Katika ulimwengu wa muziki wa Injili ndani ya Afrika ya Mashariki, jina la
Phyllis Mutisya limekuwa likihusishwa na sauti tamu ya kumwinua mtu kiroho pale madhabauni. Mwanamama ambaye amekuwa akitoa huduma yake takatifu ya uimbaji na kumsifu Mungu.
Lakini hivi karibuni katika siku hizi tatu, upepo mbaya umevunja utulivu wa ndoa yake na mumewe Bwana
Tiras Muange. Mzee
Tiras amewapatia goli la mkono umoja wa Chama cha
KATAA NDOA kwani amejitokeza hadharani akimtaja mkewe kama mchepukaji sugu, akidai kuwa ana orodha ya wanaume zaidi ya ishirini ambao mwanamama
Phyllis amehusishwa nao kimapenzi ndani ya miaka 12 ya ndoa yao.
Majina yamechapishwa hadharani β kuanzia
Masila, Kyalo, Nzau, King Muli, hadi kwa maafisa wa kijeshi kama
Cpt. Dan.
Taarifa hii imewavunja moyo wengi, hususan mashabiki wa muziki wa Injili ambao walimwona
Phyllis kama kielelezo cha imani na utiifu pamoja na ucha Mungu.
Ndoa ni ngumu, na kashfa hii inatoa funzo kuwa pete haimaanishi uaminifu wa mioyo. Ni hadithi inayowasha mjadala kuhusu unafiki, tamaa na udhaifu wa kibinadamu hata kwa wale tunaowahusudu kama βwatakatifuβ.
Mzee baba
Tiras ameonesha kuwa ataendelea kuweka hadharani orodha kamili ya wanaume ambao wametoka kimapenzi na aliyekuwa mke wake. Ikiwa ni pamoja na majina ya wanawake ambao ndoa zao zimevunjika kutokana na waume wao kuonja penzi la
Phyllis Mutisya. Huko mitandaoni mambo imechemka hatari.
NDOA BHANA! WATU WANALIWA BALAA NA WAPO NA PETE NA WAMEWEKA NADHIRI MBELE YA SIR GOD.
MECHI INAENDELEA MPAKA SASA #KATAANDOA WAPO KIFUA MBELE.