kuna kitu kinachonishangaza kuhususu hizi ndoa za mke zaidi ya mmoja. je wenye wake wengi wameoa hivyo kwasababu ya tamaa? Au wana wasaidia wanawake ambao bado hawajapata mme? Au ni utajiri ndo unawasumbua? naomba jibu
Ngomo,
Mfalme wa Swaziland anaendeleza utamaduni na mila za kwao.
Rais wa Afrika Kusini naye anapenda utamaduni wao.
Ali Mwinyi, Bilali wao ni
ruksa kulingana na mafundisho ya dini yao.
Katika mila za Kiafrika ndoa za wake wengi limekuwa ni mazoea.
Iraq wao wanapendekeza polygamy kama njia ya kuondoa tatizo la vizuka ambao wapo kama milioni moja waliopoteza waume wao kutokana na vita. Pitia hii link
https://www.jamiiforums.com/habari-...105997-ungetoa-ushauri-gani-nini-wafanye.html
Waliokuwa hawaoi wake wengi ,hufuga vimada au huwa na "marafiki" wengi wa kustarehe nao, huenda ni hizo tamaa za ngono au ndio "vijisenti" vinawasumbua.
Hata hivyo, ndoa hizi au kuwa na uhusiano wa kingono na zaidi ya mtu mmoja katika mazingira haya ya maradhi ya kaswende na ukimwi ni mtihani mzito.
Ali mwinyi aliwahi kusema,"ugonjwa umeingia pahali pabaya" Na kweli ugojwa umeingia mahali patamu.... Kama ushakua au ushabaleghe basi unafahamu nini kakusudia!!!!
Remmy aliimba "kifo hakina huruma" lakini utateseka kwanza na jamii ikikujua umeukwaa basi ni kasheshe!