Ndoa za siku hizi

Ndoa za siku hizi

Mbu ndugu yangu nina miaka 5 na miezi 3 sasa kwenye ndoa. Ndoa ni mbichi kila iitwapo leo. Nikimpigia simu mke wangu akiwa kazini huwa anafurahi hamna mfano, kwa nini? Kwa sababu tunaaminiana wala swala la kuchungana halimo akili mwetu.

Yeah subili Ndoa yako ichanganye mchokane utaona utaanza kuambiwa ufue nguo uoshe vyombo mm naenda saloon we acha bana
 
Mbu ndugu yangu nina miaka 5 na miezi 3 sasa kwenye ndoa. Ndoa ni mbichi kila iitwapo leo. Nikimpigia simu mke wangu akiwa kazini huwa anafurahi hamna mfano, kwa nini? Kwa sababu tunaaminiana wala swala la kuchungana halimo akili mwetu.

...ushachunguza kinachomfurahisha? bora tu usijue bana.
 
...nadhani kweli sijui kugusa, ...sipendi kugusa halafu mtu hapo hapo anataka muache shughuli zote 'mkalale',...Ukikataa ananuna, eti kwanini basi ulimgusa, huh!...
huh
 
Yeah subili Ndoa yako ichanganye mchokane utaona utaanza kuambiwa ufue nguo uoshe vyombo mm naenda saloon we acha bana

...tena akiwa saloon anakupigia simu anakwambia; "ukishapika mchuzi, anza kukata kata vitunguu vya kachumbari, na usisahau kunikunia nazi...!" kwa mbaaali unawasikia kina dada huko salooni wanacheeeeeeka!
 
sasa mbu ulikuwa unagusa mko ukumbini na dada na watoto wamelala chumba cha pili nini? maana wanaume wengine hawaoni raha kama hawajagusa huku wanatiza mpira!

wife anataka aguswe chumban, apate ajifyarague bila ya wasi wasi wa watoto kusikia kinachoendelea
 
Leo najiokotea mengi kweli kwenye hii mada.....ila mkono unauma sasa kwa kucut n paste😎
 
...tena akiwa saloon anakupigia simu anakwambia; "ukishapika mchuzi, anza kukata kata vitunguu vya kachumbari, na usisahau kunikunia nazi...!" kwa mbaaali unawasikia kina dada huko salooni wanacheeeeeeka!
Mnachekesha nilisoma kitabu cha Obama kuna sehemu anasema mkewe alimpigia simu akamwambia kuna ants jikoni na bafuni so akitoka kwenye mjengo akanunue.Obama anashangaa kama Mcain na Kenedy huwa wanaambiwa wapitie dawa za ants wakitoka kwenye mjengo.
Any way maisha ni jinsi mnavyofurahia the way mnavyoishi
 
sasa mbu ulikuwa unagusa mko ukumbini na dada na watoto wamelala chumba cha pili nini? maana wanaume wengine hawaoni raha kama hawajagusa huku wanatiza mpira!

wife anataka aguswe chumban, apate ajifyarague bila ya wasi wasi wa watoto kusikia kinachoendelea

...aaaarggghh, sasa hii mada nyingine tena. Yaani kugusa pia kuna mipaka? Mke wako mwenyewe uibie ibie wapi pa kumgusa? umvizie chumbani, mmefunga mapazia, msubirie mmezima taa, gubigubi ndani ya shuka tena mkinong'ona ndio umguse? No way bana..

 
mbu unanifanya nitoke kwenye mada.......lakini mkiwa na watoto lazima 'muibie' fulani hivi kugusana. ......watoto wasijekuwafuma wakapofuka bure!

ndoa lazima kuwe na sacrifices kila upande. kubali kulalia upande wke pia wakati wengine ili na yeye asione tabu kulalia uande wako muda mwingi.
 
thanks kwa mliochangia na mnaoendelea, nashukuru pia nimegundua kuna wadau wa tegeta by night,zero,nyamachabes, fyatanga, kimara kwa mushi, usangule n.k....nitatoa ofa ya tubia tuwili siku moja ila kwa kuwa humu jf tuna hide id, basi usishangae utakapopata bia toka kwa anonymous

back 2 ze mada!
naomba nieleweke kwamba nia yangu si ku-display mfumo dume ule wa kizamani kama ilivyotafisiriwa na baadhi ya wachangiaji, binafsi huwa naupinga sana na mimi ni mfano mzuri wa wababa ambao huwa wanafanya yale ambayo nikijieleza hapa itabidi nitafutiwe mtaalamu wa ku-defuse malimbwata!huwa nayafanya mengi kwa nafasi yangu, lakini wajameni hivi kweli ni sahihi mama karudi nyumbani saa kumi jioni, fine anatakiwa kupimzika, dada kakaa na watoto na kuhangaikia nyumba tangu asubuhi hawampi hata nafasi ya kupumzika, wa shule wanarudi saa kumi na moja, mama unaamka kumdai dada chai, waliorudi shule nguo zao na maandalizi ya kesho, mama unademand chai ukiwa unakodolea macho luninga yako! Baba anarudi, dada huyu huyu anaacha alichokuwa anakifanya kukimbilia kufungua geti!anakupokea na kukukaribisha, mama bize kwenye luninga, dada bila kuambiwa anamletea baba chai, baada ya chai baba unaingia kwenye kazi za nyumbani na kumuacha mama akiendelea kutazama isidingo, saa mbili unarudi kuangalia taarifa ya habari, mama ...daadaaa vipi hicho chakula bado? unamdai mtoto notebook unakuta kuna msg ya jana toka shuleni, wee jana ulichelewa kazini umewakuta wamelala! ukiuliza mama jibu sijaiona, dada akisikia .....baba samahani niliona jana lakini nilisahau kukuambia, jana mama alikuwepo tangu saa tisa mchana! dozi ya dawa za watoto lazima uhakikishe umemuelekeza dada, hata kama kwa bahati mbaya hukuweza kumpeleka mtoto hosp, alipelekwa na mama kwa shingo upande! ukimwachia mama kama si kumpa kwa muda tofauti basi kampunguzia au kumuoverdose mtoto!!!mama huyu huyu hajui iliko shule wanakosoma wanae, hana hata contact moja ya mwalimu wa mwanae!! jamaaaaaaani baba huyu atashika mangapi!?bado 95% ya matumizi ya nyumbani lazima yatoke kwa baba!
kwa upande wa huyu dada, hivi huwa hawachoki? hawana haki ya kupumzika na kuthaminiwa? ukipropose kumuongezea hivyo vijisenti vyake utasikia ...aaah zinamtosha, kwanza nyingi sana (20,000/= hiyo!!)
Mueleze kwa upendo umuhimu wa yeye kusimama kama mama kwenye nyumba yake. ni kweli wadada wanatakiwa watusaidie tu na sio ytuwaachie majukumu yote, wote baba na mama wawe responsible hapa, nafurahi kwamba unaplay part yako vizuri sana kwama ni kweli unafanya yote haya, endelea wala usikate tamaa, mingine mitihani jamani.
mimi pamoja na kuonekana nina roho mbaya au jeuri au muuaji call me whatever, i make sure my baby is ok once i get home, japo huwa nachelewa kufika home maranyingi huwa nakuta dada keshapika, but i bath my bay we talk for a while and play games, then i make sure chakula kiko mezani on time na kureview siku ilikuwaje home, mnatumizi ambayo huwa nimeyaacha (naandika kabisa, kipikwe nini na kifanyike nini home siku hiyo). weekend mara nyingi nakuwa home, tunasaidiana kufua nguo zetu na DH tunasafisha chumba chetu na mahali pengine ambapo na dhani dada hakufanya navyotaka, tunakaa na mwanetu tunacheza na kutoka out ikibidi. Dada kwangu hana kazi kwa kweli esp kwa kuwa nina familia ndogo. So my hubb n i are very good adninstrotors of the house. Budget kama nilivyokwisha kusema huko nyuma tunachangia, mwezi huu nikiwa stering mimi, mwezi ujao yeye, na pesa zingine tunapanga, tufanye nini kwa ajili ya badae. Kwa ufupi kwa kushirikiana na kujaliana tunaishi kwa raha mustarehe so far. kuna openness ya hali ya juu, unajua kucall a spade a spade and not a big spoon? we are free individual yani kwa ufupi.
So muwekane wazi kama unakwazika then see the progress. all the best and pole.
 
Yeah subili Ndoa yako ichanganye mchokane utaona utaanza kuambiwa ufue nguo uoshe vyombo mm naenda saloon we acha bana

Hayo yote nayafanya hata sasa kwa hiari yangu mwenyewe kuonyesha upendo kwa mamaaa.
 
...mwingine kaka yeye anachojua ni kufanyiwa tu mfano
1. Anaamka asubuhi anakuamsha ukamwekee maji kwenye ndoo (na yanatoka bombani na ni master bedroom)
2. Umwekee dawa ya meno kwenye mswaki (usipoweka ataoga kisha atatoka kuja kuulizia mswaki wake)
3. Anatoka bafuni (hapo unakuta pant yake kaivua kaitupia kwenye sink anasubiri uje uife!)
4. Akitoka ushampigia pasi anavaa, anakunywa chai ulomwekea kisha huyooo funguo za gari zi wapi na akifika ndani ya gari ni honi mtindo mmoja unamchelewesha na usipokimbia na viatu mkononi anakuacha unakwenda ofcn kwa daladala au ukifanikiwa kuingia kwenye gari basi kusemwa mtindo mmoja unamchelewesha teke.

MCHANA KUTWA HATA KUKUPIGIA SIMU YA SALAMU AU SMS YA I MISS YOU!

5. Akirudi jioni akute chai yake mezani na maji bafuni
6. Atizame TV huku akisubiri chakula au asome magazeti yake
7. Akishakula huyooo kitandani analala huku akisubiri wewe uje ushushe neti na kumfunika na shuka!
8. Uingie kitandani baada ya kumaliza kazi zako akudake tayari kwa chakula cha usiku.
The life continues!

Kwa style hii kweli unategemea mkeo atakuwa anamapenzi na wewe? Si atajihisi hana tofauti na huyo housegirl jamani!

Jamani mara moja moja ukinisaidia kushusha net au hata kunipigia na mimi pasi I tell you nitaikumbuka kwa muda mrefu na moyo wangu kukongwa vilivyo!!

...dada'ngu, Mume wa namna hii lazima utakuwa umemharibu mwenye weye mke! khaaa,...eti mfalme wa nyumba, ...puuuuuu!

 
kinachonishangaza zaidi ni wanaume hawa hawa waliopo bongo sasa, wakati walipokuwa viwanja vya watu huko, walikuwa wakifanya mambo telee kusaidia wake/gf zao. leo wameikanyaga tz ndo wamekuwa hawawezi tena!
 
Back
Top Bottom