Ndoa ya Prince Harry na mpenzi wake Meghan Markle yagharimu zaidi ya sh Bilion 103

Ndoa ya Prince Harry na mpenzi wake Meghan Markle yagharimu zaidi ya sh Bilion 103

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
Jumamosi iliyopita ilishuhudiwa sherehe kubwa ya harusi iliyoteka dunia kwa muda iliyokuwa inamuhusu Prince Harry na mpenzi wake wa muda mrefu Meghan Markle.

Ndoa hiyo ilihudhuriwa na wageni zaidi ya 4000 kutoka mataifa mbali mbali duniani huku mastaa wakubwa duniani kama David Beckham, Oprah Winfrey, Priyanka Chopra, Serena Williams na wengine wakiwa miongoni mwa walioalikwa.

1555.jpg

Je unafahamu gharama zilizotumika kuandaa shughuli hiyo? Basi ndoa hiyo inaweza ikaingia kwenye kitabu cha rekodi kuwa miongoni mwa ndoa zilizotumia gharama kubwa dunia.

Kwa mujibu wa Bridebook ambao wanashughulika na masuala ya harusi na Sherehe, umeripoti kuwa ndoa hiyo imegharimu kiasi cha paundi milioni 34 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 103 za Kitanzania.

Lakini pia ndoa hiyo imeweza kuzidi gharama za ndoa ya Prince William (Duke of Cambridge) na mkewe Catherine Middleton iliyofungwa April 2011 ambayo inadaiwa kuwa ilitumia kiasi cha paundi milioni 32.

Gharama za gauni alilovaa Meghan Markle ambalo limebuniwa na Claire Waight Keller limetajwa kugharimu kiasi cha paundi 300,000. Gharama ya gauni hilo limeweza kuizidi gauni la Cate Middleton alilovaa kwenye ndoa yake na Prince William ambalo liligharimu kiasi cha paundi 250,000 lililobuniwa na Alexander McQueen.

Hizi ni baadhi ya gharama nyingine za harusi ya Prince Harry na Meghan Markle:

Keki – £50,000
Muziki – £300,000
Mapambo – £130,000
Pete za ndoa – £6,000
Kupamba nywele na Makeup – £10,000
Gharama za fungate (Honey Moon) – £120,000
Vinywaji – £193,000
Chakula – £286,000
Gharama za ukumbi – £350,000
 
Hata mimi niliona ilikuwa nzuri bodi ya mikopo ya shule inahusika nanini hapa hii nchi ni nyingine ingekuwa hapa mtoto wa magu kafunga na gharama zote hizi zikatumika kwa harusi mngelalamika .
 
Kwan hawakusambaza kadi za ufadhili ka tunavyofanyaga huku bongo....ama waalikwa kaz yao ilkua kuhidhuria na kupiga vi2 2...vyote vilikua vishalipiwa!!?
 
kichwa chako kimajaa funza au? nimeuliza bodi ya mkopo we unaleta habari za njaa.

haya mambo ya mkopo yanaingiaje kwenye sherehe za harusi ya Prince Harry?
kwani watanzania wote tunategemea kusoma/kusomeshwa kwa mikopo?
Njaa zenu bakini nazo huko vyuoni....mambo ya wakubwa haya ..!!wanachuo someni acheni ulimbukeni!!!
 
Kwan hawakusambaza kadi za ufadhili ka tunavyofanyaga huku bongo....ama waalikwa kaz yao ilkua kuhidhuria na kupiga vi2 2...vyote vilikua vishalipiwa!!?
Wazungu hawana utaratibu huo
 
Wazungu hawana utaratibu huo
Asante,ckujua b4...I've never been in Europe ama hata nchi yoyote ya wazungu..hivi ko wazungu hawana utaratibu wa kusaidiana katika hali mbalimbali,mfano misiba na sherehe..!?nasikiaga kule wana ubinafsi sana yaan kila m2 yupo busy na mambo zake!!!
 
Sidhani kama ni Ubinafsi, ni Tamaduni zao wamezoea hivyo, na hakuna kulalamikiana. ..unatakiwa kujipanga mwenyewe, na kipande cha Ardhi unajijunulia kwa ajili ya nyumba yako ya milele.
 
Sidhani kama ni Ubinafsi, ni Tamaduni zao wamezoea hivyo, na hakuna kulalamikiana. ..unatakiwa kujipanga mwenyewe, na kipande cha Ardhi unajijunulia kwa ajili ya nyumba yako ya milele.
Ooh....ngoja nizichange change niende nkapate exposure kidogo.
 
haya mambo ya mkopo yanaingiaje kwenye sherehe za harusi ya Prince Harry?
kwani watanzania wote tunategemea kusoma/kusomeshwa kwa mikopo?
Njaa zenu bakini nazo huko vyuoni....mambo ya wakubwa haya ..!!wanachuo someni acheni ulimbukeni!!!
hhaha sawa
 
Back
Top Bottom