NDOA: Zamani vs Siku hizi

NDOA: Zamani vs Siku hizi

Kupenda ni rahisi, kuishi na mtu ambae sio compatible na wewe ni habari nyingine kabisa.

Kivipi?Nani kakuambia kupenda ni rahisi?Labda uwe hujui kupenda,tafsiri sahihi ya kupenda inapingana na kauli yako!
 
umenikumbusha poem flani inakwenda kwa title "Young Love, Ignorant of Reality " mi nadhani Ndoa za zamani "Arranged Marriage" ndio ilikuwa sababu kubwa zinafanya zidumu kuliko hizi za sikuhizi..! wajuwa "penzi ni upofu ama kitovu cha uzembe" utakuta mtu atoka na m.mme/m.mke ambaye hajulikani kwa yeyote watu walio karibu naye anakuja kutambulisha huyu ndio my soul mate ..! kah! mi bado sijaoa lakini nadhani chanzo kikubwa cha kutodumu kwa ndoa za sikuhizi ni kuoa/kuolewa na watu wasiofahamika na jamii inayokuzunguuka kwa kisingizio cha "TUMEPENDANA"
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kivipi?Nani kakuambia kupenda ni rahisi?Labda uwe hujui kupenda,tafsiri sahihi ya kupenda inapingana na kauli yako!

Kama ni wewe uliyeandika haya yanayofuata nadhani itakua vizuri ukiacha kupinga alimradi umempinga fulani maana hatuko hapa kushindana bali tupo kujadiliana.

Upendo unafundishwa kwenye familia,ndoa ni uamuzi sio upendo,ukijua kupenda haitakua kazi kuanzisha familia na YOYOTE kwani unakua umempenda tayari!Umempenda coz kigezo cha kupenda ni huyo awe binadam na sio awe na hela au mrefu au miguu ya bia au mtanashati!

Kujibu swali lako, sijaambiwa na mtu.
Najua kwasababu naweza kupenda watu bila kujali wanavyoishi, waliyonayo na wasiyonayo.
 
Sasa kama inaweza kuanzia popote kwanini unaona kwamba wanaoanza kwa kupendana wanakosea/ndio sababu ya ndoa kutokudumu?

Mara nyingi kinachofanya mtu afanikiwe sio anapo/anavyoanza bali ni malengo yake na namna anavyojituma kufikia matarajio yake. Zaidi ya hapo hata kama leo hii nikiamua kumchagua mtu randomly na kuoana nae huku nikiwa na malengo yasiyoendana nae au hata hiyo ndoa hatutofika popote. Mbaya zaidi ikitokea nikawa na matarajio ambayo sipo tayari kufanya kazi ili niyafikie, sitofikia na hivyo kunifanya mimi nione nilikosea step katika kumchagua mhusika even though tatizo lipo kwangu na sio kwake.

Hapana Lizzy,

On the contrary, kama watu wanaweza kuanza kwa kupendana basi naamini kuna uwezekano mkubwa kwamba ndoa yao itadumu.

Tatizo langu ni vijana wa siku hizi kuweka over-emphasis kwenye hiyo kitu inaitwa love before marriage wakati hata love yenyewe ama hawaielewi vizuri au kila mtu na version yake kichwani!!
 
Mabadiliko niliyozungumzia Mbu ni mengi, ila moja wapo ambalo nimeona kama limekuwa sugu sana kwa wanandoa ni hili litokanalo na kuingia kwa wanawake katika soko la ajira. Hili limekuwa tatizo sugu kwa kuwa pamoja na kuwa ni jambo zuri hasa katika dhana ya women empowernment and development bado limetuletea dhahma katika taasis ya ndoa. Mabadiliko haya hayajaenda sambamba na mabadiliko yetu ya kimaadili na kitamaduni.
Kwa wanawake: Wengi tumeyapokea mabadiliko haya kivyengine yaani si kama ilivyodhamiriwa. Kuwa kwetu na uwezo au opportunities za kupata ajira na kuajiriwa, kushiriki kajika soko la ajira katika hali na ushindani sawa (na wengine wakiuza utu wao) na wanaume vimetufanya tuwe na ile hali ya kiburi na ile hali ya 'hata mie ninao uwezo, kama wewe'. Ninaposema kuwa mabadiliko haya hayajaenda sambamba na mabadiliko yetu kimaadili na kitamaduni nina maanisha kuwa pamoja na uwezo huu, bado wapo wanawake ambao wamekumbatia dhana za "Wewe ndie Baba wa familia, ni jukumu lako kuhakikisha familia inaprosper na si mimi; chako ni chetu na changu ni changu, wewe ni kichwa cha familia, utajiju n.k huku kipato chake mama kikiwa ni marufuku kutumika kwenye family matters hata kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.
 
