Ndoa za makaburi janga kwa wanawake, watoto mkoani Mara

Ndoa za makaburi janga kwa wanawake, watoto mkoani Mara

Rhobi Samwel......🤣
Wanaharakati wa Bongo Wamekaa Kimkakati sana.
Anyways🤐
Wadau hamjamboni nyote?

He unafahami ndoa za makaburi wilayani tarime rieya nacserengeti mkoani Mara?

Kwa jamii ya Wakurya wanaoishi katika Wilaya za Tarime, Butiama, Rorya na Serengeti ni jambo la kawaida kuona familia ikichumbia na kuoa binti kwa ajili ya kijana wake wa kiume alifariki dunia kabla ya ndoa, lakini akiwa amefikia umri wa kuoa lakini.

Ndoa za aina hiyo hujulikana kama ndoa ya makaburi, zikimaanisha binti anayechumbiwa huolewa na mwanaume ambaye tayari amefariki dunia na kuzikwa.

Lengo la ndoa za aina hii, wenyeji wanasema ni kuendeleza jina na ukoo wa kijana aliyefariki kabla ya kuoa, kwa kuwa watoto wote wanaozaliwa na mwanamke aliyeolewa kwenye ndoa ya makaburi, huitwa kwa jina la marehemu licha ya ukweli kwamba amewazaa na mwanamume wengine.

Kwa mila na desturi za Wakurya, anayetoa mahari ndiye mwenye haki ya watoto watakaopatikana na wote huitwa jina lake hata kama hajawazaa.

Hii ndiyo maana watoto wanaozaliwa na mwanaume mwingine kwa mwanamke wa Kikurya aliyeolewa kwa kulipiwa mahari na akaachika bila mahari ya mume wa kwanza kurejeshwa, wote uhesabika wa mume wa kwanza aliyetoa mahari.

Kutokana na mila hiyo, mwanamke aliyeolewa katika ndoa ya makaburi yuko huru kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuzaa na mwanaume yeyote ampendaye ili kupata watoto wa kuendeleza jina na ukoo wa kijana ‘aliyemuoa’, yaani aliyefariki kabla ya kuoa wala kupata watoto.

Ndoa za aina hii zinakaribia kufanana na ile ya “nyumba nthobu” inayopatikani pia katika jamii ya Wakurya, ambayo mwanamke ambaye hakujaaliwa kupata watoto lakini ana mali, anaweza kumtolea mahari mwanamke mwingine na “kumuoa” kisha watoto wote atakaowazaa muolewaji wanakuwa wa mwanamke aliyemlipia ma
 
Katibu wa Muungano wa Koo 12 za Wakurya, Mwita Sibora anasema mila hiyo ni muhimu kwa kuwa endapo familia haitatekeleza mila hiyo kwa kijana wao aliyefariki basi kuna uwezekano wa familia hiyo kukumbwa na mabalaa na hata kutoweka kabisa.
So wanaolea mizimu yaani watoto kuwaunganisha na mzimu wa mtu aliyekufa.
 
"Katibu wa Muungano wa Koo 12 za Wakurya, Mwita Sibora anasema mila hiyo ni muhimu kwa kuwa endapo familia haitatekeleza mila hiyo kwa kijana wao aliyefariki basi kuna uwezekano wa familia hiyo kukumbwa na mabalaa na hata kutoweka kabisa"

Hii kauli ni tatizo
Kauli ya mental slaves
 
Naona watu mbachangia kitu msicho kijua. Mleta mada nae Kuna sehemu kapindisha ukweli.
Nisikilizeni sasa.-

Hizi Mila hazidumishwi na familia masikini na haiko kama mleta uzi alivyoeleza.

Ikitokea mtu ameolewa Kwa staili hizi basi jua atapata sapoti kama vile ambavyo angeolewa na mwanaume.

Hao wanaojidai kutoa ushuhuda ni yake magube gube yaliyoshindikana na kukimbia miji.
 
Naona watu mbachangia kitu msicho kijua. Mleta mada nae Kuna sehemu kapindisha ukweli.
Nisikilizeni sasa.-

Hizi Mila hazidumishwi na familia masikini na haiko kama mleta uzi alivyoeleza.

Ikitokea mtu ameolewa Kwa staili hizi basi jua atapata sapoti kama vile ambavyo angeolewa na mwanaume.

Hao wanaojidai kutoa ushuhuda ni yake magube gube yaliyoshindikana na kukimbia miji.
Ha ha, mabeijingi aka masimbe ndiyo yanaharibu utamaduni.


Mie nimeoa mkurya, licha ya kuwa na kazi ya umma, tena mganga mfawidhi lakini Huwa namkerembesha Kwa makusudi na anaitii hatari.



Wakurya wanapenda mwanaume mbabe kiasi na mwenye misimamo mikali. Wanagongana balaaaaa
 
Duh mila za ajabu sijawai ziona tangu nizaliwe, mara kuna mambo ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom