Ndoa yangu inateketea


Mpaka hapo huna mke. Mruhusu aende ila kabla ya kumruhusu muombe akutumie email, akupe sababu.
Hapa atakusaidia kutunza ushahidi maana siku inakuja ataomba umsamehe hii itatumika. Pia wanawake wanajua kutufarakanisha na watoto hivyo ni muhimu kupata kauli yake kwa maandishi ukayatunza kwa utetezi mbele huko.

Wewe kwa sasa ni ‘kapuku’ kwa mtazamo wake, amempata njemba mmoja aliyemfanya aombe uhamisho bila malipo. Kwa sasa anapumuliwa na huyo njemba hajui kwamba utamu wake ni kwasababu yupo kwenye ndoa.

Kama una uhakika hujamtenda wewe, muache. Iko siku utashangaa anaomba muongee. Inaweza kuchukua muda ila atarudi.

Pole mzee
 
Hakuachwa, aliacha. Elewa!
Kuacha na kuachwa kwa lugha ya kitaalamu ina maana moja.Ikiwa na maana kuwa kama umeacha kuna vitu vilisababisha au vilikukwaza,na kama alikukwaza ina maana alitoka nje ya makubaliano yenu,kwa hiyo kutoka nje ya makubaliano yenu.....ina maana amekuacha; mkuu nadhani umenielewa
 
Mm sijui kwann wanaume mnakosa msimamo katika mambo ambayo ni wazi tuachane nahilo nakupa pole ndugu yangu
 
Siamini km mtu unaweza acha ndoa tu ghafla....

kuna mambo hajasema
Ama mawasiliano ndani hayakua mazuri muda mrefu...
 
Maisha yenyewe tunaishi mara moja,kwanini uteseke na mtu umemjua akiwa mtu mzima ,achana nae fanya yako usije kufa na msongo....mimi na roho ngumu sana yani ukiniletea za kuleta siku unaondoka,nami nahamishia hawara siku hiyohiyo tena wewe unapakia mabegi yako,yeye mda huohuo anapakua mabegi yake,mapenzi huwa hayanipa shida kamwe
 
.. Mkuu, hivi kweli wapo Waganga wanaoweza kuyafanya hayo?? For real??
 
Hako kademu kasenge kana mambo ya kitoto kutopandishwa mshahara ndiyo useme unataka ndoa ife?

Nigga just secure your kids muache aishi maisha yake.
 
Pole sana Mkuu hakuna ndoa hapa.
 
Kuishi na mwanamke is an ART ukijua hilo hutakaa uumie au uumizwe na mwanamke
 
Its not always about money, Unaweza ukawa na pesa na bado mke akakukimbia, this things happens to everyone, awe maskini au tajiri
True Mkuu. Tajiri Mkubwa duniani Bill Gates hao wanamwagana na Mkewe....!
Ni kweli Mkuu. Sio kila mara kwamba inahusu kuwa ama kutokuwa na hela...[emoji853][emoji853]
 
Kweli wengi tunatamani nafasi kama hiyo ya kuambiwa tuachane maana viambatanisho havipatikani
 
Mbona alishakuacha Sikh nyingi.
Kitendo cha kuomba UHAMISHO TU.
Ilikuwa IMEIIISHA HIYO.

Najua hutaki kusikia hii.
Ila ndo uhalisia.
MUACHE!!!!!!!!!!
Unaumia ila utapona
Unateseka ila utapona
Unavurugwa ila utapona.
MUDA NI DAWA NZURI MNO.
Uruhusu ukusaidie kwenye hili.
Usipigane vita ambayo umeshashindwa.
 
Unaoa mkufunzi wa chuo kikuu, halafu wewe tia maji tia maji!
Wazazi wetu wanaamin ukiwa mkufunzi wa chuo (lecturer) ina maana una akili sana, sasa how come pamoja na hizo akili aishi na mtu tia maji tia maji, lazima wamshauri akufutilie mbali.


Ukweli kinachokuweka na ww karibu na hutaki kuachana na hayo matesi ni hilo hilo unapowaza kwamba mke wangu lecturer na itakuwa asilimia kubwa ndio mtunza familia, najua wanaume wenye familia za hivyo wanalegeaga sana hawakazi kitu ambacho mwisho wa siku wake zao wanaanza kuwakazia wao.

Mm siruhusu mke wangu kukaa kaa au kwenda kwenda kwao ovyo ovyo hata anapenda yeye.

Ukaruhusu ahamie na afikie kwao kisa karibu na kazini kwake, kwan dar hapo hakuna chumba cha elf 50 angepanga na kuanzia si ana mshahara...

Anyaway mm nakushauri kigumu na kiume zaidi, demu wako kapata mraruaji anamtawanya kweli kweli, kama hutakubaliana na kuachwa utakufa siku sio zako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
[/QUOTE]
.. Mkuu, hivi kweli wapo Waganga wanaoweza kuyafanya hayo?? For real??
Wapo Mkuu, na kwa maoni yangu hiyo ndo kazi rahisi zaidi. wengine watakwambia upeleke nguo yake, wengine watakwambia utaje jina lake, na wengine watakupa dawa ukachome umwite na zote zinafanya kazi.

Hizi ndoa zinazovunjika sio bure kwa asilimia nyingi ni mambo ya kiroho yanachangia.
 
Maelezo yako yanaonyesha ni jinsi gani ulivyo mshirikina,acha mrudie Mungu
Kuna mwenzako ni Mchungaji alikuja kuniambia aniongoze sala ya toba ili Niokoke, nikamuuliza, huko Kanisani kuna Mama anashutumiwa kuwa mchawi, kwanini hawamfukuzi? Na kwanini mimi nikakae pamoja na mtu ambae ameharibu hata familia yangu?

Mimi siwezi kuishi maisha ya kinafiki, na watu kama nyie ndo wale mnaenda kwa waganga usiku wa manane msijulikane...
 
Pole sana,ila
Pole sana, ila kwa sasa jikite kwenye matibabu upone vizuri kwani afya bora ndiyo mtaji
Sasa kwa akili yako yote hayo yanawezekana kwa binadamu? Hao wengine wanawezaje kuheshimu ndoa na wakawa na upendo na Waume zao japokuwa hawana sifa zote hizo? Binafsi naona ni hatari Sana kumng' ang' ania mwanamke Kama kasema hakutaki. Maana anaweza akakuletea mauzi ukamuua na kuishia jela.
 
Pole na majanga yaliyokupata broo,
Binafs mm bdo sijaingia kwenye ndoa ila shida kubwa nlipoiona hapa n kukubali mkeo akuache kijijini aje mjini,alaf hata kama ukweni n jiran na udsm na kwenu ni mbali lkn kama mwanamke ulishamlipia mahari means siyo wa kule kwao tena angepaswa aishi kwenu,

Alaf mwisho n kwamba huyu mpaka ameamua kuja dar hata kama wewe ndio ulimpambania akapata uhamisho inaonesha alikua na jambo lake muda mrefu tu,huenda alikua amemkumbuka ex wake ndio akaona mbinu bora n kuhamia dar ili iwe rahisi kuwa nae


Hitimisho,mshirikishe kwenye hili jaribu kaka,jitahd upone kwanza alaf ujaribu kumuweka karibu kimazingira,ikishindikana kama ukikubal ujaribu plan b ya mganga kama walivyokushauri


Alaf nyie mnaosema amuache iv mnajua nguvu ya mapenzi??angekua wa kumuacha asingekuja kwenu kuomba ushauri.
 
Huna mke,mwache aende tu
 
Upo Saudia Arabia mkuu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…