Pamoja na kukosa hofu ya Mungu, bado kuna sababu nyingine.

Nikupe mfano, huko nitokako mwanamke alikuwa anatafutiwa mume wala asiye mjua. Kunq upendo hapo? Utampendaje mtu usiyemjua unamwona siku ya ndoa?

Tena kuna wakati unaletewa kibabu, unalazimisha kuolewa kwa kupigwa lakini bado ndoa zilikuwa zinadumu.

Ukisema hofu ya Mungu, sidhani maana hizi dini ni tamaduni mpya. Lakini bado babu zetu wamekaana wake zao hadi vifo vilipowatenganisha wakati hawakuwa wanajua kanisa lolote zaidi ya matambiko ya jadi.

Mi naona ni mwingiliano wa tamaduni zaidi katika nyanja zote.

ndio maana nikasema watu hawana hofu ya mungu na wala hawafati mila na desturi zao maana najua wapo ambao hawaamini habari za mungu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
ndoa za zamani walikuwa hawafahamiani wala kujuana lakini walijifunza kupendana na waliweza kuhimili lolote katika ndoa kwa uvumilivu na upendo wa dhati....za sasa imekuwa kama fasheni mtu anaolewa kuondoa aibu kwenye familia...unaweza kuta msichana anampenda mvulana lakini mvulana sio sana inabidi kuoa kwa huruma fulani vivyo hivyo kwa mvulana anapenda sana bi dada anakubali kwa vile asionekana mbaya au baada kukosa wa kumwoa.... pia wengine wanaoana umri unakwenda bora lolote au jamaa maisha yanalipa. kwa jumla maisha ya ndoa za sasa yanaangalia vitu na sio upendo wa dhati

Dada aksante.
 
Sasa mkwe kama zamani kupendana kulikua kunakuja baadae huo upendo wa dhati walikua wanaangalia vipi kabla ya kukubali/amua kuoana?

mkwe nilikwenda kwa rafiki yangu mamake akawa anaelezea wakati wa kuolewa kwake ilivyokuwa naomba ninukuu '' nilikuwa simjui wala sikuwa kumwona na ndoa ilifungwa kwa sababu waliambia na wazazi na ni lazima walikubali na hata walipotoka kanisani baada ya ndoa alikimbia kujificha lakini baadae wakaishi na upendo ukawepo na hata nilipokuwa na kwenda pale walikuwa wanapendana sana huwezi tegemea kupata story hiyo katika upendo huo. nafikiri baada ya ndoa waliyakubali yote kwa upendo bila kuangalia chochote kitu akajifunza kumpenda kumthamini nakuona anatakiwa kufanya yale yanayotakiwa kama mke/mume
 
Faiza unaweza usieleweke hapa!Hebu fafanua kuoa ni nini,kuoelewa ni nini na kuoana ni nini,utakua umetoa msaada,naweza kuwa nimekuelewa lakini eleza zaidi!

Nimejaribu kuelezea katika post #7, naomba ipitie tena na kama hujanielewa nifahamishe, ntajaribu kuelezea tena kivingine.
 
mkwe nilikwenda kwa rafiki yangu mamake akawa anaelezea wakati wa kuolewa kwake ilivyokuwa naomba ninukuu '' nilikuwa simjui wala sikuwa kumwona na ndoa ilifungwa kwa sababu waliambia na wazazi na ni lazima walikubali na hata walipotoka kanisani baada ya ndoa alikimbia kujificha lakini baadae wakaishi na upendo ukawepo na hata nilipokuwa na kwenda pale walikuwa wanapendana sana huwezi tegemea kupata story hiyo katika upendo huo. nafikiri baada ya ndoa waliyakubali yote kwa upendo bila kuangalia chochote kitu akajifunza kumpenda kumthamini nakuona anatakiwa kufanya yale yanayotakiwa kama mke/mume

Vijana wa siku hizi hawawezi kuelewa hii concept hata ukitumia Majeshi yote ya ulinzi na usalama!!
 
