Kupenda ni rahisi, kuishi na mtu ambae sio compatible na wewe ni habari nyingine kabisa.
Kivipi?Nani kakuambia kupenda ni rahisi?Labda uwe hujui kupenda,tafsiri sahihi ya kupenda inapingana na kauli yako!
Upendo unafundishwa kwenye familia,ndoa ni uamuzi sio upendo,ukijua kupenda haitakua kazi kuanzisha familia na YOYOTE kwani unakua umempenda tayari!Umempenda coz kigezo cha kupenda ni huyo awe binadam na sio awe na hela au mrefu au miguu ya bia au mtanashati!
Sasa kama inaweza kuanzia popote kwanini unaona kwamba wanaoanza kwa kupendana wanakosea/ndio sababu ya ndoa kutokudumu?
Mara nyingi kinachofanya mtu afanikiwe sio anapo/anavyoanza bali ni malengo yake na namna anavyojituma kufikia matarajio yake. Zaidi ya hapo hata kama leo hii nikiamua kumchagua mtu randomly na kuoana nae huku nikiwa na malengo yasiyoendana nae au hata hiyo ndoa hatutofika popote. Mbaya zaidi ikitokea nikawa na matarajio ambayo sipo tayari kufanya kazi ili niyafikie, sitofikia na hivyo kunifanya mimi nione nilikosea step katika kumchagua mhusika even though tatizo lipo kwangu na sio kwake.
Pamoja na kukosa hofu ya Mungu, bado kuna sababu nyingine.
Nikupe mfano, huko nitokako mwanamke alikuwa anatafutiwa mume wala asiye mjua. Kunq upendo hapo? Utampendaje mtu usiyemjua unamwona siku ya ndoa?
Tena kuna wakati unaletewa kibabu, unalazimisha kuolewa kwa kupigwa lakini bado ndoa zilikuwa zinadumu.
Ukisema hofu ya Mungu, sidhani maana hizi dini ni tamaduni mpya. Lakini bado babu zetu wamekaana wake zao hadi vifo vilipowatenganisha wakati hawakuwa wanajua kanisa lolote zaidi ya matambiko ya jadi.
Mi naona ni mwingiliano wa tamaduni zaidi katika nyanja zote.
ndoa za zamani walikuwa hawafahamiani wala kujuana lakini walijifunza kupendana na waliweza kuhimili lolote katika ndoa kwa uvumilivu na upendo wa dhati....za sasa imekuwa kama fasheni mtu anaolewa kuondoa aibu kwenye familia...unaweza kuta msichana anampenda mvulana lakini mvulana sio sana inabidi kuoa kwa huruma fulani vivyo hivyo kwa mvulana anapenda sana bi dada anakubali kwa vile asionekana mbaya au baada kukosa wa kumwoa.... pia wengine wanaoana umri unakwenda bora lolote au jamaa maisha yanalipa. kwa jumla maisha ya ndoa za sasa yanaangalia vitu na sio upendo wa dhati
Sasa mkwe kama zamani kupendana kulikua kunakuja baadae huo upendo wa dhati walikua wanaangalia vipi kabla ya kukubali/amua kuoana?
Faiza unaweza usieleweke hapa!Hebu fafanua kuoa ni nini,kuoelewa ni nini na kuoana ni nini,utakua umetoa msaada,naweza kuwa nimekuelewa lakini eleza zaidi!
mkwe nilikwenda kwa rafiki yangu mamake akawa anaelezea wakati wa kuolewa kwake ilivyokuwa naomba ninukuu '' nilikuwa simjui wala sikuwa kumwona na ndoa ilifungwa kwa sababu waliambia na wazazi na ni lazima walikubali na hata walipotoka kanisani baada ya ndoa alikimbia kujificha lakini baadae wakaishi na upendo ukawepo na hata nilipokuwa na kwenda pale walikuwa wanapendana sana huwezi tegemea kupata story hiyo katika upendo huo. nafikiri baada ya ndoa waliyakubali yote kwa upendo bila kuangalia chochote kitu akajifunza kumpenda kumthamini nakuona anatakiwa kufanya yale yanayotakiwa kama mke/mume
Basi tukubaliane kwamba tatizo sio watu kutaka kupendana kwanza bali ni yale yanayowasukuma kuamini wanapendana. Kwasababu mabadiliko yanapotokea (vigezo vyao vya kupenda vinapokuwa tofauti na mategemeo yao) ndipo matatizo huanza. Hivyo mimi ntabaki kua mmoja wa wanaoamini kuingia ndoani kwakua nampenda mwenzangu nae ananipenda ndio njia sahihi kwangu na sio kukubali tu ndoa huku nikitumaini tutapendana huko mbeleni.Hapana Lizzy,
On the contrary, kama watu wanaweza kuanza kwa kupendana basi naamini kuna uwezekano mkubwa kwamba ndoa yao itadumu.
Tatizo langu ni vijana wa siku hizi kuweka over-emphasis kwenye hiyo kitu inaitwa love before marriage wakati hata love yenyewe ama hawaielewi vizuri au kila mtu na version yake kichwani!!
Women rights - women's rights.
Vijana wa siku hizi hawawezi kuelewa hii concept hata ukitumia Majeshi yote ya ulinzi na usalama!!
Basi tukubaliane kwamba tatizo sio watu kutaka kupendana kwanza bali ni yale yanayowasukuma kuamini wanapendana. Kwasababu mabadiliko yanapotokea (vigezo vyao vya kupenda vinapokuwa tofauti na mategemeo yao) ndipo matatizo huanza. Hivyo mimi ntabaki kua mmoja wa wanaoamini kuingia ndoani kwakua nampenda mwenzangu nae ananipenda ndio njia sahihi kwangu na sio kukubali tu ndoa huku nikitumaini tutapendana huko mbeleni.
mkwe nilikwenda kwa rafiki yangu mamake akawa anaelezea wakati wa kuolewa kwake ilivyokuwa naomba ninukuu '' nilikuwa simjui wala sikuwa kumwona na ndoa ilifungwa kwa sababu waliambia na wazazi na ni lazima walikubali na hata walipotoka kanisani baada ya ndoa alikimbia kujificha lakini baadae wakaishi na upendo ukawepo na hata nilipokuwa na kwenda pale walikuwa wanapendana sana huwezi tegemea kupata story hiyo katika upendo huo. nafikiri baada ya ndoa waliyakubali yote kwa upendo bila kuangalia chochote kitu akajifunza kumpenda kumthamini nakuona anatakiwa kufanya yale yanayotakiwa kama mke/mume
Babu DC
nilikuwa napenda kumsikiliza sana yule bibi, ni marehemu sasa
yaani unaweza jiuliza mapenzi haya tunayojidai kwamba
namfahamu/tunayafahamu sana oooohhh nampenda kutoka rohoni
inakuwaje hayadumu hata kwa miezi 3
migogoro kila kona mmmmmhhh
kweli ni kitendawili au ndio ujuaji umetawala
Kwahiyo babu wewe hisia zako kwa bibi DC zikoje?Hakuna neno Lizzy,
Mie ni miongoni mwa wale ambao hadi sasa sina hakika kama nafahamu maana ya hicho kitu mnaita kupenda. Kwa vile tunasonga mbele, naamini kwamba ama nafanya vizuri au mwenzangu keshanizoea na kukubali mapungufu yangu!!
Tuendelee kupeana shule!!
Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.
Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.