Ndoa yako inaingia migogoro mnashindwana na mkeo anaamua kuondoka lakini ukweli ni kwamba hukutaka aondoke,lkn ulipoanza kuhoji kana kwamba anachelewa Kurudi ndani unahisi ameanza kujihusisha na wanaume wengine,akapata sababu ya kuondoka huku akijisemea
"familia nalisha mwenyewe wewe huna kazi unategemea nitafute halafu na makelele juu!!
Anaamua kuwaita watoto wote watatu.....
Akisema twendeni....unamwita mkeo kwasababu unampenda unamwambia sikua na nia mbaya...kama MWANAUME Lazima nihoji,hebu usiondoke tuyamalize pls!
mke anakukazia anakwambia sitaki Mimi naondoka!
Unamuuliza mtoto mkubwa "Gift ,unaniacha nawewe?" mwanao kipenzi gift anakusaliti anawaita na wadogo zake wanamwandamia mama yao huku ukibaki na mshangao😮😮😮.
Unavumilia kukaa wiki bila familia,unatumia kila jitihada ili mkeo arudi lkn wapi! Unafunga safari uende kwa wakwezo na hawaonyeshi ushirikiano unarudi kwako bila mke.....usingizi hauji,chakula hakipandi,unabaki stress tupu.
Hujui wa kumuuliza na kumshirikisha yaliyokupata na hukuwa na kawaida ya kushirikisha watu wengine matatizo ya ndoa yako....na hukuwa na urafiki na watu wengine tangia ulipooa zaidi ya mkeo.kusema ukweli unapita kipindi kigumu Sana!!
Unafika mwezi,miezi miwili mwili umeisha, na kwasababu ya msongo wa mawazo uliokuwa nao unajikuta kwenye shida ya vidonda vya tumbo..... kila ukila chakula unatapika....
mwenye nyumba anajua mkeo yuko kwao kusalimia sawa na ulivyomwambia lkn wapangaji wenzio wanakutana na mkeo mjini kapendeza ni hatari!! Lkn hakuna anayekugongea mlangoni akuulize umeshindaje.
Baada ya miezi mitano unasikia mkeo kaolewa.
Unaishiwa nguvu......unadhoofu zaidi yaani wewe ni kushinda ndani tu.....wapangaji wenzako hawakuoni kutoka wala kuingia ndani ila mlango kwa nje haufungwi.....
kumbe tangia ulipoweka miguu juu ya meza umekaa juu ya kochi lako ukiwaza nini hatima ya maissha yako kumbe ulikata roho paleoale😟😟
Mwili wako ukaanza kujiozea,na kadri ulivyozidi kuoza ukakosa hata balance ya kukaa kwenye kiti hakuna anayejua (wanadamu hawana upendo) serikali za mitaa wanakuja kushtuka zimepita siku nyingi ndio wanaita polisi wanakukuta umekuwa mifupa....na mdomo wako ulionesha ulilia sana kabla ya kukata roho.
Any way niseme na walio hai maana wewe haupo nasi.......
Wanawake,ishini na waume zenu kwa utii na kwa upendo usio na unafiki na kwa kuvumiliana.
Haya maisha yanaenda kasi sana,hautaishi milele duniani....usimtendee mtu jambo usilopenda kutendewa.usiwe sababu ya mwenzio kulia na siku zake kufupishwa.....
Kuna wakati ndoa zinapita kwenye jua kali Sana....lkn fahamu jua litakoma saa za jioni zikifika......ukibahatika kupendwa pendeka hata pasipokuwa na kitu....na wanaume vile vile fanyeni kazi ili msiingie kwenye majaribu yasiyokuwa na ulazima!!
Philemon Kuhani Mwakalambo