Ahsante mkwe, nimekupata. Mpaka hapo mimi nimeelewa kwamba tatizo halipo kwenye kupenda kwanza ama kuoana kwanza bali ni kwenye utayari wa watu kukabiliana na ndoa, majukumu yake na changamoto zake.
Kwa maana hiyo hata kizazi cha leo tukiachana ile dhana ya "nilimuoa akiwa mrembo na sasa amechuja. . . niliolewa nae akiwa na kazi inayomlipa vizuri na sasa hanayo. . .nilimuoa ili nisifiwe mjini na sasa sifa zimeisha " hivyo hanifai tena tutafika mbali. Uzuri wa wazee wetu ni kwamba hawakuchaguana kwa sura, mali na mengine kama hayo.Walichaguana ili wasaidiane though tunaweza kudhani kizazi cha leo ndio kinachosaidiana zaidi ila ukweli ni kwamba kizazi cha leo kimetawaliwa na ubinafsi zaidi. Mtu anaingia kwenye ndoa kwaajili yake tu, kwa mahitaji na matakwa yake tu.Namna anayoishi haimhusu mwenzi wake, hivyo hata akitoka nje (cheat) au akitaka kuachana hamfikirii mwenzake bali anajifikiria mwenyewe.