NDOA: Zamani vs Siku hizi


....kwahiyo tunakubaliana ili ndoa zidumu inabidi kurudisha na kuzisimamia mila, desturi na tamaduni zetu za asili
(mwj1 jana alinikumbusha jando baada ya mie kusisitizia unyago) ....tuwakataze mabinti zetu haya ma kitchen party ya khanga moja sijui laki si pesa....,

...vile vile tuvikumbatie vifuani mwetu vitabu vyenye miongozo ya kiimani badala ya waraka wa Beijing ambao haujatafsirika vyema kwenye jamii yetu, ama?
 
Kuna wanawake wengine hata ufanyaje yeye ni mtu wa kukulaumu tu kana utimizi majukumu yako nyumbani, na anataka wewe ufanane na nyani ngabu kisa nyani ngabu ni mbeba mabox maarufu basi anataka na wewe uwe na ujiko huo!

Awali ya yote, majina yangu yanaandikwa kwa kutumia herufi kubwa kwa herufi ya kwanza - kama hivi Nyani Ngabu.

Na mimi si mbeba mabox maarufu. Mimi ni Raisi wa Wabeba Mabox. Usisahau hiyo, ni Raisi. Okay my friend?
 

Matola ongezea wale ambao kaugomvi kadogo ukoo na mashoga zake wote watajua.

Mapungufu ya mume/mkewe kila mtu anayafahamu.

Tatizo ni kwamba watu hawaoani kwaajili yao bali wanaoana kwaajili ya familia na jamii.Hivyo inakua ngumu kujitoa mazima. Matokeo yote vijitatizo vyote vidogo vidogo lazima vifike kwa mama na baba, maamuzi yote amabyo yanatakiwa yawe kati ya mune na mke lazima yapitie kwa wazazi ama waangalie jamii inaoneje. Hao wanaojali jamii ndo hao wanaotaka ferrari ili wasifike mjini wakati bado wanaishi kwenye nyumba ya kupanga.
 
Awali ya yote, majina yangu yanaandikwa kwa kutumia herufi kubwa kwa herufi ya kwanza - kama hivi Nyani Ngabu.

Na mimi si mbeba mabox maarufu. Mimi ni Raisi wa Wabeba Mabox. Usisahau hiyo, ni Raisi. Okay my friend?
Okey, Nyani Ngabu Rais wa Wabeba Mabox, i hope waziri Mkuu atakuwa MM Mwanakijiji
 
Mbu kuna mtu anapigwa kwa kuwa kachelewa kuipokea simu yake hata kama sababu ilikuwa ni kumuattend mtoto!!!

...lol....sasa haya ndiyo aliyoyasema AshaDii, mambo ya utandawazi nayo yanaathari kubwa kwenye ndoa za kisasa, ...mobile phones, emails, facebook, sms nk nk....yaani imekuwa ni kasheshe juu ya kasheshe lakini ipo njia kuyakabili haya iwapo mwenzako hapendi, au?

...kuna haja gani kumuonyesha mumeo umefanikiwa kuwa add ex boyfriends wako wote kwenye facebook? au sms zisizotulia usiku kucha ...muda ambao ulitakiwa kuwa na mumeo kwenye udugu wa shuka? haya ndio ninayoyasema kama kwenye issue ya makaburini huyo anayejitia 'samaritan' na kuja kumsuta mwanaume mwenziwe jamiiforums...unaona sasa?



...hiyo sasa nayo hila weye, iweje umjazie chumvi mumeo bana? utamuua....!
au ati umeacha kumtilia chumvi kwenye mboga, lazima uchapwe kidogo, kofi lisiloumiza....lol
 

Kwanza Mbu tusilaumu teknolojia pekee, kama asingepigwa kwa kuchelewa kupokea simu angepigwa kwa kuchelewa kufungua mlango au kuleta maji ya kunywa.Mtu mwenye visa haihitaji sababu, yeye chochote kwake anaona kinastahili kichapo.

Hahahahaha, sasa jamani bahati mbaya siinatokea wakati mwingine?Ukizingatia na jinsi wamama wengine wanavyokua na mambo mengi ya kufanya, wala mimi sioni ajabu. Ila angalau wewe umesema shurti achapwe kofi lisilouma, wenzako wanapiga mpaka kesho yake mama akiinua kujiko aweke sukari kwenye chai mkono unatetemeka.
 
