Research Consultant
JF-Expert Member
- Dec 29, 2022
- 453
- 772
Wasalaaaam
Ndugu, jamaa na marafiki
Naamini mpo salama na majukumu ya kujijenga kiuchumi na kijamii yanaendelea
Mimi ni kijana niliyejiajiri, umri wangu naelekea katika third flow
Nina ndoto ambazo nimekuwa nikiziota kwa muda mrefu sasa na kiukweli zinanitesa sana na zinaniumiza sana, Naomba masaada wa kujuwa maana ya hizi ndoto ni nini na najinasuaje kutoka kwenye ndoto hizo
NDOTO YA KWANZA
Hii kwa hivi karibuni haijanijia sana ila imekuwa ikinitesa sana kila ninapoiota, huwa naota nadondoka kwenye korongo refuuuu sana, yaani ni refu kiasi ambacho najikuta na weweseka sana na ninaposhtuka nikiwa kitandani muda mwingine nakuta hadi jasho linanitoka. Hii ndoto imekuwa ikirudia rudia sana kiasi cha kuniogopesha sana hivyo natamani kujua maana yake ni nini na nifanyeje isiniijie tena
NDOTO YA PILI
Hii ndo kubwa kuliko na imekuwa ikijirudia sana na hata usiku wa leo nimeiota tena, huwa naota nipo na marafiki zangu wengi either wa shule ya msingi au sekondari katika mazingira ya shule tulizosoma. Wengine ambao nakuwa nao kwenye hizo ndoto sina mawasiliano nao na wala hatukuwuhi kuwa washkaji. Tupo mazingira ya shule either Darasani tunafundishwa au mazingira ya shule tukicheza. Muda huo tumevaa uniform za shule woote. Kuiota hii ndoto so shida shida ni inapojirudia rudia sana nahisi kuna alert napewa ila mimi naipuuzia kwa sababu sielewi ndoto hizi zina maana gani
Kwa wale wataalamu wa ndoto nawakaribisha sana mnieleweshe maana ya ndoto hizo ni ipi na nawezaje kuzishinda au nisiziote tena
Natanguliza Shukran