Hapana Lizzy,

On the contrary, kama watu wanaweza kuanza kwa kupendana basi naamini kuna uwezekano mkubwa kwamba ndoa yao itadumu.

Tatizo langu ni vijana wa siku hizi kuweka over-emphasis kwenye hiyo kitu inaitwa love before marriage wakati hata love yenyewe ama hawaielewi vizuri au kila mtu na version yake kichwani!!
Basi tukubaliane kwamba tatizo sio watu kutaka kupendana kwanza bali ni yale yanayowasukuma kuamini wanapendana. Kwasababu mabadiliko yanapotokea (vigezo vyao vya kupenda vinapokuwa tofauti na mategemeo yao) ndipo matatizo huanza. Hivyo mimi ntabaki kua mmoja wa wanaoamini kuingia ndoani kwakua nampenda mwenzangu nae ananipenda ndio njia sahihi kwangu na sio kukubali tu ndoa huku nikitumaini tutapendana huko mbeleni.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Lakini wapo pia wanawake walioyapokea mabadiliko haya kwa kuchukua nafasi za waume zao kwa kutowashirikisha katika maamuzi makubwa ya kifamilia just because wanamudu gharama. Mf. kununua assets kama viwanja, magari na kisha kuvitumia au kuvimiliki katika hali ya "Umimi" wakisahau kuwa when you get married, you leave I for Us (Source: Taylor Perry: Why Did I get Married Part 1).
Na mwisho wapo wengine walioyapokea haya katika hali ya Ulimbukeni kama wamepata bwana mpya. Kapata kazi, kapanda cheo kidogo, haoni faida ya kuwa na mume. Anatafuta sababu anadai kuachana.

Kwa wanaume: Wapo walioyapokea haya mabadiliko kwa hali ya kuyakana kisilence. Kuwa mshahara wa mkewe haumhusu na yeye kama kichwa cha familia anakufa na tai shingoni ili afulfill mahitaji ya familia. Mshahara wa mkewe hauhoji, na hata mke akuvoluntier yeye kama kashikwa sana atapokea but atarudisha akipata. Matokeo yake mke anajifunza kujizoesha kuspend mshahara wake the way apendavyo, saluni, vikuku na vishaufu. Sasa shughuli ni pale Mr maji yanapofika shingoni, ndipo anaanza kuwa na gubu kwa mkewe na kususiana kwa mtindo wa ..................Hivi kwani wewe mshahara wako una kazi gani, unahonga n.k. Sasa jiulize ulishamzoesha mwenyewe kuwa pesa yake ni yake sasa unaihitaji isaidie familia unashindwa pa kuanzia unaanza kwa gubu, mke hatoelewa bila kumwelewesha. Mnaanza kulumbana.

Wapo wale waliopokea mabadiliko haya kwa staili ya take advantage of the situation. Ilmradi mama nawe mwisho wa mwezi unakinga mkono, anakuachia majulkumu yote mpaka yale yaliyotakiwa kuwa yake ayabebe mama/mke. Anageuka mwanaume ambaye mshahara wake haujulikani uendako na nahitaji yote ya familia ni mama anayacover. Anakuwa mume anayelelewa.

Mwe!
 
MJ1,

Nimesema awali kabisa kwamba tuko kwenye kipindi cha mpito na kwa hiyo kuna confusion katika uendeshaji wa maisha yetu ya ndoa katika mazingira mapya. Mbaya zaidi kuna ombwe la social system (unlike in the past) ambayo ingetusaidia kuendesha ndoa zetu. Hata wale ambao ndoa zimevuta vuta kidogo, hawana uhakika wa kesho itakuwaje na hawawezi kueleza kwa ufasaha kitu gani kimewafikisha hapo. Bado ni mchezo wa pata potea.

Ngoja kwanza nipate dinner...nitarudi baadaye kidogo!!
 
Women rights - women's rights.

Hapo ndipo unapokosea siku zote. Hii ni kama ile ya kuleeee, unakumbuka? na hilo lako kosa la wengi sana si wewe tu, lakini nani wa kuwakosoa? kumbuka women rights, ni haki zinazowahusu wanawake ambazo bado hazijawa zao na women's rights ni tayari haki zao. (kabukuwe tena kuhusu "possessive tense"). Sikisii.
 
