Ndoa ya Ronaldo: Mali zake hazitaguswa wakitengana kwa sharti amlipe mkewe posho ya milioni 300 kila mwezi

Ndoa ya Ronaldo: Mali zake hazitaguswa wakitengana kwa sharti amlipe mkewe posho ya milioni 300 kila mwezi

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
1787764800133.png


Cristiano Ronaldo na mchumba wake wa muda mefu Georgina Rodriguez walisaini makubaliano ya kabla ya ndoa (prenup) siku moja tu kabla ya harusi yao iliyofanyika mwezi huu August 11, 2026

Makubaliano hayo yanaweka mali zao tofauti na ndoa yao, mali na pesa za Ronaldo zinazoripotiwa kuwa zaidi ya £1 bilioni (takriban TSh trilioni 3.61), hazitakuwa sehemu ya mgawanyo nje ya mkataba waliosaini ikiwa watakuja kutengana (divorce)


Georgina anaripotiwa kupata $121,000 kila mwezi (takriban TSh milioni 320.3) kama posho yake binafsi wakati wakiwa pamoja ndani ya ndoa.

Georgina anapaswa kukubali jukumu kamili la malezi ya watoto wote, akiwemo mtoto ambaye Ronaldo alikuwa naye kabla ya kukutana naye.

Nyumba ya kifahari ya Ronaldo huko La Finca, Madrid, Hispania yenye thamani ya £5 milioni (takriban TSh bilioni 18.03), inadaiwa kusajiliwa kwa jina la Georgina na kuwa mali yake hata wakija kutengana.

Kampuni za Ronaldo, haki zake za picha, na uwekezaji wake vinabaki kuwa mali yake binafsi hata baada ya kutegana.

Iwapo Wangetengana yaarifa hizo zinadai Georgina atapokea:

$110,000 kwa mwezi maisha yake yote, takriban TSh milioni 291.2 kwa mwezi.

$500,000 za child support hadi watoto watapofikisha miaka 18, takriban TSh bilioni 1.32 kila mwezi

Magari 2 ya kifahari.

Likizo 2 za kifahari kila mwaka, zote zikiwa zimelipiwa.

Kwa kifupi: Georgina hataambulia mali za Ronaldo nje ya hizo za kwenye mkataba, Kila mmoja anabaki na mali alizopata au kujenga kwa jina lake, huku Georgina akipata malipo na manufaa ya ziada yaliyowekwa kwenye makubaliano hayo.
 
Uwezo wa kujiwndeleza kwa hizo hela atakuwa nazo sana
Kwanza ni maarufu tayari na pia kakutana na watu wengi maarufu duniani.

Hizo sio hela ndogo kwa kufanya chochote
 
Umeondoka jojina, umeniachia masikitiko,jojina jojina aaah ... Ooh georgina…siku uliondoka,uliniacha nakua na majonzi,umekwenda kuishi mbali namii ...

Ooh georgina…siku uliondoka,uliniacha nakua na majonzi,umekwenda kuishi mbali namii…georgina wa wamamaaa,sipati usingizi nikikumbuka,tulivyoishi mimi na we Georgina aaaa!!

Tangu umeondoka,,,umeniachia masikitiko,, sipati usingizi nikikumbuka,,,tulivyoishi mimi na wewe,,,,georgina wa mamaa

Ni wimbo mkuu,zilipendwa classic lyrics zake hizo hapo juu
Aina hii ya vijana ndo mmesababisha nchimbi ajiuzuru
 
Kwahiyo hata wakitengana bado mwanamke atalipwa kiinua mgongo Hadi anakufa...Njia ni hakimu style yaani asipate hata Mia mbovu hata wakitengana.
 
Back
Top Bottom