Hii mada imenivutia na nimesoma michango ya wote. Wote kwa njia moja au nyengine tunakubaliana kuwa mmomonyoko wa maadili, kutofuata mila na desturi zetu, kung'ang'ania haki na kusahau/kuepuka wajibu...pamoja na sababu nyingi tu, zinazofanya ndoa za kisasa kutodumu (kwa muda mrefu).

Kama angalizo tu, ningependa kwanza kukumbushia kuwa hata zamani zilikuwepo ndoa zilizoshindikana (jamaa yangu wa karibu aliwahi kuolewa mara 16, mara 3 aliolewa na mume huyo huyo). Pia wapo wanaume waliooa mara zisizo hesabu. Tafauti ya zamani sasa, ni kuwa zamani kesi za kuvunjika kwa ndoa zilikuwa zinahesabika, wakati sasa ndoa zinazodumu ndio zinazohesabika.

Kwa kuongezea kidogo katika mengi yaliyokwishasemwa, nitagusia nukta mbili:

1.- Kujuana saaana kabla ya ndoa" kunachangia. Hii inatafautiana na wazazi wetu waliokuwa wanaoa/wanaolewa/wanaoana hata bila ya kujuana. Nimeweka kwenye vifungo "kujuana sana" kwa sababu hivyo ndivyo tunavyojidai, eti kwa sababu tu wamelala kitanda kimoja miaka mingi kabla ya kuoana. Katika kipindiki hiki cha kubanjuana, kila mmoja huwa anaficha makucha yake na baada ya ndoa yanafichuka yale yote yaliyokuwa yamefichika.

2.- Wakati zamani kuacha/kuachika kulikuwa aibu na mjane alikuwa anaonekana vibaya katika jamii, leo mtu kujidai ni mjane imekuwa fesheni. Tumekutana na wangapi wanawake kwa wanaaume ambao wamo katika ndoa lakini wakitoka tu nje ya nyumba zao wanavua pete na/au kujitangaza ni wajane? Tumefikia mahali kujitaja kuwa umeoa/umeolewa tunaogopa kuoneka wa "zamani". Nina wasiwasi watu wa aina hiyo hata humu JF wamo. Na kama anecdote tu, nimeona majuu watu wanaandaa sherehe za kuacha/ kuwachwa. Sijui lini na hili nalo litafika kwetu, ikiwa bado halipo.

Kwa kuchangia tu mawazo kuhusu nini tufanye ili ndoa za vizazi vijavyo zidumu, nahisi njia pekee ni sisi tulioko ndani ya ndoa sasa kuzidumisha ndoa zetu na kuwa mfano mwema kwa vizazi vyetu, vyenginevyo hata tukaweka mitaala na silibasi mashuleni, ikiwa tunawafunza kile ambacho sisi tulishindwa kukitekeleza, wao hawataweza.
 
Reactions: Mbu

Mkuu Mbu mimi kwa maoni yangu mporomoko wa NDOA ZA KISASA unachangiwa na haya yafuatayo:

ELIMU:

Wanawake wa siku hizi wengi wamesoma sana ukilinganisha na wale wa miaka ile ambao asilimia kubwa walikuwa wameishia madarasa ya chini sana au hawakusoma kabisa. Elimu hii waliyoipata hawa wanawake katika ndoa za kisasa imewasaidia kwanza kujua haki zao ndani ya ndoa na pia kujua nini watakacho ndani ya ndoa. Si rahisi hawa kuwaburuza kama gari bovu kama walivyokuwa wanafanyiwa Wanawake katika ndoa za enzi zile ambao walikuwa wanayavumilia mengi sana ndani ya ndoa ili mradi watunze ndoa zao. Hawa wa kisasa wana kisomo cha hali ya juu, kazi nzuri na kipato kikubwa ambacho kinawawezesha kabisa kuishi wenyewe bila matatizo na hivyo kutohitaji kumtegemea mume katika mahitaji yao muhimu ikiwemo makazi, chakula n.k. Kwa maoni yangu si kweli hawa wana dharau au kiburi kama ambavyo Wanaume wengi tunavyodhani bali tu wanahitaji kuheshimiwa kama wake, kuonyeshwa mapenzi ya kweli, na kuthaminiwa kwa mchango wao ndani ya ndoa. Kunapotokea tatizo katika ndoa ambazo Wanawake wake ni wasomi mara nyingi hitimisho la Wanaume ni kwamba huyu ana kiburi kwa sababu kasoma, kwa sababu ana kazi nzuri na mshahara mzuri vitu ambavyo mara nyingi havina ukweli wowote. Unaweza kukuta tatizo dogo sana likawa kubwa kupita kiasi kwa dhana potofu kabisa na hata kuvunja ndoa.

