Ndoa ya Tiras Muange na Phyllis Mutisya kimeumana, Usaliti madhabauni

Unamwaga mchele wote kwa kuku πŸ˜ƒ
 




Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Phyllis Mutisya, amefichuliwa na mumewe, Tiras Muange, kuwa na mahusiano na zaidi ya wanaume 20, atangaza talaka kupitia ukurasa wake wa facebook.

Post hio ilichanganya kiingereza na kiswahili, hili ni toleo la kiswahili pekee

.........................

hii inauma sana.. tuchukue nafasi kumtia moyo kaka yetu kwa magumu aliyopitia hadi akaamua kuachilia

Hakuna kitu huwa kinamuumiza mwanaume kama anapojaribu kuzungumza na mwanamke kuhusu TABIA yake inayomuumiza kila siku, lakini badala ya kumsikiliza, anapandwa HASIRA na kugeuza hali kumfanya mwanaume aonekane ndiye mwenye tatizo.

Tumepitia miaka 12 ya changamoto kubwa katika ndoa yetu. Kupitia dhiki na faraja, mabaya na mazuri, nyakati za chini na za juu za maisha yetu, tumepigania Upendo wetu na tukavuka milima na mabonde pamoja.

Ninapoitazama safari yetu na jinsi tulivyofika hapa, matunda mazuri yanaonekana: miaka 12 ya kusherehekea ndoa, watoto wetu, familia zetu, huduma zetu kwa Mungu, marafiki zetu, na mwishowe watoto wetu wa kiroho. Hata hivyo, matunda mabaya (matukio mabaya yanayojirudia) yanaendelea kunivunja moyo.

viapo tulivyokula tunapaswa kuwa waaminifu, tupendane, tuheshimiane na tuzeeke pamoja. Lakini, nikiangalia nyuma, haya mahusiano yamevunjika kwa sababu zinazojulikana vyema kwako.

Nyakati nyingi ulizokuwa na mapenzi ya siri, kutoroka kwenda kusex, usaliti katika vyumba vya kulipia ( hoteli
& Airbnb) na ukiwa kwenye safari za road trips, ni mambo ambavyo hayana thamani kwa madhara uliyosababisha. Katika miaka 8 sasa, umempa moyo wako si mwanaume mmoja bali wanaume wengi, wakiwemo wenye ndoa, huku ukivunja mioyo ya wake zao. Naomba wake zao wapate neema ya kukusamehe - Masila, KKyalo, Nzau, KSamuel, Skiilu, Benito, MTitus, King Muli, Major Jackson, BSingi, SMutuku, Polycarp, NRichard, KSila, MStephen, Cpt.Dan, KJohn, EGriffins, Nyanzwii, Tash, Zabuh na wengineo.

Kwa sasa, tumefika kilele cha uhusiano yetu kwa pamoja. Wakati wa kubadilika umeisha. kuwasiliana kwetu ni shida. Kufahamikiana ni taabu. Mambo tunayotumaini kuwa hayatatokea kila tunapofungua ukurasa mpya wa penzi letu yanaendelea kujirudia na si hivyo tu, yanaporudiwa huwa ni kwa kiwango kikubwa na machungu zaidi. Mbona yafanyike tena kwa kurudiwa? Kwanini urudie kuleta madhara na maumivu katika usaliti, udanganyifu na uzinifu kwenye ndoa ?

Mbona usiniheshimishe kwa vikao vyako ? Mbona hupeane sifa mbaya kunihusu hata kwa familia, na unajua wasema uongo? Mbona usiheshimu madhabahu unayo hudumu?

Moyo wangu una maumivu na maisha yangu yamevunjika. Ninakosa amani kwa kutokupata hali na mazingira sahihi ya kupona. Unavyolipukwa na hasira zako, kunikelelesha bila sababu, madharau na kunikosea heshima vimenishusha na kunimaliza.

Mungu wangu nakuomba unipe amani inayozidi uelewa wa wanadamu. NIMEKUACHIA UWE NI NDEGE HURU, Nenda ukafanye uzinzi kwa uhuru wote.

NAHITAJI AMANI NA NAFASI YA KUPATA AHUENI KATIKA HAYA YOTE.

.........................

Usisahau ku like(follow)page yetu
 
Ndoa tamu ila usaliti unapoingia inakuwa chungu, unajaribu ujizime data uzuge hujui anachokifanya mke wako mambo yaende lakini kuna kiwango huwezi kuzidisha uvumilivu
 
Mmh! Diamond aliona mbali sana, binafsi Wakenya huwa siwaamini, hata wale wa Bibilia wanao jiita Watakabifu...
 
Wewe unamwita my dear wife watu wanampa nao wa mgonngo kwa foleni. Aisee kataeni ndoa
 
Wanawake bana ni kuwapenda tu kwa macho.
Usilete lete upendo kwao, labda kwa mamaako tu.
Hata jana kuna janamke librazil limenikera masaa 8 tuko kazini.
Nikaona niondoke maana ntamuwasha makofi nifungwe ananivuta shati
'unaenda wapi njoo tunywe chai"
Aisee nilimpiga jicho nafkiri alitaka kunya kabisa,
Sikutoa jibu lolote nikatimka zangu.
 
Mhh hapo umefurahi.
 

Hao wabrazil ndio jehanam kabisa, Mungu akurpushie mbali
 
Hata ungekuwa wewe mke wako anasafiri miezi mitatu ungefanyaje?
 
Atakuwa bado anampenda si bure, orodha yote hiyo na bado ameweza kuandika page ndefu zaidi ya zile gazette la mzalendo. Huyu mzee pia ana walakini!
 
Si umemaliza kusoma,
Mwaga na wakwako
 
Hapo sijui mimi ndio sijaelewa kinge'nge ama vipi......eti wako Mbooni ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…