Wadau hamjamboni nyote?
He unafahami ndoa za makaburi wilayani tarime rieya nacserengeti mkoani Mara?
Kwa jamii ya Wakurya wanaoishi katika Wilaya za Tarime, Butiama, Rorya na Serengeti ni jambo la kawaida kuona familia ikichumbia na kuoa binti kwa ajili ya kijana wake wa kiume alifariki dunia kabla ya ndoa, lakini akiwa amefikia umri wa kuoa lakini.
Ndoa za aina hiyo hujulikana kama ndoa ya makaburi, zikimaanisha binti anayechumbiwa huolewa na mwanaume ambaye tayari amefariki dunia na kuzikwa.
Lengo la ndoa za aina hii, wenyeji wanasema ni kuendeleza jina na ukoo wa kijana aliyefariki kabla ya kuoa, kwa kuwa watoto wote wanaozaliwa na mwanamke aliyeolewa kwenye ndoa ya makaburi, huitwa kwa jina la marehemu licha ya ukweli kwamba amewazaa na mwanamume wengine.
Kwa mila na desturi za Wakurya, anayetoa mahari ndiye mwenye haki ya watoto watakaopatikana na wote huitwa jina lake hata kama hajawazaa.
Hii ndiyo maana watoto wanaozaliwa na mwanaume mwingine kwa mwanamke wa Kikurya aliyeolewa kwa kulipiwa mahari na akaachika bila mahari ya mume wa kwanza kurejeshwa, wote uhesabika wa mume wa kwanza aliyetoa mahari.
Kutokana na mila hiyo, mwanamke aliyeolewa katika ndoa ya makaburi yuko huru kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuzaa na mwanaume yeyote ampendaye ili kupata watoto wa kuendeleza jina na ukoo wa kijana ‘aliyemuoa’, yaani aliyefariki kabla ya kuoa wala kupata watoto.
Ndoa za aina hii zinakaribia kufanana na ile ya “nyumba nthobu” inayopatikani pia katika jamii ya Wakurya, ambayo mwanamke ambaye hakujaaliwa kupata watoto lakini ana mali, anaweza kumtolea mahari mwanamke mwingine na “kumuoa” kisha watoto wote atakaowazaa muolewaji wanakuwa wa mwanamke aliyemlipia ma