Umeona eeh.
Jamani hivi kama mume au mke ataacha kwa kiwango kikubwa kuonyesha love kwa maneno na vitendo, mumewe au mkewe mnategemea atapata wapi love??? Kila mtu anapenda kuwa loved; je kuolewa au kuoa ndio mwisho wa kupendwa au ndio tukubali kuwa mapenzi ya ndoa ni ya kibubu bubu; mradi watu wana do basiiii? Ukioa/ukiolewa ndio mwisho wa mtu kupendwa????
Nina rafiki yangu yeye huwa ananiuliza, hivi NK kweli mume wangu ananipenda mbona ana wanawake wengi sana? (kimoyo moyo najiuliza yeye hajuhi mi ntajuaje?). Afu huyo huyo anajijibu; lakini angekuwa hanipendi asingeweka picha yangu ofisini kwake (anajipa moyo).
Sasa mkiwapa wenza wenu sababu za kujiuliza maswali kama haya jueni mnamkaribisha shetani. Maana huyo rafiki yangu ni bomba akikwambia hajaolewa wala hana watoto utakubali; na watu wanamsumbua sana japo wanajua ni mke wa mtu. Sasa mumewe ka relax tu kisa keshamuweka ndani. Shaurilenu. Kuna siku huyo dada aliniacha hoi tulikuwa tunaongelea kufunga kizazi akasema sifungi ng'o nikiachika nikaolewa tena ? Meaning ameshaangalia uwezekano wa kuanza new life na mwanaume mwingine.
Kuna wanaume badala ya kuonyesha mapenzi kwa wake zao wao wako busy kujipendekeza kwa ndugu wa mke; wanadhani watawasaidia siku watakapopigwa chini. Lol. Unakuta mtu ana credibility kubwa kwa wakwe lakini home sifuri.
Mpende mkeo bana otherwise atapendwa na wenzio.
Na sie wanawake tuanze kuonyesha mapenzi ya wazi kwa waume zetu tuone kama hawata respond. Anza kumfanyia suprises ofisini na home; anza kumkisi mkikutana baada ya kazi. Fanya hivyo kwa hata miezi sita kama hata respond basi huyo ana lake jambo.