Vijana wa siku hizi hawawezi kuelewa hii concept hata ukitumia Majeshi yote ya ulinzi na usalama!!

Babu DC
nilikuwa napenda kumsikiliza sana yule bibi, ni marehemu sasa
yaani unaweza jiuliza mapenzi haya tunayojidai kwamba
namfahamu/tunayafahamu sana oooohhh nampenda kutoka rohoni
inakuwaje hayadumu hata kwa miezi 3
migogoro kila kona mmmmmhhh
kweli ni kitendawili au ndio ujuaji umetawala
 
Basi tukubaliane kwamba tatizo sio watu kutaka kupendana kwanza bali ni yale yanayowasukuma kuamini wanapendana. Kwasababu mabadiliko yanapotokea (vigezo vyao vya kupenda vinapokuwa tofauti na mategemeo yao) ndipo matatizo huanza. Hivyo mimi ntabaki kua mmoja wa wanaoamini kuingia ndoani kwakua nampenda mwenzangu nae ananipenda ndio njia sahihi kwangu na sio kukubali tu ndoa huku nikitumaini tutapendana huko mbeleni.

Hakuna neno Lizzy,

Mie ni miongoni mwa wale ambao hadi sasa sina hakika kama nafahamu maana ya hicho kitu mnaita kupenda. Kwa vile tunasonga mbele, naamini kwamba ama nafanya vizuri au mwenzangu keshanizoea na kukubali mapungufu yangu!!

Tuendelee kupeana shule!!
 
mkwe nilikwenda kwa rafiki yangu mamake akawa anaelezea wakati wa kuolewa kwake ilivyokuwa naomba ninukuu '' nilikuwa simjui wala sikuwa kumwona na ndoa ilifungwa kwa sababu waliambia na wazazi na ni lazima walikubali na hata walipotoka kanisani baada ya ndoa alikimbia kujificha lakini baadae wakaishi na upendo ukawepo na hata nilipokuwa na kwenda pale walikuwa wanapendana sana huwezi tegemea kupata story hiyo katika upendo huo. nafikiri baada ya ndoa waliyakubali yote kwa upendo bila kuangalia chochote kitu akajifunza kumpenda kumthamini nakuona anatakiwa kufanya yale yanayotakiwa kama mke/mume

Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.

Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.
 
Babu DC
nilikuwa napenda kumsikiliza sana yule bibi, ni marehemu sasa
yaani unaweza jiuliza mapenzi haya tunayojidai kwamba
namfahamu/tunayafahamu sana oooohhh nampenda kutoka rohoni
inakuwaje hayadumu hata kwa miezi 3
migogoro kila kona mmmmmhhh
kweli ni kitendawili au ndio ujuaji umetawala

Nakuhakikishia kuwa wengi wao ukiwauliza kwa nini wanadai wanawapenda hao wapenzi wao utashangaa majibu watakayokupa!!

Unaweza kusikia vitu kama...unajua ni mzuri sana kiasi kwamba siwezi kupata msichana mzuri kama yeye (utadhani anatafuta uzuri wa kula na kushiba). Au msichana anakwambia kuwa....yaani ananipenda sana, ananipigia kila baada ya saa 2 na kila ninachomwomba ananitimizia.....Too childish..

Nadhani tuko kwenye kipndi kigumu sana tena ukizingatia bado kuna blending ya kizazi cha kijijini na kile cha egoli egoli wa mijini!!
 
Hakuna neno Lizzy,

Mie ni miongoni mwa wale ambao hadi sasa sina hakika kama nafahamu maana ya hicho kitu mnaita kupenda. Kwa vile tunasonga mbele, naamini kwamba ama nafanya vizuri au mwenzangu keshanizoea na kukubali mapungufu yangu!!

Tuendelee kupeana shule!!
Kwahiyo babu wewe hisia zako kwa bibi DC zikoje?
Mnaishi kwasababu umemzoea au kwasababu unampenda?
 
Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.

Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.

Hapo nakubaliana na wewe,

1. Watu wengi hawailewi vizuri concept ya ndoa. Wanafanya kuingia kichwa kichwa!
2. Ubinafsi umezidi sana......wanandoa wanataka kuwa kwenye ndoa na hapo hapo wabaki kama watu huru....Katika matumizi ya vitu (meterials) na mambo mengine yanayohusu maisha!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom