jamani si akina baba wote ambao hawawajibiki, mbona mie nafanya kazi lkn my wife hafanyi kazi but room kwetu nafanya yafuatayo
1.nafua pants zetu wote mara ya mwisho yeye kufua nadhani ni miezi km 4 imepita
2.usafi wote wa kupiga deki na kufuta vumbi huwa nafanya mie, kusafisha choo na bafu nafanya mie
3. Daily mie ndo natandika kitanda nakubadilisha mashuka
4. Akisuka rasta zake siku akitaka kufumua basi atakuja baba nani hii nifumue nywele huwezi amini room namfumua nywele ni vitu ambavyo nimevizoea
nna moyo sana wa kusaidia na hii imenijenga toka nikiwa home kwetu my late father alipenda sana usafi na alisisitiza sana kuwa msafi room basi ikanijenga nikawa siwezi kumwachia mtu mwingine afanye usafi wa pants zangu na hii ndo imenifanya mpaka leo nione ni kitu cha kawaida sana.
Hii imenifanya niwe karibu sana na mke wangu huwa mpaka najiuliza km wanaume wengine wangekuwa hivi wangefaidi sana mapenzi ya wake zao ingawa wengi wanadhani eti mwanamke atakudharau lkn si hivyo. Hii imefanya tuwe kama marafiki kwa kweli, hakuna kununiana nuniana kwa hovyo, wala visasi visivyo na maana hakuna siri kila atakachofanya ntaambiwa kwanza.