Mbu ndugu yangu nina miaka 5 na miezi 3 sasa kwenye ndoa. Ndoa ni mbichi kila iitwapo leo. Nikimpigia simu mke wangu akiwa kazini huwa anafurahi hamna mfano, kwa nini? Kwa sababu tunaaminiana wala swala la kuchungana halimo akili mwetu.
Mbu ndugu yangu nina miaka 5 na miezi 3 sasa kwenye ndoa. Ndoa ni mbichi kila iitwapo leo. Nikimpigia simu mke wangu akiwa kazini huwa anafurahi hamna mfano, kwa nini? Kwa sababu tunaaminiana wala swala la kuchungana halimo akili mwetu.
Mbu imagine mko wawili tu home na mkeo ina maana hamtasaidizana?
huh...nadhani kweli sijui kugusa, ...sipendi kugusa halafu mtu hapo hapo anataka muache shughuli zote 'mkalale',...Ukikataa ananuna, eti kwanini basi ulimgusa, huh!...
...ushachunguza kinachomfurahisha? bora tu usijue bana.
Yeah subili Ndoa yako ichanganye mchokane utaona utaanza kuambiwa ufue nguo uoshe vyombo mm naenda saloon we acha bana
Ni upendo kutoka kwangu full stop.
Mnachekesha nilisoma kitabu cha Obama kuna sehemu anasema mkewe alimpigia simu akamwambia kuna ants jikoni na bafuni so akitoka kwenye mjengo akanunue.Obama anashangaa kama Mcain na Kenedy huwa wanaambiwa wapitie dawa za ants wakitoka kwenye mjengo....tena akiwa saloon anakupigia simu anakwambia; "ukishapika mchuzi, anza kukata kata vitunguu vya kachumbari, na usisahau kunikunia nazi...!" kwa mbaaali unawasikia kina dada huko salooni wanacheeeeeeka!
sasa mbu ulikuwa unagusa mko ukumbini na dada na watoto wamelala chumba cha pili nini? maana wanaume wengine hawaoni raha kama hawajagusa huku wanatiza mpira!
wife anataka aguswe chumban, apate ajifyarague bila ya wasi wasi wa watoto kusikia kinachoendelea
Leo najiokotea mengi kweli kwenye hii mada.....ila mkono unauma sasa kwa kucut n paste😎
Ooohh nilitaka andika tiGo...! upendo
Mbu umenichekesha hapo mahitaji muhimu na ya kibinadamu kama yapi?
Mueleze kwa upendo umuhimu wa yeye kusimama kama mama kwenye nyumba yake. ni kweli wadada wanatakiwa watusaidie tu na sio ytuwaachie majukumu yote, wote baba na mama wawe responsible hapa, nafurahi kwamba unaplay part yako vizuri sana kwama ni kweli unafanya yote haya, endelea wala usikate tamaa, mingine mitihani jamani.thanks kwa mliochangia na mnaoendelea, nashukuru pia nimegundua kuna wadau wa tegeta by night,zero,nyamachabes, fyatanga, kimara kwa mushi, usangule n.k....nitatoa ofa ya tubia tuwili siku moja ila kwa kuwa humu jf tuna hide id, basi usishangae utakapopata bia toka kwa anonymous
back 2 ze mada!
naomba nieleweke kwamba nia yangu si ku-display mfumo dume ule wa kizamani kama ilivyotafisiriwa na baadhi ya wachangiaji, binafsi huwa naupinga sana na mimi ni mfano mzuri wa wababa ambao huwa wanafanya yale ambayo nikijieleza hapa itabidi nitafutiwe mtaalamu wa ku-defuse malimbwata!huwa nayafanya mengi kwa nafasi yangu, lakini wajameni hivi kweli ni sahihi mama karudi nyumbani saa kumi jioni, fine anatakiwa kupimzika, dada kakaa na watoto na kuhangaikia nyumba tangu asubuhi hawampi hata nafasi ya kupumzika, wa shule wanarudi saa kumi na moja, mama unaamka kumdai dada chai, waliorudi shule nguo zao na maandalizi ya kesho, mama unademand chai ukiwa unakodolea macho luninga yako! Baba anarudi, dada huyu huyu anaacha alichokuwa anakifanya kukimbilia kufungua geti!anakupokea na kukukaribisha, mama bize kwenye luninga, dada bila kuambiwa anamletea baba chai, baada ya chai baba unaingia kwenye kazi za nyumbani na kumuacha mama akiendelea kutazama isidingo, saa mbili unarudi kuangalia taarifa ya habari, mama ...daadaaa vipi hicho chakula bado? unamdai mtoto notebook unakuta kuna msg ya jana toka shuleni, wee jana ulichelewa kazini umewakuta wamelala! ukiuliza mama jibu sijaiona, dada akisikia .....baba samahani niliona jana lakini nilisahau kukuambia, jana mama alikuwepo tangu saa tisa mchana! dozi ya dawa za watoto lazima uhakikishe umemuelekeza dada, hata kama kwa bahati mbaya hukuweza kumpeleka mtoto hosp, alipelekwa na mama kwa shingo upande! ukimwachia mama kama si kumpa kwa muda tofauti basi kampunguzia au kumuoverdose mtoto!!!mama huyu huyu hajui iliko shule wanakosoma wanae, hana hata contact moja ya mwalimu wa mwanae!! jamaaaaaaani baba huyu atashika mangapi!?bado 95% ya matumizi ya nyumbani lazima yatoke kwa baba!
kwa upande wa huyu dada, hivi huwa hawachoki? hawana haki ya kupumzika na kuthaminiwa? ukipropose kumuongezea hivyo vijisenti vyake utasikia ...aaah zinamtosha, kwanza nyingi sana (20,000/= hiyo!!)
Yeah subili Ndoa yako ichanganye mchokane utaona utaanza kuambiwa ufue nguo uoshe vyombo mm naenda saloon we acha bana
...mwingine kaka yeye anachojua ni kufanyiwa tu mfano
1. Anaamka asubuhi anakuamsha ukamwekee maji kwenye ndoo (na yanatoka bombani na ni master bedroom)
2. Umwekee dawa ya meno kwenye mswaki (usipoweka ataoga kisha atatoka kuja kuulizia mswaki wake)
3. Anatoka bafuni (hapo unakuta pant yake kaivua kaitupia kwenye sink anasubiri uje uife!)
4. Akitoka ushampigia pasi anavaa, anakunywa chai ulomwekea kisha huyooo funguo za gari zi wapi na akifika ndani ya gari ni honi mtindo mmoja unamchelewesha na usipokimbia na viatu mkononi anakuacha unakwenda ofcn kwa daladala au ukifanikiwa kuingia kwenye gari basi kusemwa mtindo mmoja unamchelewesha teke.
MCHANA KUTWA HATA KUKUPIGIA SIMU YA SALAMU AU SMS YA I MISS YOU!
5. Akirudi jioni akute chai yake mezani na maji bafuni
6. Atizame TV huku akisubiri chakula au asome magazeti yake
7. Akishakula huyooo kitandani analala huku akisubiri wewe uje ushushe neti na kumfunika na shuka!
8. Uingie kitandani baada ya kumaliza kazi zako akudake tayari kwa chakula cha usiku.
The life continues!
Kwa style hii kweli unategemea mkeo atakuwa anamapenzi na wewe? Si atajihisi hana tofauti na huyo housegirl jamani!
Jamani mara moja moja ukinisaidia kushusha net au hata kunipigia na mimi pasi I tell you nitaikumbuka kwa muda mrefu na moyo wangu kukongwa vilivyo!!