Kuwashirikisha watu wa nje katika matatizo ya ndani ya ndoa:

Hapa ninamaanisha marafiki, mashoga, colleagues n.k. Zamani matatizo ya ndani ya ndoa yalikuwa yanajulikana kwa wanafamilia tena wale wa karibu sana. Hawa tatizo lilipotokea na wao kufahamishwa walijitahidi kwa hali na mali ili kuyamaliza matatizo katika ndoa husika na wakati mwingine hata majirani wasijue kwamba Mr & Mrs A walikuwa na matatizo makubwa katika ndoa yao. Siku hizi si hivyo kabisa mume/mke akiwa na matatizo basi watu wote anaowafahamu wakiwemo marafiki, majirani, colleagues, wasusi/vinyozi kule saloon atawaelezea matatizo katika ndoa yake. Hawa wengi wao huwa haiwatakii mema ndoa husika. Na wengine si ajabu wataweka matatizo hayo mtandaoni (hapa JF tumeshaona mifano chungu nzima siku za nyuma). Haya matatizo kujulikana na watu wengi kiasi hicho tena wengine wanasubiri kwa hamu kuona ndoa inasambaratika hayasaidii kwa kweli katika kudumisha ndoa. Wengine walioombwa ushauri wa nini mume/mke afanye kufuatia tatizo lilitokea ndani ya ndoa mfano mke/mume kutembea nje bila hata ya kufikiria athari kubwa sana labda kwa watoto katika ndoa ile hutoa ushauri, "Achana naye, wanawake/wanaume wa maana wako chungu nzima siku hizi." badala ya kujaribu kuwasaidia wana ndoa wale wamalize matatizo yao bila kuisambatarisha ndoa yao.

Utandawazi:

Miaka ya nyuma ilikuwa humtongozi mwanamke mpaka umemuona akakuvutia labda kwa sura yake, tabasamu lake, miguu yake, miondoko yake (kama Naomi Campbell au Tyra Banks 🙂🙂) wowowo lake n.k. Sasa hili lilihitaji muda kwa kweli ili uweze kumfuatilia binti huyo mpaka uweze kukubaliwa kama mpenzi, lakini siku hizi ni tofauti kabisa. Unaweza ukamtongoza binti yeye yuko bara tofauti na ulilopo wewe kupitia mtandao na huku hujawahi hata kumtia machoni. Na ikitokea akakubali basi mnaweza kujenga penzi la nguvu sana tena la kweli kabisa.

Pia mtandao na hata TV zimechangia kuwafanya wanandoa wasiwe karibu karibu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Miaka hii utakuta nyumba nyingi zina TV mbili mbili mama anaangalia vipindi vyake na baba anaangalia vipindi vyake kila mmoja hapendi vipindi vya mwenzake. Pia utakuta kila mtu ana laptop yake mume yuko JF kwenye siasa na mke yuko MMU 🙂🙂 hawa hawapati muda kabisa wa kukaa kama mume na mke na kama wote ni waajiriwa basi hali ndio inazidi kuwa mbaya sana katika ndoa yao hata linapotokea tatizo dogo sana basi kwao huwa ni kubwa sana kwa sababu kwanza hawajuani kila mtu yupo kivyake vyake tu (MBL Married but lonely, MBA Married but available & MBU Married but unsatisfied) hahahahaha lol! watu kama hawa pamoja na kuwa wamo kwenye ndoa lakini hawajuani kabisa hivyo ni rahisi mno kufikia maamuzi ya kuachana kwa sababu hawana uchungu wowote na ile ndoa yao maana wanaishi kama strangers tu wanalala kitanda kimoja lakini ukiondoa kulala pamoja kila mtu yuko kivyakevyake. Tatizo dogo tu ndani ya ndoa basi mume/mke hata kabla ya kukaa chini kuongea na mwenzie kishakimbilia kwa marafiki kuelezea kilichotokea au kishaandika MMU 🙂🙂 kuomba ushauri bila hata ya ndugu wa karibu kwa wanandoa hao kutaarifiwa chochote kile kuhusiana na tatizo husika.

