Ndoa ya Lola na Peter: Umri na ukabila unavyoitesa familia ya akina P-Square

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,378
Reaction score
3,383


Lola




Peter na Lola

Nimekuwa nikisikia kuhusu kutofautiana kwa Peter na Paul vijana wa Kinaijeria wanaounda kundi lao la P- Square.

Hivi karibuni waliibuka katika mitandao ya kijamii na kuufahamisha umma wa mashabiki wao kwamba wamamemaliza tofauti zao.

Lakini kumbe bado ugomvi wao unafukuta chini kwa chini, kwani hivi karibuni Peter amenukuliwa akisema kwamba kuisha kwa tofauti zake na familia alimozaliwa kutategemea iwapo tu mkewe Lola ataheshimiwa.

Inadaiwa kwamba mama yake Peter alimkataa Lola tangu mwanzo kwa sababau anatokea katika kabila la Yoruba wakati Peter anatokea katika kabila la Igbo. Kwa mila na desturi zao haya makabila hawaoleani kwa sababu zao wanazozijua, ingawa inadaiwa Igbo wanaamini kwamba wanawake wa Ki Yoruba wana mkosi na wanapenda kumiliki waume zao kwa maana wana sauti katika nyumba.

Lakini pia kuna tatizo la tofauti ya umri kati ya Peter na Lola. Kwa umri Lola ni mkubwa kuliko Peter na hiyo ndiyo iliyomjengea mama yake Peter hofu kwamba mwanaye atakwenda kumilikiwa na Lola na hatakuwa na sauti. kwa hiyo hata kabla hajafariki alishamkataa Lola kuolewa na mwanaye. Lakini Peter kwa kiburi keshamzaliwaha Lola watoto wawili, jambo ambalo limemuwia gumu kuvunja ndoa yake na Lola.

Kwa upande wa wanafamilia, karibu wote wamepinga ndoa yake kwa madai kwamba Peter amekwenda kinyuma na mama yake mzazi na kwa sababu alifariki akiwa bado ameshikilia msimamo wake ndipo hapo swala hilo linapozidi kuwa gumu.

The saga is continue...........
 
Nimekuelewa sana hapo uliposema karibia wote, siyo wote.....
Kwa kufwatilia kwangu kwa mbali nakumbuka Paul alikuwa mstari wa mbele kwenye hii harusi, na kama nakumbuka alisema yeye hahusiki na huo mkanganyo sababu Peter kampenda huyo na ni mkewe, sasa kaanzaje ugomvi baada ya kumkubali Lola?
Katika jamii ugomvi hauepukiki, iwe kwa ndugu au watu tu. Hili la kusingizia mtu fulani ndo chanzo cha ugomvi huwa kinanitesa sana. Huu ugomvi ungekuwa kati ya Peter na kaka yao ningekubali kabisa kuwa chanzo ni kutomkubali Lola, lakini kwa Paul? sijui......
Lakini hata kama chanzo ni kutomkubali Lola, nani mwenye kosa? ni Lola au hao wasiomkubali? yeye kapendwa na kapenda, aache kufwata moyo wake sababu third parties hawamtaki? who are they?
Asante The Boss kwa kunishtua hapa, najua unakumbuka uzi wangu, lol!
 
Last edited by a moderator:



Fixed Point
, nakubaliana na wewekw3amba Paul alikuwa mstari wa mbele katika harusi ya pacha mwenzie Peter, lakini kuna minong'ono kwamba kaka yao ana mchango katika tofauti zao.

Ngoja nifanye utafiti mdogo nitaendelea kuweka dondoo hapa
 
Msala wote huu hapa:


P-SQUARE: Peter gives condition for peace - Vanguard News
 

Fixed Point
, nakubaliana na wewekw3amba Paul alikuwa mstari wa mbele katika harusi ya pacha mwenzie Peter, lakini kuna minong'ono kwamba kaka yao ana mchango katika tofauti zao.

Ngoja nifanye utafiti mdogo nitaendelea kuweka dondoo hapa
Umeona eeehhhh!
siajabu huyo kaka mtu alikuwa anawaonea wivu wadogo zake na akawa anatafuta namna ya kuwatenganisha tangu zamani, hii ndo kachukulia loop hole. Na watazamaji badala ya kufanya analysis zinazofaa tuna-make conclusion kwa kutumia majungu...... sijui tutafika!
 
wanaijeria wametovuruga balaa

sasa ni kufuatilia tu, si joshua, si cocaine, si peter na paulo you name it

haya....
 


Fixed Point
, nakubaliana na wewekw3amba Paul alikuwa mstari wa mbele katika harusi ya pacha mwenzie Peter, lakini kuna minong'ono kwamba kaka yao ana mchango katika tofauti zao.

Ngoja nifanye utafiti mdogo nitaendelea kuweka dondoo hapa
Hizo tafiti utafanyia kupitia nini?
 
Wanawake ndo chanzo cha tatizo mahala popote pale duniani. Hata lingekuwa sio hilo kwakuwa washasogeza wanawake lazima wangekosana tu! Sumu ya eva kwa baba adamu pale hedeni itatutafuna sana!!
 
Kuingilia mahusiano ya watoto just kwa personal interest ni hatari sana. Wakwe wa aina hii ni hatari sana. Ils nimegundua wazaxi wanapenda sana kuingilia affairs za watoto walio na uwezo kifedha na mali!!! Wivu syndrome"!! Kina hohehahe hutasikia hata wakifuatwa hata akuoa fisi.
 
Si wavunjike tu watuwache tupumue.....................

Halafu Piere anaonekana ni stubborn sanaaa si ajabu yeye ndo anakuza mambo
 
Tusiposhikamana wakati huu watanzania,dhambi ya ubaguzi sisi pia itatutafuna!

Kwa Nigeria ni too much sio kama tunavyochukuliana kibongobongo hawa kwa ukabila hata Kenya hawaoni ndani wako too much Wayoruba, WaIgbo au WaHausa wana na tv station zao kabisa mbaya zaidi hali hii wanaichukulia hadi kwenye mambo ya kijamii mf kuoa au kuolewa... Cc Janjaweed
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…