Ndoa yangu inateketea

Pole ndg, kwa sasa nafikiri pambania afya yako maana afya ni mtaji mkubwa, zungumza nae na mzazi wake wa kiume kama yupo pia, ukipata nafuu utaenda kumwona na kuzungumza kwa ndani zaidi, maana kwa hali uliyonayo hapo hm uamuzi wowote unaweza athiri afya ya mama yako mzazi tena,
 

Mwanamke akikupenda mwanaume atafanya chochote kile kuwa nae, ila akimchoka mwanaume ni mbaya mnoooo

Pole sana mc night mimi ningekushauri ufanye uweke nguvu yako kwenye kujenga maisha yako. Maisha yako ni yako hata mapacha wenyewe wanaishi kwenye mfuko mmoja lakini kwenye maisha halisi kila mmoja anasimama mwenyewe

Kaka zangu, wanangu wa kiume jengeni maisha yenu mjenge heshma itakayowapa amani na maamuzi sahihi kwenye nyumba zenu
 
Nafikiri Nakuelewa mkuu. Nimetunza hii
 
Yaani unaongea kinyonge sana mpaka nashindwa kukushauri....
 
kuishi na mwanaume hana hela ni kipaji,punguza makasiriko tafuta hela
[emoji1787][emoji1787]tatizo ni pale hana hela na bado ana tabia mbayaa, inachosha sana. Bora akose hella halafu ajiheshimu, tutaishi kwa amani.
 
Daaah! Mganga tena??
 
Pole ndugu,huo ni mtihani,unaopaswa uushinde,huyo mwanamke hakupendi na usilazimishe akupende,ATAKUUMIZA ,aliye wa kwako,tayari MUNGU kamuandaa,inahitaji uvumilivu,UTASHINDA!
 
Kuna "wife material" na "material wife" ....jiongeze brother [emoji846][emoji846]
 
Pole kwa yanakusibu.
Usilazimishe sana mapenzi hata kama unaumia vipi.
Kama umeshajaribu kurudisha amani ikashindikana na unatambua kabisa hujamkosea kitu kaa kimya usimbembeleze tena.
Fanya mambo yako tafuta Kazi taratibu. Saidia watoto wako pale unapoweza. Jikeep busy na mambo mengine kama ni wako atarudi tu.
 
Pole sana mkuu, hatua ya mwanamke kukutamkia kuachana jua hapo ndoa haipo. Ushauri wangu: chukua watoto wako, pambana unavyoweza kuwapatia nahitaji yao na kuwaonesha upendo wa hali ya juu hii itakusaidia kuwa busy na kumsahau kabisa huyo mwanamke. muda wa maisha duniani ni mchache sana hivyo usiutumie muda vibaya kulazimisha mapenzi/ndoa badala ya kupambana kutafuta ili watoto wako wakukumbuke hata utakapokuwa haupo.
 

Safi sana mwanaume ni msimamo sio kuyumbishwa hapo nakupongeza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…