Nadhani kwa maoni yangu mambo haya yanachangia sana katika mporomoko mkubwa uliopo katika ndoa za kisasa ukilinganisha na zile za enzi zile na sidhani kama kuna uwezekano wa kurekebisha hali hii.




 

...kwa kiwango kikubwa nimecheka sana na mchango wako kwenye thread hii, mengi uliyoyaelezea ni kweli tupu na uniruhusu ku quote haya ambayo nitaendelea kuyatumia mara nyingi maishani mwangu;


....
zamani kesi za kuvunjika kwa ndoa zilikuwa zinahesabika, wakati sasa ndoa zinazodumu ndio zinazohesabika.
Tumefikia mahali kujitaja kuwa umeoa/umeolewa tunaogopa kuoneka wa "zamani"
....classic!

...ila hilo la huyo aliyeolewa mara kumi na tano dahh?, miongoni mwa hizo kaolewa mara tatu na mume huyo huyo? ...anafaa kungizwa kwenye Guiness Book of Records...
 


hahahahahahahahaha!....kaka asante sana kwa mchango wako japo hilo dongo hapo juu duuhhh!?
soulmate wangu akilisoma naomba asikuelewe...hehehe
 
Reactions: BAK


hahahahahahahahaha!....kaka asante sana kwa mchango wako japo hilo dongo hapo juu duuhhh!?
soulmate wangu akilisoma naomba asikuelewe...hehehe


....Hahahahahah lol! madongo yote yatakayorushwa nitaomba yaelekezwe kwa muanzisha thread lol!
 
Ukiona tuko kimya ujue ni Conservative, siamini katika haki za wanawake.

labda na yeye ni wa hivyo.
Nakimbia nisije pondwa mawe bure.

Mmomonyoko wa ndoa umeanzia kwenye haki za wanawake.

Kwa mara ya kwanza nakuona Dada Mkuu ukiweka mpira kwapani...

Njoo bwana useme yanayokukereketa..

Au umeamua kuzira hata ndoa yenyewe??

Babu DC
 

....Hahahahahah lol! madongo yote yatakayorushwa nitaomba yaelekezwe kwa muanzisha thread lol!

Hapana Kaka,

Sheria za JF zinasema kuwa mwenye dhamana ni mwandishi!!

Nimeupenda sana mchango wako.....Hizo MBs, ....hakuna ambayo inawaelezea wale wachache ambao wanasikia hizo hadithi nje??
 
safi sana FF kumbe kwny haya mambo unaakili namna hii tofauti na kulee kwenye siasa........u made ur points very clear n loud.:violin:
 
unazidi kunifungua akili FF ,natamani na mm nipate wa kuoana naye lol.:busu
 
Hapana Kaka,

Sheria za JF zinasema kuwa mwenye dhamana ni mwandishi!!

Nimeupenda sana mchango wako.....Hizo MBs, ....hakuna ambayo inawaelezea wale wachache ambao wanasikia hizo hadithi nje??

Sijakupata Mkuu DC naomba ufafanue
 
usijali nimeisoma yote ,lol!kweli mapenzi ya tamthilia yanaharibu...jamani ya kina Alehandro tuwaachie kina Alehandro wenyewe na tamthilia zao.:ranger:
 
Sijakupata Mkuu DC naomba ufafanue

Umetaja tatu,

MBL
MBA
MBU,

Hakuna abbreviation inayotumiwa kwa wale ambao wako ecological (wanatesa kwa raha zao na kusikia hizi simuliz kwa wengine)??
 
...ila hilo la huyo aliyeolewa mara kumi na tano dahh?, miongoni mwa hizo kaolewa mara tatu na mume huyo huyo? ...anafaa kungizwa kwenye Guiness Book of Records...
Zilikuwa mara kumi na sita, na wanaume 13. Cha ajabu, mume wa mwanzo ambaye alilazimishwa na jamaa yake, mara ya mwanzo hawakukaa hata mwaka mmoja wakawachana. Badae akaolewa na waume wengine mara nne, mume wa kwanza akamwoa tena na kuishi pamoja miaka 10, wakawachana: Bibi akaendelea kuolewa tena na tena na tena hadi mara 7, mwisho akaja kuolewa na mume yuleyule wa mwanzo mpaka wakafariki wazee, kwanza bwana badae bibi. Cha ajabu, wakati bibi alikuwa anaolewa, bwana alikuwa anasubiri awachwe aoe tena. Very sad, hawakupata watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…