, nikapendwa sana na madereva wa daladala hasa lile - Super Najmunisa- Karikaoo hadi Mwananyamala, na hata nauli nilikuwa sitozwi.. kumbuka nilikuwa mwanzoni kabisa kabla ya kwa mama Tambaza, nilikuwa naishi Yombo Dovyo na nilikuwa natembea kwa mguu toka saa 9 usiku kupitia vingunguti either hadi Magomeni nipande Super Najmunisa ( daladala) au kariakoo na niliweza kumaliza nilichokuwa nakitafuta.

Maisha haya, Mungu anijalie niyaandikie kitabu kabla hajaniita ili vijana wajifunze. Kukata tamaa ya maisha iwe mwisho kwa yeyote anayetaka kutoboa.
Hapo kwenye kitabu....itabidi ufanye hivyo mzee....Tena skills za uandishi unazo...unajua kueleza kwa maandishi
 
Back
Top Bottom